Aibu rais kulala hadharani!

anagalieni rais wenu anavyolala hadharani
2722d1224755716-aibu-rais-kulala-hadharani-jknauchovuwatrip.jpg

Wanaobisha walete video jamani....Hapo Mh Rais anauchapa jamani.
Kwasababu mikono ni kama ime hang hivi na hivyo inaonyesha hakuwa kwenye movement yoyote ile.
Angalia huo mkono wake wa kushoto kuanzia kwenye kiganja unavyoning'inia...Wale wanaodai alikuwa kwenye movement basi ni wazi si kweli cause hakuna sapoti kwenye mkono wake ili kuweza kusapoti movement ya mwili ama hata kifua na kichwa.
Hata ukiangalia wengine wote wako aware...Ni wazi alikuwa amechoka.
 
Kuongoza Nchi sio lelemama eti. Huyu Rais wetu ni MCHAPAKAZI sana. Sema tu humu ndani bado kuna watu wana "Marais" wao mioyoni mwao hata baada uchaguzi kukamilika tangu 2005!
 
Jamani,hebu sasa tumwache Raisi wetu apumnzike.
Pale alikuwa katika kutafakari nakuona anawezaje kuongoza nchi na kutuletea maisha bora.Si mnaona mafanikio.
 
Hakuna aibu yeyote...Mheshimiwa ni binadamu kama sisi na lazma achoke. Pia hatuna uhakika wa kwamba kweli alikuwa amelala, labda alikuwa anainama tu. JK ni kipenzi cha wananchi, wanaemtia doa ni wafuasi wake!
 
Hakuna aibu yeyote...Mheshimiwa ni binadamu kama sisi na lazma achoke. Pia hatuna uhakika wa kwamba kweli alikuwa amelala, labda alikuwa anainama tu. JK ni kipenzi cha wananchi, wanaemtia doa ni wafuasi wake!


Kama jk ni kipenzi cha wananchi, inamaanisha wananchi wake ndio wafuasi wake. Na kama wanamtia doa JK ni wafuasi wake... basi wanamtia doa ni wananchi ambao ndio wafuasi wake. Maskini.... kazi anayo.
 
Kama jk ni kipenzi cha wananchi, inamaanisha wananchi wake ndio wafuasi wake. Na kama wanamtia doa JK ni wafuasi wake... basi wanamtia doa ni wananchi ambao ndio wafuasi wake. Maskini.... kazi anayo.

Rais anachapa kazi mpaka namuonea huruma.Sasa hivi yuko Tabora akijaribu kuifungua Tabora kwa mawasiliano ya barabara ili iunganishwe vema na Mikoa ya jirani na nchi kwa ujumla.Nani aliyewahi kuitafutia maendeleo mikoa ya Tabora na Kigoma kama anavyofanya JK?

Yuko mara huku mara kule akifanya kazi za wananchi.Kiongozi asiyekuwa na jazba,hamaki na inavyoelekea hana mpango wa kufanya ukandamizaji wa mawazo ya watu kama wale waliomtangulia.Ukiandamna andamna ,onesha hisia zako na Serikali itazifanyia kazi.

Hakuna kurudisha wanafunzi nyumbani kwa FFU.hakuna kupiga mabomu kwa viongozi wa upinzani,hakuna mtu aliyewekwa lupango kwa mawazo yake ya kisiasa.Huyu ni JK kipenzi cha Wananchi.

Kama kalala au hakulala kwenye msiba bado ni yule yule Jk mchapakazi ambaye kila tukio kwake ni headline!! Ni Rais ati!!Mara kaibiwa laptop! News hiyo,mara kalala! news hiyo!!Mke wake akienda salon nayo news.mtoto wake akienda sokoni news nayo!
 
....Aliona mende pale chini alipokaa so alikuwa anajaribu kumkanyaga ili asilete rabsha kwenye kadamnasi.
 
....Aliona mende pale chini alipokaa so alikuwa anajaribu kumkanyaga ili asilete rabsha kwenye kadamnasi.

