Aibu: Kina mama watu wazima wadakwa wakijiuza | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Aibu: Kina mama watu wazima wadakwa wakijiuza

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by RICH OIL SHEIKH, Mar 8, 2012.

 1. RICH OIL SHEIKH

  RICH OIL SHEIKH JF-Expert Member

  #1
  Mar 8, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 882
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  [​IMG][​IMG][​IMG][​IMG][​IMG]

  Na Richard Bukos

  INASIKITISHAJE? Wakati wenzao wakijituma kufanya kazi ili kusukuma mbele gurudumu la maisha, akina mama wenye umri uliosogea, ambao ni mama zetu, wamenaswa laivu wakifanya biashara haramu ya kuuza miili yao.

  WANASWA ENEO LA WAZI
  Katika oparesheni iliyoendeshwa na jeshi la polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki iliyopita, akina mama hao walitiwa nguvuni baada ya kukutwa wakijiuza katika eneo la wazi, Buguruni Kimboka jijini Dar es Salaam.
  Majina ya wanawake hao na umri wao katika mabano ni Sauda Mussa (52), Jacqueline Francis (40), Laurencia Rafael (40) na Grace Robinson (40).

  WANA BIFU NA MABINTI WADOGO
  Kwa mujibu wa wenzao ambao hawakunaswa, waliozungumza na paparazi wetu bila kujua, akina mama hao wamekuwa wakijihusisha na biashara hiyo tangu kitambo na kwamba huwa wana bifu na mabinti wadogo wanaojiuza.

  PURUKUSHANI ZA KUKAMATWA
  Uchunguzi wa Amani ulibaini kuwa katika eneo hilo, kuna akina mama wengi wanaojiuza na hao waliokamatwa ni wale walioshindwa kuwakimbia polisi katika purukushani ya kukamatwa.

  INASIKITISHA
  Kwa umri wa akina mama hao, vijana wa Kamanda Suleiman Kova waliowanasa walisema kuwa ni tukio la aibu na la kusikitisha kwani walipaswa kutulia nyumbani na kula matunda ya watoto wao au kujihusisha na shughuli nyingine za ujenzi wa taifa.

  KUPANDISHWA KIZIMBANI
  Baada ya kukamatwa, akina mama hao walitarajiwa kupandishwa kizimbani katika Mahakama ya Jiji la Dar es Salaam, Sokoine Drive, Februari 27, mwaka huu kujibu shitaka hilo.

  Global publishers.
   
 2. Shinto

  Shinto JF-Expert Member

  #2
  Mar 8, 2012
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 1,781
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mbona wamevaa kiswahili swahili ila majina yao ni ya wale 'wasomi'?
   
 3. Sniper

  Sniper JF-Expert Member

  #3
  Mar 8, 2012
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,944
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Maisha magumu wafanyeje? JK si aliwahaidi Maisha bora kwa kila Mtanzania?
   
 4. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #4
  Mar 8, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,456
  Likes Received: 5,844
  Trophy Points: 280
  Wamedanganyia.......:lol::eyebrows::embarassed2:
   
 5. M

  Mr.Mak JF-Expert Member

  #5
  Mar 8, 2012
  Joined: Feb 23, 2011
  Messages: 2,635
  Likes Received: 496
  Trophy Points: 180
  Police wanafanya kazi nzuri sana. Tunaomba muendelee na huo ujasiri wa kutupunguzia aibu
   
 6. M

  Mpigaji JF-Expert Member

  #6
  Mar 8, 2012
  Joined: Feb 6, 2011
  Messages: 386
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Jina halina uhusiano na usomi!Mbona Profesa Ali Mazrui ana jina la Kiswahili ni msomi anayeheshimika katika Afrika?
   
 7. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #7
  Mar 8, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,896
  Likes Received: 5,357
  Trophy Points: 280
  mbona najisikia kwenda kumtoa kwa dhamana huyo kimodo wa nyuma!!
   
 8. Makindi N

  Makindi N JF-Expert Member

  #8
  Mar 8, 2012
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 1,068
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Tena sio Afrika, ni dunia......
   
