Aibu polisi! Kamati ya Kova haijamhoji hata mtu mmoja kuhusu kutekwa kwa Dr ulimboka!

Kova ni kama yule mfalme aliyesema amevaa nguo nzuri anapita mitaani kwa maringo mpaka katoto kaliposema "ona mfalme yuko uchi!" Kuna siku ataabika.
 
Mimi nataka said Kubenea ahojiwe , hizo habari za uchochezi anazitoa wapi?
Hata Said hawatamhOji kwa sababu anaujua ukweli kama aujuavyo KOVA.NDUGU ZANGU DUNIA HII NI KIJIJI UKIINGIA KWENYE MITANDAO YA SIMU NI RAHISI SANA KUPATA MAWASILIANO YOTE YA DR ULIMBOKA KABLA YA KUTEKWA KWAKE NA HIO NDO KAZI ANAYOTAKIWA KUIFANYA KOVA.NA SERIKALI INAPOKUWA KIMYA KAMA ILIVYO SASA HIVI INATOA MWANYA KWA WATU KUUPATA UKWELI PASI NA SHAKA NA WENGINE KUHISI TOFAUTI KWANI SERIKALI YAO IMESHINDWA KUWAPA TAARIFA ZA KIUCHUNGUZI NA KUPIGA DANADANA KWA JAMBO AMBALO KIUPELELEZI NI RAHISI SANA.WAINGIE KWENYE MTANDAO WA SIMU WAFUATILIE WALIOKUWA WANAWASILIANA NAE WOTE.
 
............mkuu unachekesha kweli, polisi wako sahihi ni sawa na kuuliza mdomo wakati wa kula, teh teh teh
 
Walijua wameshamaliza kazi na jamaa ni marehemu, kumbe Mungu mkubwa sasa wameumbuka hawana pa kutokea. Polisi magamba, Usalama wa mafisadi, TAKUKURU ni majanga mengine ya Taifa kama lilivyo janga la "kumchagua" tena Kikwete 2010.


Yaani serikali wamevuliwa nguo hadharani; kauli zao sasa aibu kwao.


"Baba yetu uliye mbinguni........ Duniani kama Mbinguni""


Tehe tehe tehe!!!!!!!!!!!!!

Wanajisahau kuwa Mbinguni ya waovu ni hapa hapa Duniani. Lazima Mungu awaumbue mwaka huu tutaona mengi.



MIZAMBWA
NABII MTARAJIWA!!!
 
Serikali makini haitakiwi kuweka ghadhabu inaposhindwa hoja. Serikali makini daima hukubaliana na lile lililo la ukweli.
 
hapo kwenye red hata mimi nimejiuliza sana! Ninamashaka na huo umri!?

hiyo picha sio ya rama! ni ya mkurugenzi mkuu wa usalama wa taifa! rama sio mkongwe ivyo! huyo jamaa kaitoa tu kwenye gaazeti mojakwa moja! nashangaaa hawa mwanahalisi wana mpaka VRC,MOBILE NO ndo wakose picha ya rama?
 
Yeyote aliyempa mkong'oto Ulimboka anastahili kila sifa.

Wewe lazima utakuwa MUISLAMU tu! Kwa Mkristo wa Kweli Soma 1 Wakorintho 13:4-13 love does not delight with evil.... and the Bible says the Love of God (AGAPE) has been sge abroad upon our hearts by the Holy Spirit... true Christians wamenisoma...
 
usijali, kamati iko bize, inazunguka makanisani kusikiliza watu wanaotubu!!! Kwa lugha ya kwetu kova = konokono
 
Ushahidi upo lakini hakuna wa kumhoji.. Huwezi kuhoji usalama wa taifa... Tangu lini umesikia serikali ya marekani inahoji FBI huwezi itakula kwenu
 
Ushahidi upo lakini hakuna wa kumhoji.. Huwezi kuhoji usalama wa taifa... Tangu lini umesikia serikali ya marekani inahoji FBI huwezi itakula kwenu

kaka kwenye red hapo taratibu.....usilinganishe bahanuzi na messi..please.
 
Mimi nataka said Kubenea ahojiwe , hizo habari za uchochezi anazitoa wapi?

Siyo kuhojiwa, Kubenea anapaswa kupelekwa mahakamani kwa kuchapisha habari za uchochezi. Huko ndo atajieleza alizipata wapi hizo habari.

Ujasiri wa kumkamata na kumhoji Kubenea haupo.

Wanajua akifika mahakamani ataanika vyote.

Ila wanachoweza kufanya ni kumpangia mkasa kama wa Ulimboka.
 
Wewe lazima utakuwa MUISLAMU tu! Kwa Mkristo wa Kweli Soma 1 Wakorintho 13:4-13 love does not delight with evil.... and the Bible says the Love of God (AGAPE) has been sge abroad upon our hearts by the Holy Spirit... true Christians wamenisoma...

Huyo shetani alikuwa anaitisha migomo wagonjwa zetu wanateseka, wanakufa, hawapati kuangaliwa, leo mnakuonea huruma? mnamuonea huruma nduli huyo mtoa roho za watoto wadogo? Ingekuwa sikatazwi kumlaani mtu basi huyo ningemtakia laana zote za dunia zimshukie kama bado hazijamshukia.

Nasema wazi kabisa, aliyempa mkong'oto huyo, yeyote yule, basi kafanya la maana sana. Sasa anaelewa kuumwa ni nini, yeye alikuwa hajui mtu akiwa mahututi na yupo kitandani anategemea wenzake inakuwaje anapowachwa bila kuhudumiwa.
 
Ujasiri wa kumkamata na kumhoji Kubenea haupo.

Wanajua akifika mahakamani ataanika vyote.

Ila wanachoweza kufanya ni kumpangia mkasa kama wa Ulimboka.

​Kama hawana huo ujasiri basi walilofanya linaonyesha ni kiasi gani wao ni dhaifu.
 
Back
Top Bottom