AIBU KWA CCM: Wanashindwa kuirudisha Arusha chini ya himaya ya CCM pamoja na kutumia polisi!

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
233
Matukio ya jana na leo katika mji wa Ukombozi wa Arusha umeianika serikali ya CCM bila nguo mbele ya mgeni wao kutoka nchi tunakotembezea bakuli hali nchi yetu ni tajiri.

Kikubwa zaidi yanaonyesha mji huo ni kama vile CCM imekwisha kabisa hali iliyojitokeza tangu uchaguzi wa mwaka jana. Wanachofanya ni kutumia polisi kujaribu eti waonekane CCM bado ipo hapo.

Ni aibu kubwa sana kwa CCM kupoteza mji waliokuwa wanaringa nao wa kitalii na mikutano ya kimataifa.

Serikali ya magamba imejaribu kutumia nguvu kubwa tangu uchaguzi mkuu, uchaguzi wa meya, na hadi sasa lakini wanaArusha wako imara sana.
 
Mie nadhani hilo (kwenye red) ndilo linawauma zaidi -- yaani inakuwaje mji wao huu umetwaliwa na CDM? Lakini pia kuna Mza, Mbeya, Iringa Moshi. Shinyanga na Sumbawanga walifanya umafia tu kushinda.

Kusema kweli wanaArusha wameonyesha njia.
 
Lakini mie nauliza -- kosa la Lema ni lipi? Mie nadhani polisi waliweke suala hili wazi.

Hivi mtu akienda kusikiliza kesi yake atangaze kwamba watu wengine wasiende kusikiliza kesi yake? Sheria hiyo imeanza lini?

Hivi mtu akitoka mahakamani kusikiliza kesi yake ni lazima aondoke hapo kwa gari? Sheria hii nayo imeanza lini?

Hivi mtu akikataa dhamana na kukubali kwenda rumande ni kosa? Sheria hii imeanza lini?

Hivi iwapo dhamana iko wazi na wadhamni wanataka kumtoa hakimu anakataa ni kosa? Hii sheria imeanza lini?
 
Kuna kitu kinanitatiza hapa. Hivi kweli CCM wanaweza kuendelea kujigamba majukwaani na mbele ya wafadhili wanakotubembelezea misaada ya milo yetu kwamba Tanzania ni nchi ya amani?

Mtu mwenye akili timamu anaweza kukubali hilo, hasa akiona matukio ya Arusha?

Tafadhalini CCM, acheni kudanganya umma eti Tanzania ni nchi ya amani!
 
6a00d8341bf80a53ef00e5500f61808834-800wi.jpg

Mabomu yarindima Arusha kuanzia saa 11Asubuhi baada ya wanachama na wapenzi wa
chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) kufanya mkesha ambapo waliwasha moto wa matairi na
wengine kuanza kuyashambulia magari kulikopelekea polisi kuvurumisha mabomu ya machozi na baadhi ya viongozi wa
chama hicho kushikiliwa na polisi akiwemo katibu mkuu wa chama hicho Wilbroad Slaa .​

Serikali ya Rais Kikwete imeingia tena mtegoni baada ya vyombo vyake vya mihimili ya utawala kukosa haki na busara na hivyo kutoa maamuzi tata ambayo yamesababisha mikusanyiko na uvunjwaji wa amani jambo ambalo kisiasa litaigharibu serikali ya Tanzania katika jumuiya za kimataifa.

Kukamatwa kwa viongozi wa chama cha upinzani ambao walikuwa na mikutano pamoja na mkesha wa amani bila vurugu ni dalili tosha za serikali kukandamiza demokrasi nchini.

Hayo yametokea Arusha wakati huo huo Arusha imefurika na vyombo mbalimbali vya habari vya kimataifa kutokana na ujio wa Prince Charles ambaye anatazamia kutembelea Arusha.

Busara ingetumika haya yote yasingetokea na Tanzania ingebaki na heshima yake, kwa sasa serikali imejivua nguo. Kwa kuna kila dalili za kukosa washauri wenye busara katika nafasi kama hizi. Hii ya kutumia nguvu tu badala ya akili ni kasoro kubwa katika utawala.
 
Mwenye majibu hayo jamani atusaidie maana na mimi yananitatizo kama mkuu hapo juu
 
Hapo umenena mkuu.ila bado tuna hitaji kujua nini kinachoendelea kwa jioni ya leo
 
kuna chombo cha habari cha kimataifa kilichofanya covarage ya kutosha kuhusiana na tukio la jana na leo?
 
Hali ikoje sasa katika mji wa ukombozi Arusha? Je wana Chadema walikuwa na nguvu ya soda na sio Umma kama hali ni shwari?
 
Kwa sasa TZ hakuna AMANI wala UTULIVU. Kilichobaki ni UVUMILIVU peke yake, ambao nao naona unazidi kutoweka. Mungu ashushe kheri.
 
Akili za wafuasi na viongozi wa CDM ziko mbele mara milioni elfu kumi ni tofauti na zile za CCM, Waberoya et al...
 
Na huyo prince chazi akicheza na a-town tutampiga mawe. safi kabisa lazima mataifa wajue kwamba hapa nchini hali si shwari kama wanavyo fikiri nchi hii hakuna haki kabisa.
 
Na huyo prince chazi akicheza na a-town tutampiga mawe. safi kabisa lazima mataifa wajue kwamba hapa nchini hali si shwari kama wanavyo fikiri nchi hii hakuna haki kabisa.
A. Town Masharaharo tu mmeanguka zaidi ya Gadafi. mnaogopa risasi na mabomu huku mkidai Mji wa Ukombozi Plz wapelekeeni viongozi wenu Msosi selo na wambieni na wao wakatae dhamana wakanyee ndoo gerezani. Mapinduzi hayafanywi kwa nguvu ya Valuu wala kiroba cha Jogoo
 
Back
Top Bottom