Aibu polisi! Kamati ya Kova haijamhoji hata mtu mmoja kuhusu kutekwa kwa Dr ulimboka!

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
233
Yule kamanda wa polisi mkereketwa Na 1 wa CCM, Suleman Kova, afanye weledi katika kazi yake kwa kuutangazia umma ile kamati yake ya kipolisi ya kuchunguza sakata la kutekwa na kupigwa kwa Dr Ulimboka imefikia hatua gani?

Iwapo aliona ni weledi kwake kuutangazia umma, tena kwa mbwembwe kubwa kwamba ameunda kamati ya kuchunguza sakata hilo, awe jasiri tena na mbwembwe kwa kutuambia amefikia hatua gani, amehoji watu wangapi nk nk.

Vidokezo vyangu vinaonyesha kamati hiyo haijamhoji hata mtu mmoja! Haijamhoji hata yule Dr Deo Michael aliyokuwa na Dr Ulimboka wakati yule Rama (aka Abeid) na mabaunsa wake walipomteka Ulimboka.

Jameni, tuseme kile cha kweli kabisa na cha haki, hii si aibu kubwa kabisa katika jeshi letu la polisi katika kukosa weledi katika kazi zake hasa kutetea haki na maisha ya watu?

Mtu pekee aliyehojiwa ni yule kichaa mmoja aliyedai 'kutubu' kwamba ndiye alihusika na baadaye yeye mwenyewe kukiri kwamba huwa ana tabia ya kusema hovyo.
 
Watahoji nini? Watekaji wote wa Ulimboka wametoka Ikulu. Unadhani Kova hapo atakuwa na ubavu? Walichojaribu kufanya
ni cover up lakini nayo inawaripukia usoni.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Wametumia mbinu ya kifisadi eti swala liko mahakamani no right 2 discuss
 
Kwa kukosa majibu kwa umma sasa serikali inafungia magazeti kwa sababu dhaifu!
 
Yule kamanda wa polisi mkereketwa Na 1 wa CCM, Suleman Kova, afanye weledi katika kazi yake kwa kuutangazia umma ile kamati yake ya kipolisi ya kuchunguza sakata la kutekwa na kupigwa kwa Dr Ulimboka imefikia hatua gani?

Iwapo aliona ni weledi kwake kuutangazia umma, tena kwa mbwembwe kubwa kwamba ameunda kamati ya kuchunguza sakata hilo, awe jasiri tena na mbwembwe kwa kutuambia amefikia hatua gani, amehoji watu wangapi nk nk.

Vidokezo vyangu vinaonyesha kamati hiyo haijamhoji hata mtu mmoja! Haijamhoji hata yule Dr Deo Michael aliyokuwa na Dr Ulimboka wakati yule Rama (aka Abeid) na mabaunsa wake walipomteka Ulimboka.

Jameni, tuseme kile cha kweli kabisa na cha haki, hii si aibu kubwa kabisa katika jeshi letu la polisi katika kukosa weledi katika kazi zake hasa kutetea haki na maisha ya watu?

Mtu pekee aliyehojiwa ni yule kichaa mmoja aliyedai 'kutubu' kwamba ndiye alihusika na baadaye yeye mwenyewe kukiri kwamba huwa ana tabia ya kusema hovyo.

Mkuu unanifurahisha... Ulitaka wahoji nini wakati ukweli wote wanaujua wao tena zaidi ya ujuavyo wewe?
 
Mtekaji ni ikulu sasa kova anaweza kumhoji kikwete kwa utekaji wa dr.uli?.muulize said kubenea atakwambia
 
Mimi nataka said Kubenea ahojiwe , hizo habari za uchochezi anazitoa wapi?
 
many Tanzanians do not care about HUMAN DIGNITY and have turned life to "...ni bora mkono uende kinywani".
...just telling lies to public on daylight!!!
 
Walijua wameshamaliza kazi na jamaa ni marehemu, kumbe Mungu mkubwa sasa wameumbuka hawana pa kutokea. Polisi magamba, Usalama wa mafisadi, TAKUKURU ni majanga mengine ya Taifa kama lilivyo janga la "kumchagua" tena Kikwete 2010.

Watahoji nini? Watekaji wote wa Ulimboka wametoka Ikulu. Unadhani Kova hapo atakuwa na ubavu? Walichojaribu kufanya
ni cover up lakini nayo inawaripukia usoni.
 
Mhhh, hii kali.

Hapa ni Hemed Msangi akiwa na Kova.....
_MG_9760.JPG
Na huyo mama hapo ni nani?

Watahoji nini? Watekaji wote wa Ulimboka wametoka Ikulu. Unadhani Kova hapo atakuwa na ubavu? Walichojaribu kufanya
ni cover up lakini nayo inawaripukia usoni.
 
Kubenea kati mchanga kwenye msosi kabla haujaiva....the food was half cooked.:A S-baby:
 
kikwete apimwe DNA! labda si mdanganyika! sijahi ona serikali ya kipuuzi kama hii!
 
Mi nadhani Kamati yake hiyo haina haja ya kuhoji mtu yeyote, sababu kwaza imegundua kwamba kila mtu anaujua ukweli wa nini kilitokea na sababu zake, lakini pia wameshatambua kwamba wamempata mtu wa kudanganyia tayari na wamekwenda haraka sana kumpeleka mahakamani na "USHAHIDI WOTE KABISA " wanao kwamba ni "MKenya". Unajua inakera sana kuwauliza watu "Ati leo ni Jumapili?" wakati inajulikana wazi kwamba leo ni Jumanne na watu wako kwenye shughuli zao na wala hawakwenda kanisani. Kwa hiyo mkuu, wako sahihi hao, bora pesa waliyopewa kwa kazi hiyo wamalizie mabanda yao kupaka rangi kwa sababu ripoti imekamilika anyway. Hii ndiyo Bongo.
 
Hawa watu ni WACHEZAJI wazuri sana wa FILM.

Anaweza kuwa mwema sana kwako ila siku ikifika akumalize, hata kama ulikuwa Mama watoto wake.... Utaishia Pande.

Halafu atarudi kulala kama hakuna kilichotokea na mwisho kuanza KULIA KWA UCHUNGU kuwa Majambazi yameuwa Mke wake.
mamamama huyo ndiye rama?? hebu nijuzeni basi, ni wa kumuogopa kuliko ebola!
 
Back
Top Bottom