 9. Mtego wa Noti

  Mtego wa Noti JF-Expert Member

  #9
  Mar 8, 2012
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 2,229
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 160
  wanasemaga old is gold...labda hao wana utamu wa aina yake ukilinganisha na hawa vidogodoo...
   
 10. S

  Shansila Senior Member

  #10
  Mar 8, 2012
  Joined: Jan 28, 2012
  Messages: 189
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  I dont see anything dramatic here,kwa maisha gani hapa bongo hao wasijiuze?Na bado....utasikia na wengine usiowatarajia wako kimboka.Life linazidi kuuma,angalia bei ya gas na bidhaa nyingine za home.
   
 11. R

  Rapture Man JF-Expert Member

  #11
  Mar 8, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 411
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Vyombo vya dola mko wepesi sana kukamata watu wenye vi-kosa vidogo vidogo. Kamateni mafisadi waliojaribu kumwua Dr. Mwakyembe, walioiba pesa za EPA, walioiba pesa zetu na wakakiri waliiba (Pan African Energy), etc. Hamna hata aibu kukimbizana na wenye hatia ndogo ndogo? Mnanichosha!
   
 12. Babuu blessed

  Babuu blessed JF-Expert Member

  #12
  Mar 8, 2012
  Joined: Oct 14, 2010
  Messages: 1,340
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Wanadai haki zao akuna mwanaume anaetakakuwalea
   
 13. TIQO

  TIQO JF-Expert Member

  #13
  Mar 8, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 13,832
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 0
  Alafu hawa bei chee tu tiGo unapewa kwa buku 3
   
 14. l

  luckman JF-Expert Member

  #14
  Mar 8, 2012
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 160
  wee ni chizi,udini ukabila na udaku ndo umekujaaa badala ya kuwa na mawazo kichwani ya kujenga, nenda kakamuliwe hilo bichwa watoe upuuzi wote!
   
 15. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #15
  Mar 8, 2012
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Hawa kama wazazi wetu kabisa lakini utaona wateja ni vijana wanakula tiGo dahh kwa bei chee
   
 16. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #16
  Mar 8, 2012
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,468
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Inaonekana wewe ni mteja wao mzuri sana.
   
 17. yatima

  yatima JF-Expert Member

  #17
  Mar 8, 2012
  Joined: Mar 2, 2011
  Messages: 354
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Hivi ni kweli jamani???? Mbona hawajavaa design ya kujiuza???? Au ndio wamebambikiwa kesi??? manake nchi hii ina vituko vingi ......labda wamekutwa wanaongea ........kwani biashara ya kujiuza ni ENEO LA WAZI NDIO IKO??? Mie siamini - hawa polisi/mgambo saa ingine "reasoning capacity yao ni low" labda walitaka kujieleza wakaambiwa HAKUNA TWENDE KITUONI............ni ilikuwa ni usiku au mchana?????

  HADI KINA MAMA HAO WAMEFIKIA MASWAIBA HAYA.........KWELI TANZANIA INACHOSHA

  NAWAPA POLE KINA MAMA WA WATU ......WANATAFUTA LABDA CHAKULA CHA WATOTO ...... MUNGU TUSAIDIE WATANZANIA :shock::A S embarassed:
   
 18. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #18
  Mar 8, 2012
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,566
  Likes Received: 3,861
  Trophy Points: 280
  wangapi wanajiuza maofisini na vilabuni vya pombe na hawaonekani wala kujulikana?

  si aibu hii!! wako kazini na wanapata wateja, aibu iko wapi?

  kwa nini aibu isiwe kwa anayenunua ilakwa anayeuza??
   
 19. satellite

  satellite JF-Expert Member

  #19
  Mar 8, 2012
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 603
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Shame on you
   
 20. Kennedy

  Kennedy JF-Expert Member

  #20
  Mar 8, 2012
  Joined: Dec 28, 2011
  Messages: 11,249
  Likes Received: 2,931
  Trophy Points: 280
  Hivi Dunia imekwisha au watu ndiyo wamekwisha? Kazi kwelii kwelii!
   
Loading...