AIBU: Uwanja wa ndege wa Dar es Salaam wakosa umeme, ndege zashindwa kutua!

Duh, hii aibu kwa viongozi wetu, wameshindwa kutimiza malengo yao. Hayo ni maisha bora kwa kila mtanzania.
 
Habari za kuthibitika kutoka uwanja wa ndege wa kimataifa wa mwalimu Nyerere uliopo Ukonga Dar-es-Salaam hakuna umeme na generator yake haifanyi kazi hivyo wanatafuta jenereta nyingine wafunge ili kuwe na mawasiliano kwani tangu jioni ya leo hakuna ndege inayoingia wala inayotoka.. Wasafiri wa usiku huu wataondoka kesho saa tatu asubuhi..

poleni wasafiri mlioguswa na hili.
 
Ni jambo la aibu na kusikitisha.Ndege ya KLM imesimama KIA kwa masaa manne na muda si mrefu imeamuliwa abiria wapelekwe Arusha Mjini Hotelini mpaka kesho asubuhi watakapopelekwa Dar.
 
kwa nini watu mnakasirika wazungu wanavyotuita sisi ni MANYANI?
NGELEJA JUZI KASEMAJE?
 
Jibu rahisi la kisiasa litakuwa

Waige mifano ya migodi . Serikali imeshasema kila mwenyeuwezo wa kuzalisha umeme azalishe
 
  • Thanks
Reactions: Aza
Ni aibu kubwa sana kwa nchi lakini kama kawaida yetu si ajabu kuona viongozi wetu wakichekacheka tu! Hata mkuu wa nchi akiambiwa nae ataishia kusikitishwa kama mimi tu. Hawezi kufanya lolote. Ndiyo Tanzania hiyo inayojiandaa kwa mabilioni ya fedha kusherehekea miaka 50 ya uhuru. Upuuzi gani huu!!!
 
Kila uchaguzi una matokeo kama vile kupanda mbegu kuiivyo na matokeo. Iweje waliopanda washangazwe na mavuno yao au wale waliochagua na chaguo lao?
kuna mbegu zingine zinaendelea kupandwa huko
attachment.php
attachment.php
 
Umeme wa Tanzania ni mradi wa mtu,kama umeme ukiwa wa uhakiki watakosa ulaji,kama huamini hili fuatilia mikataba yote ya kufua umeme iliopo hapa nchini Ushangae.
 
Ngeleja alisema mwisho wa mgao ni juzi cha kushangaza mgao umeongezeka zaidi,we dont care about uchumi wetu and more to come....
 
Sure,,,,,,mgao kwa sasa ni mkali sana,tangu atangaze naona ndo hali imekuwa ngumu
Ngeleja alisema mwisho wa mgao ni juzi cha kushangaza mgao umeongezeka zaidi,we dont care about uchumi wetu and more to come....
 
Asubuhi Precision wana abiria foleni hadi nje,umeme ulirudi saa 10 lakini still bado unakatika
 
Mambo yananipa hasira sana,hadi inafkia sehemu unawaza mambo mengi ya hatari.

Ukisikia mtu kajtoa mhanga chanzo ni mambo kama yanayoendelea Tanzania.

VIONGOZ WETU WAONGO SANA MTU NA KICHWA KUBWA TUMBO KUBWA UNAENDA IGUNGA KUADAA WANANCH,WANANUNUA MAGARI YA KIVITA KUZUIA MAANDAMANO MELI IMEZAMA WANASHDWA KWENDA KUOKOA WATU WANATUDANGANYA KAMA WATOTO,UMEME TATIZO WENYEWE WANAKULA NA KUWEKEANA POSHO NONO.KUMBUKA KUFA NI LAZMA NA WALA SI OMBI
 
Jana nimeshuhudia aibu ambayo sijawahi kushuhudia sehem nyingine. Umeme ulikatika uwanja wa JNIA na kusababisha kushindwa kutua au kupaa kwa ndege hivyo safari zote zilizokuwa zifanyike jana usiku zikafutwa.

This is exclusively made in Tanzania.
 
Back
Top Bottom