Aibu nyingine ya serikali: Haina pesa kuendesha mitihani ya Taifa kidato cha pili mwaka huu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Aibu nyingine ya serikali: Haina pesa kuendesha mitihani ya Taifa kidato cha pili mwaka huu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by DT125, Nov 4, 2011.

 1. D

  DT125 JF-Expert Member

  #1
  Nov 4, 2011
  Joined: Oct 19, 2011
  Messages: 203
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  Taarifa kutoka kwa walimu wakuu wa shule za sekondari na wasimamizi wa mitihani wa Kanda ya Mashariki iliyofanyika jana katika shule ya sekondari ya Kilakala, wameelezwa kuwa TAMISEMI wametoa pesa kidogo sana ambazo hazitoshelezi uendeshaji wa mitihani hiyo. Hata wanasema hao walikaa kwenye semina hiyo hata bila ya kupata maji ya 200 ya kunywa, chai wala chakula.

  Wakuu wa shule za Manispaa wameelezwa kuifata mitihani hiyo kwa usafiri wa kujitafutia wenyewe walielezwa na Afisa Elimu Manispaa hiyo kuwa hana pesa ya mafuta kusambaza mitihani hiyo. Hakutakuwa na pesa za kulipa wasimamizi wasaidizi na wakuu wa shule kutoka serikalini.

  Dalili zinaonesha kuwa usiri wa mitihani huenda ukawa mdogo sana.

  Huenda ikavuja sana.
   
 2. Puppy

  Puppy JF-Expert Member

  #2
  Nov 4, 2011
  Joined: Oct 6, 2011
  Messages: 2,267
  Likes Received: 653
  Trophy Points: 280
  Tutafika Tu
   
 3. F

  FredKavishe Verified User

  #3
  Nov 4, 2011
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 1,090
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Ndo tanzania hiyo kikwete yuko bze kwenda kubembea'pinda hana sauti'membe na ghadaf na ushoga'mkullo hajui kwanin thaman ya sh inaporomoka'sitta yuko bize na visasi'shukuru kawamba kasema serikal haina hata ela za mikopo kwa watz'spika wa bunge yuko bize na cdm'nadhona yuko bize na lema'
  hakuna hata kiongoz mmoja wenye interest na taifa
   
 4. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #4
  Nov 4, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,921
  Likes Received: 453
  Trophy Points: 180
  Natabir mitihani hiyo itafanyika ndani ya siku 3 tu yote ishaisha, si uliona form 4, ndani ya wiki tu madent mguu juu, hamna pesa za kuwalipa wasimamizi. Anyway tutafika tu
   
 5. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #5
  Nov 4, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,376
  Trophy Points: 280
  Uk wasitishe hiyo misaada tuone kama tuna uwezo wa kufikiria nje ya misaada
   
 6. Pelekaroho

  Pelekaroho JF-Expert Member

  #6
  Nov 4, 2011
  Joined: Sep 15, 2010
  Messages: 1,502
  Likes Received: 102
  Trophy Points: 160
  Inashangaza na kusikitisha kwa wakati mmoja, huwa najaribu kumfuatilia kwa ukaribu saana naibu waziri wa elimu mheshimiwa Philip Mulugo anapofanya ziara zake kama mwenyewe anavoziita za kushitukiza, kuna wakati alikwenda mitaa ya wazo hill, kule mitaa ya kiwanda cha cement akafika katika shule na kuanza kuchukua mahudhurio ya waalimu ambao wameingia darasani na ambao hawakuingia darasani, juzi kati hapa kafungia shule moja ipo Sinza nasikia walikuwa wanatumia mtaala wa Kongo na medium of instruction ni Kifaransa, fine, namsifu saana kwa kazi hiyo, lakini kwa mtizamo wangu mimi hizo ni kazi za mkaguzi wa elimu wilayani na au Mkoani pia Kanda.

  Waziri alipaswa kuhakikisha kuwa maandalizi ya mitihani yanafanyika vizuri kwa sababu mitihani ndiyo upimaji au mrejesho wa ubora wa kazi inayofanyika katika kipindi fulani cha masomo, mitihani kama ya kidato cha pili au cha nne inafanyika mwisho wa mwaka.

  Kwa watu walio makini utayarishaji wa mitihani unaanza mara usajiri wa watakaofanya mitihani unapomalizika, gharama na mahitaji ya mitihani inafahamika, zaidizaidi ni uzembe na kutowajibika. Yapo masuala muhimu ambayo yangepaswa kushughulikiwa na Waziri, waalimu wanadai malimbikizo ya mishahara, pamoja posho mbalimbali ambazo ni stahili zao, wapo watu hawajapandishwa madaraja yao inavostahili.

  Zipo shule ambazo zinatoza ada na michango mingine kwa dola ya Marekani (wakati serikali ishasema malipo yote yafanyike kwa pesa ya kitz), zipo shule zimeajili waalimu kutoka nje ya nchi na hawana vibali vya kufanya kazi nchini au hawapo nchini kihalali, na haya yote yanafanyika wakati tunasherehekea miaka 50 ya uhuru.

