Hasara
Senior Member
- Dec 29, 2006
- 138
- 9
Aibu tupu Dodoma
2007-11-07 15:40:07
Na Mary Edward, Dodoma
Licha ya kinyang`anyiro cha uchaguzi wa Chama cha Mapinduzi CCM, kumalizika salama, lakini aibu zilizotokea huko zimebaki kuwa simulizi katika mji mzima wa Dodoma.
Habari za uhahika zilizolifikia gazeti hili zinadai baadhi ya wapambe wa washindi wa nafasi za Ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, NEC, wamefanya aibu za aina yake wakati walipomwagika mitaani kusherehekea ushindi wa watu wao.
Inadaiwa baadhi yao walizidiwa na kilevi, na kujikuta wakifanya vioja vitupu ambavyo haviendani kabisa na hadhi zao.
Imedaiwa kuwa katika baadhi ya maeneo, baadhi ya vigogo na makada maarufu wa chama hicho walilewa chakari kiasi cha kushindwa kutembea na wengine kutembea peku huku wamebeba viatu mikononi.
Wengine inaelezwa kuwa walikodi bar nzima na kulipia gharama zote ili kila mwenye kujisikia kunywa na kula nyama choma, afanye hivyo kwa kadri ya uwezo wa tumbo lake.
Mashuhuda wanasema ofa hiyo ya mipombe iliyotoa fursa kwa kila mtu, iliwafanya baadhi ya wapambe kulewa chakari na wengine kujikuta wakifanya mambo ya aibu.
Mwandishi wa PST alishuhudia baaadhi ya wapambe wakiwa wamelewa chakari huku wakiwa bado wamejipamba kwa mabango ya kuwapigia debe watu wao.
Hata hivyo, mwandishi amebaini vilevile kuwa wengi kati ya waliokuwa wakisherehekea kupita kiasi ni pamoja na wale walioshinda kinyang`anyiro hicho kwa mara ya kwanza, baada ya kuibuka vinara kufuatia ushindani mkali uliokuwepo.
Hata hivyo, wakati baadhi ya wapambe wakifanya vurugu kutokana na furaha iliyowakumba, hali ilikuwa tofauti kwa walioshindwa ambao wengi walionyesha dalili za kulia hadharani, akiwemo kada mmoja maarufu aliyekuwa akiwania nafasi kupitia Umoja wa Wanawake wa whama hicho, UWT.
SOURCE: Alasiri