Aibu nyingine kwa TFF

WOWOWO

JF-Expert Member
Aug 3, 2011
590
430
Shirikisho la Soka nchini TFF limeendelea kuzoa aibu tupu kwa Timu ya Taifa (Taifa Stars) kushindwa kusafiri kwenda Sudan kukipiga na Timu ya Taifa ya nchi hiyo kutokana na kuchelewa kutafuta ticket kwa ajili ya usafiri wa wachezaji.Mbaya zaidi mechi hiyo iko kwenye Calendar za Fifa na inatambuliwa na shirikisho hilo la kabumbu duniani.

Hii sasa ni aibu ya tatu kwa shirikisho hilo katika kipindi cha mwaka mmoja.Ya kwanza ni ile ya Kutokuimbwa wimbo wa Taifa kwenye mechi ya kimataifa dhidi yetu na Morocco wakati JK akiwa Mgeni rasmi na ya pili ni ya Kukatika kwa umeme kwenye mechi ya Fainali ya Kagame Castle Cup kati ya Simba na Yanga.

Ni kama tumerogwa vile kila kitu tunaboronga.Timu ya Taifa imeshuka hadhi kwa sasa hata Friend mechi za kimataifa imebaki ya kuomba kucheza na Palestina,Jordan.

Source: Magazeti ya Leo.
 
Back
Top Bottom