  Mwalimu alisema ili tuendelee tunahitaji watu, siasa safi na uongozi bora. Leo wao wanaita Utawala bora, kweli tunatawaliwa na sio kuongozwa kama ambavyo mwalimu alipenda iwe. Tafakali Chukua Hatua!
   
 7. F

  FJM JF-Expert Member

  #7
  Nov 4, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  UK wakisitisha misaada yote tutakula majani - haina ubishi!
   
 8. Sigma

  Sigma JF-Expert Member

  #8
  Nov 4, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 5,015
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Sherehe za miaka 50 ya uhuru.....
   
 9. mama D

  mama D JF-Expert Member

  #9
  Nov 4, 2011
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 1,755
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Namsubiri Faiza Fox atoe maoni yake.
   
 10. kaburungu

  kaburungu JF-Expert Member

  #10
  Nov 4, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 1,599
  Likes Received: 2,455
  Trophy Points: 280
  Labda pesa zimeisha kwa sa7bu zilitumika kusomeshea kaka zao watatu wa TCRA...
   
 11. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #11
  Nov 4, 2011
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 8,998
  Likes Received: 582
  Trophy Points: 280
  Ikivuja tutaiweka hadi JF na kwenye FB watoto wasome majibu ili wasisumbue vichwa vyao, wakimaliza watakuwa viongozi wetu baadae maana nina hakika vyuo vikuu watafika na madesa watayakuta huko.
   
 12. mwakaboko

  mwakaboko JF-Expert Member

  #12
  Nov 4, 2011
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 1,841
  Likes Received: 253
  Trophy Points: 180
  Huyo FF mambo mazito kama haya hayawezi kwa kuwa hayajadiliwi kwenye vijiwe vya kahawa
   
 13. Manumbu

  Manumbu JF-Expert Member

  #13
  Nov 4, 2011
  Joined: Oct 28, 2009
  Messages: 1,751
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Sisi ni wa kuthubutu bwana...tutaweza tu na tutasonga mbele...hata kama ni kwa kuua viwango, na kuzamishana chini...hao ndio sisimmmm!!!
   
 14. Zinedine

  Zinedine JF-Expert Member

  #14
  Nov 4, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 1,189
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Vipi, na ya form six haitofanyika nini ili vijana wetu wapewe Div. 1 wote ili wende Udom?
   
 15. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #15
  Nov 4, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,468
  Likes Received: 4,127
  Trophy Points: 280
  Hii sasa ni balaa, mbona pesa za kusherehekea miaka 50 ya uhuru zipo?
   
 16. T

  Tata JF-Expert Member

  #16
  Nov 4, 2011
  Joined: Dec 3, 2009
  Messages: 4,729
  Likes Received: 645
  Trophy Points: 280
  Pole sana FJM inaonekana wewe ni mhanga wa hii imani iliyojikita serikalini na CCM kuwa bila kuomba misaada kwa hawa wazungu/wachina/waarabu hatuwezi kuishi kama nchi. Mimi naamini kuwa kama kuna jambo moja ambalo nchi hii inahitaji sana kwa sasa ni kwa hawa wanaoitwa wafadhili kuacha mara moja kutoa hiyo inayoitwa misaada ili tutumie kidogo vichwa kupata suluhu ya matatizo yetu badala ya kuendelea na mtindo wa sasa wa kutumia masaburi na matumbo yetu kufikiri huku tukitegemea kupewa pesa za bure na hawa wakoloni mamboleo.
   
 17. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #17
  Nov 4, 2011
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Ninachokiona hapa ni kuwa demand na supply haviendani. Si kwamba hela zimepungua ukilinganisha na zamani bali shule na wanafunzi vimeongezeka zaidi ya mara 100 wakati ongezeko la hela ni mara 20 tu.
  Tunashukuru kwa kutuletea shule nyingi lakini pia tunawashauri wajipange vizuri kuzihudumia.
  Sina cha kuwasifu watangulizi wa serikali hii na shule zao chache zilizotufanya wengi wetu tuwe mbumbumbu na ndo maana hata sasa hivi tunaogopa kuingia kwenye East Africa federation.
   
 18. n

  nchasi JF-Expert Member

  #18
  Nov 4, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 525
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 45
  Pesa zote zimemegwa kwenda kwenye sherehe za miaka 50 ya UHURU. Hivyo ndo vipaumbele vya MAGAMBA bwana. Bora mabilioni yatumike kwenye sherehe, Elimu yenyewe ni ya hapa bongo ambayo haina tija, wakati watoto wa walio kwenye system wanasoma elimu bora ya gharama kubwa ambayo italeta tija kwenye familia zao. "TAFAKARI, CHUKUA HATUA"
   
 19. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #19
  Nov 4, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 17,966
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  Kazi kubwa kufanikiwa kwenye elimu,za ufisadi zipo.
   
 20. Mhadzabe

  Mhadzabe JF-Expert Member

  #20
  Nov 4, 2011
  Joined: May 20, 2009
  Messages: 1,643
  Likes Received: 710
  Trophy Points: 280
  Eti yakitokea ya kutokea lawama wanamegewa walimu. I hate u stu....p ...dy govnt.
   
Loading...