Aibu! Serikali yakiri haina takwimu za ajira

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
234
My Take:
sasa sijui serikali hii imekaaje. Picha inayopatikana ni kwamba hufanya sensa kila miaka kumi kuwaridhisha wafadhili wanaotoa misaada. Mwaka jana Kapuya aliliambia Bunge serikali ilikuwa imetengeneza ajira 1.3 millioni tangu JK ashike nchi 2005! Katika kampeni za uchaguzi, Dr Slaa alihoji serikali itoe orodha hiyo ya 1.3 millioni, katika sekta zipi.

Hakika waziri Kapuya alikuwa muongo kupindukia na serikali kwa ujumla ilishindwa kumjibu Dr Slaa kwa hoja hiyo na badala yake kumtukana matusi ya nguoni.

Sasa soma hii aibu nyingine.




Tanzania haina takwimu za ajira

Waziri wa Kazi na ajira Gaudensia Kabaka katika mkutano na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam jana.

Serikali inakabiliwa na upungufu wa utoaji taarifa za soko la ajira, hali ambayo inatokana na kukosekana kwa takwimu sahihi katika sekta hiyo.

Hata hivyo, serikali kupitia Wizara ya Kazi na Ajira imekuwa ikifanya jitihada kubwa katika kushughulikia suala hilo, ili iweze kupatikana takwimu sahihi kwa maendeleo ya nchi.

Hayo yalisemwa na Waziri wa wizara hiyo, Gaudensia Kabaka, katika mkutano wake na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam jana.

Alisema ili kufanikisha hilo, wizara yake imekuwa ikiomba kupitia wadau wengine kuingiza viashiria vichache vya masuala ya ajira katika tafiti zao.

“Serikali kupitia wizara yangu, imekuwa ikikabiliwa na upungufu wa taarifa sahihi kuhusu soko la ajira za kuwezesha maendeleo ya nchi, lakini unaendelea kuomba wadau mbalimbali kuingiza viashiria vichache vya masuala ya ajira katika tafiti zao… mfano utafiti wa mapato na matumizi ya kaya na wa viwanda” alisema Waziri Kabaka.

Alieleza kuwa, wizara hiyo kwa kushirikiana na Shirika la Kazi Duniani (ILO), Vyama vya waajiri na waajiriwa, imeamua kwa dhati kushughulikia suala la upatikanaji wa taarifa sahihi za soko la ajira.

Kabaka alisema kwa kuweka mfumo wa kitaifa wenye ufanisi na wa gharama nafuu utawezesha upatikanaji wa taarifa sahihi za soko la ajira kwa wakati na mara kwa mara.

“Mchakato umeshaanza kwa kufanya majadiliano na wadau na moja ya mambo yaliyokubalika na wadau ni kuandaa mwongozo wa kitaifa kuhusu ukusanyaji, uchambuzi na utoaji taarifa za soko la ajira na ifikapo Juni mwaka huu mfumo huu utaanza kutumika” alisema Waziri huyo.

Aliongeza kuwa; “Umuhimu wa taarifa sahihi za soko la ajira unaweza kujitokeza kwa ngazi ya mtu binafsi, kitaifa, kwa wataalam na pia katika ngazi za kimataifa kulingana na mahitaji, ikiwemo kusaidia serikali katika maamuzi na kuridhia mikataba mbalimbali kama ile ya soko la pamoja la Afrika Mashariki, kufungua mipaka ya ajira kwa kujua fani na ujuzi unaokosekana nchini” alisema Kabaka.

Aidha, alisema kutokana na ukuaji wa haraka wa nguvu kazi ya taifa, maendeleo ya sayansi na teknolojia hasa habari na mawasiliano, sera ya ajira iliyopo imeonekana kutokidhi baadhi ya mahitaji na mabadiliko hayo.

CHANZO: NIPASHE
 
Ila unajua ahadi ya ajira milioni moja ya JK ilikua so ambiguous na vigumu kupimika. Una pima vipi ajira zilizo tengenezwa na serikali? Je ni ajira zinazo tolewa moja kwa moja na serikali au hata MF1 nikianzisha kampuni hizo ajira zita hesabiwa na serikali? Mimi nadhani ni vigumu sana kupima ajira zinazo tokana na serikali unless ni ajira za moja kwa moja serikalini (iwe serikali kuu au serikali za mikoa na halimahsauri za jiji).

Ila pia ina shangaza kwamba serikali haipimi mafanikio yao wenyewe. Kama wewe uliahidi ajira X kwa nini usiangalie ni ajira ngapi zime patikana? Kama zime patikana zaidi ya X uangalie nini kili fanyika kilicho leta ajira hizo ili sera hizo ziendelezwe na kama haukufikia idadi hiyo ni kwa nini haukufika.
 
Back
Top Bottom