Kweli mkuu umenena, hakuwa mende alikuwa sisimizi ,tena amem'bana kwa miguu yote miwili ili asifurukute na kuleta madhara..teh teh teh..

Haya leteni hoja nyingine sasa..
 
hajalala, hapa alikuwa msibani.

pengine alikuwa anazungusha shingo tu kwa staili
 
..nilisoma kitabu cha "the making of african statesman:moi"

alielezea ratiba yake kama mtu anayeamka mapema zaidi na kulala late zaidi .....na hakuna mzaha kati kati.....

Saa 10.00 alfajiri kila siku huamka na kusali kwa dk 30.....
Saa 10.30 kamili hufanya mazoezi ya viungo [dk 30]
saa 11 kamili huoga na kuvaa [dk 30]
saa 11.30 hupata kifungua kinywa [uji na maziwa]..ets na kuelekea ofisini
saa 12 kamili bendera ya jamuhuri inapopandishwa yeye tayari huwa ofisini
na kazi ya kwanza aliyokuwa akifanya ni kuwasiliana na wakuu wa ulinzi na usalama kupata taarifa,,...

Baada ya hapo ratiba yake ya kazi za ofisini hukamilika saa 12....hurudi nyumbani na kupumzika kidogo ...saa mbili kamili hupata mlo..na kuendelea na vikao na wasaidizi wake hadi saa 4 usiku au 5..baada ya hapo hupata muda wa kusoma taarifa ya kazi zake za kesho aliyoandaliwa na msaidizi wake....

Mara nyingi inaelezwa kuwa alikuwa akilala saa 7 hadi 8 kila siku..........na wala haikuwa ajabu kuwa na miadi ya kikazi hadi saa 6 usiku.....

Nadhani ratiba kama niliyoieleza hapo juu ni kielelezo tu cha ratiba za viongozi waliodhamiria ....haitatofautiana na ya mwalimu...,na wengine kama hao.....

Tatizo na viongozi ambao ikifika usiku kama saa hizi badala ya kufanya tafakari ......huyoo anajiiba kwenda kariakoo kucheza dhumna na maswahiba ....ambao hawana la kumshauri..au kona kona!!

Phil umeniacha hoi na hiyo ratiba ya "baba" Moi. Kumbe ndio maana aliweza kuwaweka "kiganjani" wakenya bila kufurukuta kwa miaka 24, na hata sasa hivi nasikia bado yeye ndio rais by proxy kupitia kwa Mwai Kibaki a.k.a Moi Kabaki!
 
Kwanza napinga kuwa alikuwa amelala. Kama ni msibani ni jambo la kawaida mtu kusikitika na akaposi anavyotaka. Yeye naye ni binadamu kama wewe. Kwanza nampa hongera kwa umri aliokuwa nao bado ni active na anafanya mambo mengi japo wengi tunaona hafanyi kitu. Mi nafikiri kuwa washauri wake au wataalam wake ndo waku blame hapa kuwa pengine hawamshauri ipasavyo? Au pia washauri/wataalam wake wanafanya hivyo delibarately ili kumwangisha aonekane hafai.

Kufanikiwa kwa rais yeyote yule kunatokana na wale wataalaam wanaomshauri hata kama angekuwa na akili na utendaji kiasi gani.

Fahamu kuwa Rais ni public face na majukumu ya kiuwakislishi rather than kiutendaji ni mengi mno. Hivyo watendaji wake na washauri wanatakiwa wawe smart sana.

Hapa mi naona ajipange upya kuhusu washauri ni all spheres(kisiasa, kijamii na kiuchumi).
 
Mwisho wa yote tukumbuke kuwa naye ni Binadamu na anaweza kupitiwa na usingizi, kama kweli alikuwa amelala!

Niliwahi kuona watu wanalala usingizi kwenye kumbi za disco bila hata kushutuliwa na makelele ya hiyo miziki!
 
Si ajabu alikuwa anaota yuko Jamaica kwenye mimbea..
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom