Aibu Kuu: Waumini tunapoteza imani, Wachungaji wanagombea Sadaka!

Fortilo

JF-Expert Member
Apr 10, 2012
5,008
15,611
Hapo zamani kidogo(20yrs back) makanisa na sehemu nying za dini(Kwa dini zote) ilikuwa ni sehemu kuu ya huduma ya kiroho na waumini kusaidiana kimwili ikibidi, muda ulipozidi kusogea likaja wimbi la wachungaji binafsi na injili binafsi wakati huo huo likajitokeza wimbi la wajasiriamali wa kidini.

Wamekuja na majina tofauti na sio lengo la uzi huu kuzungumzia majina hayo.

Kwa kudeclare interest mimi ni mkristo na nitazungumzia namna tunavyouziwa injili(Over charged) Kwa mifano michache tu.

1.Leo kanisani tumezindua mwaka wa shukrani, na projection ni kukusanya mil.200,

Kilichonishangaza sio amount... kwamba kila jumuia tutatoa 2.4M..(Not a big deal) issue ni kwenye matumizi yake....kupanua sehemu za parking , renovate private fathers houses (to look more comfortable? make a palace?), kuongeza eneo etc etc......

Hakuna hata shilingi kumi itakaotumika kuendeleza Injili au kuhudumia waamini masikini zaidi na wao wapate walao kipato au mlo kama Bwana Yesu alipofanya kwenye mkutano kwa vipande vitano vya samaki na mikate miwili....

Kiukweli nimejisikia vibaya sana...... hivi kweli kanisa limefika huko? ubinafsi wa namna gani huu??? imefika mahali kanisa linazungumzia mafanikio in terms of revenue?? really?

Hivi kuongeza waamini wanaomcha Mungu kwa roho na kweli, wanaohudumiwa na kanisa si sehemu ya mafanikio?? Hiyo ni moja.

2. Lipo hili la wachungaji kununua magari ya kifahari na private jet.....(Kuish maisha ya anasa to be exact) wakati hakuna shule, wala mradi wowote wa kuendeleza kanisa na kuendeleza waamini waliopo pale.... hivi Yesu angefanya hivi kuna mtu nje ya Israel angeijua injili kweli? Hata kwa kuhadithiwa?

Niseme tu... imenigusa sana, kuna kipindi serikali ilikuwa na mchakato wa kutoza kodi taasisi za dini.. nafikiri ni baada ya kuona wanaenda nje ya matakwa yao kijamii(Kutoa huduma) na badala yake kuingia kwenye biashara.

Hivi kama mkombozi Bank ambayo inatoza kodi ya 1% kama escort charge ya pesa yeyote ya kanisa... huduma iko wapi? vipi masikini wanaojitolea kufanya usafi bure, kulima mashamba, na kufuga bure mali za kanisa wao walipwe na nani?

Nimeamua kuileta hapa najua kuna mchanganyiko wa watu wengi na wengine ni mapadre na wachungaji..... kanisa linapoteza waamini na hakuna jitihada zozote za makusudi za kuwainua kama walivyofanya waanzilishi wa makanisa haya Africa...... its sad and shame....

NOTE: Nimezungumzia ukristo maana ndiyo ninaoujua zaid..

Yesu okoa kanisa lako,

Amen.
 
Ndugu mleta mada una point.
Kwa kweli hali ya baadhi ya makanisa kiimani imeporomoka mno, na badala yake pesa na biashara kwa ujumla imechukua nafasi kubwa.

Hata yale makanisa makubwa yalioaminika kwa kuheshimu taratibu na miiko ya imani nao wamepotoka pia.
Mfano kuna kanisa huko Arusha limefanya biashara ya hoteli kwa mkopo toka crdb, limeshindwa kulipa matokeo yake wamewakamata waumini walipe hilo deni. Sadaka kwa sasa ni kulipa deni na wala sio tena swaka la imani kama ilivyokuwa mwanzo.
 
watu wanaiba,wanaanya utapeli halafu wanakimbilia kanisani na kupewa vyeo vikubwa hayo ndio matokeo yake wanafikiri pesa ndio kigezo cha kwenda mbinguni ukweli makanisa yanakera wao kikubwa si kuabudu bali ni jinsi gani unavyotoa mchango
 
Ndugu mleta mada una point.
Kwa kweli hali ya baadhi ya makanisa kiimani imeporomoka mno, na badala yake pesa na biashara kwa ujumla imechukua nafasi kubwa.

Hata yale makanisa makubwa yalioaminika kwa kuheshimu taratibu na miiko ya imani nao wamepotoka pia.
Mfano kuna kanisa huko Arusha limefanya biashara ya hoteli kwa mkopo toka crdb, limeshindwa kulipa matokeo yake wamewakamata waumini walipe hilo deni. Sadaka kwa sasa ni kulipa deni na wala sio tena swaka la imani kama ilivyokuwa mwanzo.
Sijui twende wapi kwa sasa, muda sio mrefu makanisa yataanza kutengeneza waamini wasioenda kanisani kabisa.... in the long run wana turn out to be a perfect atheist
 
nilijaribu keenda makanisa 3 tofauti huko kote unakumbana na michango isiyo na mbele wala nyuma.
 
Makanisa yamekuwa ni biashara kwa sasa, anayetoa sadaka nyingi ndiye anayetambulika, kusifiwa na kuheshimiwa; suala la kukomaa kiimani na kiroho hakuna tena.

Binafsi nimeamua kukomaa na ''MUNGU'' na si makanisa na madhehebu na sadaka ninayotaraji kutoa kanisani ni ile itakayobaki baada ya kusaidia wahitaji kama masikini, wagonjwa zaidi wanaotoka katika kundi la ndugu, jamaa, marafiki.

Nimechoshwa na injili za mavuno na kutoa sadaka kila inapofika jumapili.
 
PHILE1879 said:
One last chance Jaribu kwenda Jumba la Ufalme la MASHAHIDI Wa Yehova
hakuna sadaka wala fungu la kumi.
Gharama za uendeshaji wa kanisa huwa zinalipwa na nani!?
 
hapa utashangaa huu uzi utavamiwa na waislamu na kuanza kutukana wakristo, na wakristo wengine wataanza kuwajibu matusi na uzi unaharibika pengine kufungiwa au kufutwa
halafu utasikia wanajigamba eti "great thinker"
 
Back
Top Bottom