The Invincible
JF-Expert Member
- May 6, 2006
- 6,006
- 3,275
Hivi kweli Tanzania haina mzalendo yeyote mwenye sifa za kuwa mshauri wa viwanda mpaka tupate kutoka Japan? Au ndio kuomba fedha kwa njia mbadala? Nasikia kichefuchefu kwa hii tabia ya ombaomba. Vichwa vyote vya hapa JF kwa mfano, pasingekosekana walau watano wenye sifa hiyo.
Hii habari hapa chini nimeitoa Tanzania Daima.
Tanzania yapata mshauri wa viwanda toka Japan
na Tamali Vullu
SERIKALI ya Japan imeipatia Tanzania mtaalam mshauri wa masuala ya viwanda, ili kusaidia kushauri kuhusiana na jitihada za kuongeza kazi ya kuanzisha na kuendeleza viwanda nchini.
Taarifa iliyotolewa na Ikulu jana, ilieleza kuwa mshauri huyo, Yoshiyasu Mizuno, aliwasili nchini mwanzoni mwa mwaka huu na leo atakutana na Rais Jakaya Kikwete kwa mazungumzo na kupeana mikakati ya jinsi ya kuendeleza viwanda nchini.
Mizuno ambaye alianza kazi Februari 4, mwaka huu, atakuwa nchini kwa makubaliano ya miaka miwili.
Taarifa hiyo kwa vyombo vya habari inaeleza kuwa, tangu kuwasili nchini, Mizuno amekuwa akifanya kazi chini ya Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko, lakini mipango ya kudumu ni kwa mtaalamu huyo kufanya kazi katika Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, ambayo imeanzishwa upya, baada ya mabadiliko ya hivi karibuni ya muundo wa serikali.
Mizuno amekuja nchini kutokana na maombi yaliyotolewa na Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete kwa Serikali ya Japan wakati alipotembelea nchi hiyo mwishoni mwa 2006.
Rais alitoa ombi hilo kwa kutilia maanani uzoefu mkubwa wa Japan katika maendeleo ya viwanda, na alitaka mtaalam mshauri huyo kuja kusaidiana na wataalam wa ndani katika kuboresha eneo la maendeleo ya viwanda, ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.
Jukumu la msingi la mtaalamu huyo ni kuishauri serikali kitaalam katika kuendeleza viwanda nchini kulingana na malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo.
Taarifa hiyo inaeleza ushauri huo unalenga kuiwezesha sekta ya viwanda kukua na kuwa chachu ya maendeleo, na kuwa miongoni mwa sekta zinazochangia kwa kiasi kikubwa katika kukuza uchumi na kuondoa umasikini.
Mtaalam mshauri huyo anatarajiwa pia kutoa ushauri wa jinsi nchi nyingine zilivyoweza kutumia sekta ya viwanda kama moja ya mihimili ya kukuza uchumi.
Pia serikali inatagemea kuwa mtaalam mshauri huyo atachangia katika maandalizi ya mkakati unganishi na mpango madhubuti ambao utabainisha maeneo ya kipaumbele katika sekta ya viwanda yatakayoleta matokeo ya haraka katika muda mfupi, wa kati na ya muda mrefu.
Aidha, mtaalamu huyo anatarajia pia kusaidia katika mikakati ya kuendeleza maeneo maalum ya uzalishaji wa bidhaa za kuuzwa nje, yaani Export Processing Zones (EPZ).
Mkakati huo pia utasaidia katika kuibua miradi katika maeneo mbalimbali ya kipaumbele, hususan viwanda vya mbolea kwa maendeleo ya kilimo na maeneo maalum ya viwanda na biashara.
Source:http://www.freemedia.co.tz/daima/2008/3/5/habari7.php