Aibu! Kibada Primary School, shule iliyopo 12KM kutoka Ikulu haina madawati, wanafunzi wanakaa chini

Leo asubuhi katika harakati zangu za kwenda kuhakiki jina langu kwaajili yakupiga kuranimejionea maajabu , nikasikitika sana, kweli hii shule iko Kigamboni, wilaya ya Temeke ni shule iliyopo barabarani kabisa, karibu kabisa na serikali ya mtaa. Nimesikitika kwakweli, 12km, je shule zilizopo huko vijijini ? N

Nimetafakari sana nikaumia sana, kweli seriakali inanunua magari 777 kweli, wanafunzi hawana dawati ambalo hata 20,000/- halifiki jamani.

Hapa tuna Mmbuge ndugu Faustin Ndungulile anakaa almost 6 km kutoka shule hii ilipo, na sasa hivi anagombea tena miaka mitano ijayo kwa ticket ya CCM.

Huyu Mmbunge yuko huku JF.

Nawaomba wanajamvi mnielekeze ilipo ofisi ya huyu mbuge ,au mwenye namba zake za simu nitumie hapa, huyu bwana sijaona la maana alilofanya kule Kigamboni, basi tu kuna barabara ambayo ameshindwa kuimalizia ya kisiwani imebaki kama 5km tu iungane na lami, nyingine aliahidi kuimalizia ila wapi. Lakini kwa hii shule hapana kabisa.

Mbona Filikunjombe aliweza kule Ludewa? Si chama chenu, wewe umeshindwaje hayo madawati na uko jikoni? Angekuwa upinzani ningeelewa kwa siasa za Tanzaniza!

Ambao wanakaa huko Kigamboni nendeni mkajionee, msiseme mimi naleta maneno ya uongo na nimemhoji mwalimu mkuu Mr. Komba akasema ndio hali halisi.

Nawasilisha wana jamvi.

Nimesoma bandiko lako. Nakushukuru kwa kuonyesha concern. Nianze kwa kukusahihisha kidogo. Bei ya dawati si chini ya Tsh 100,000 kwa hapa mjini na sio Tsh 20,000.
Binafsi, nimechangia madawati takribani 5000 ndani ya miaka mitano. Ila bado natambua changamoto ya upungufu wa madawati bado ni kubwa. Bado tuna upungufu wa madawati 20,000. Wastani wakuandikisha darasa la kwanza kila mwaka ni 150-300. Hivyo kila mwaka shule inahitaji madawati mapya 50-100 kwa wanafunzi wa darasa la kwanza.

Pamoja na juhudi za Halmashauri, bado mchango wa wadau binafsi unahitajika. Kupitia wadau wa Social media (Twitter) tumeweza kuondoa tatizo la madawati katika shule ya Mjimwema.

Nikuombe "Nivea", Mimi na wewe tuunganishe nguvu katika kutatua tatizo hili. Kwa Pamoja tunaweza kuleta "Maendeleo" na "Mabadiliko" ya kweli. Nimekutumia namba yangu kwa PM.
Nawatakia wadau wote uchaguzi mwema siku ya Jumapili.
Asanteni
Dkt Faustine Ndugulile
 
Huo ndio ukweli. Kwa ujumla Ndungulile hajaitendea haki Kigamboni.Kazi yake kubwa ilikuwa ni mji mpya wa Kigamboni. Kasoro zake ni hizi.
1. Haishi Kigamboni anayeishi huko ni mama yake na yeye aliishi zamani
2. Haitishi vikao vyovyote jimboni mwake kuhusu shughuli za maendeleo ya jimbo zaidi ya pilika za mji mpya
3. Hashiriki shughuli za maendeleo mfano aliwahi kuombwa kuchangia Kituo cha Polisi Kibada, ukarabati wa Zahanati ya Kibada, Ukarabati wa zimamoto nk. akaahidi kutoa michango lakini akatokomea bila kutoa chochote na yote hayo wamefanya wananchi kwa kushirikiana na diwani. Zipo ahadi zake nyingi ambazo ameshindwa kutekeleza yeye anazifahamu.
4. Fedha ya mfuko wa jimbo haina report wala maelezo kwa wananchi. Kama sikosei hii kaipiga yote kimya.
5. Kazi zake anazifanya kwa simu hata sisi huwa tunamwona bungeni na wananchi wake wengi hawamfahamu hata kwa sura waikutana naye barabarani.
6. Wananchi waliwahi kuchukuliwa ardhi yao kwa Tzs. 2m kwa Ekari wakaomba awasaidie akagoma lakini kwenye mji mpya wakiwa tayari kulipwa TZS. 140m kwa ekari aligoma akidai wananchi hawajashirikishwa wakati wao waliridhia na vikao vilifanyika.

Kwa ujumla anahitaji kupumzishwa na mabadiliko yafanyike. Tumchague Lucy Magereli wa Chadema ni anayafahamu matatizo yetu na yuko tayari kutumika kwa ajili ya jimbo lake

Kwa ujumla hafai tena kuwa kiongozi wa Kigamboni. Suala la mji mpya linaendelea kwa namna nyingine hivyo hana propaganda nyingine za kufanya na yule hasimu wake waliyetofautiana hayupo tena
 
Nimesoma bandiko lako. Nakushukuru kwa kuonyesha concern. Nianze kwa kukusahihisha kidogo. Bei ya dawati si chini ya Tsh 100,000 kwa hapa mjini na sio Tsh 20,000.
Binafsi, nimechangia madawati takribani 5000 ndani ya miaka mitano. Ila bado natambua changamoto ya upungufu wa madawati bado ni kubwa. Bado tuna upungufu wa madawati 20,000. Wastani wakuandikisha darasa la kwanza kila mwaka ni 150-300. Hivyo kila mwaka shule inahitaji madawati mapya 50-100 kwa wanafunzi wa darasa la kwanza.

Pamoja na juhudi za Halmashauri, bado mchango wa wadau binafsi unahitajika. Kupitia wadau wa Social media (Twitter) tumeweza kuondoa tatizo la madawati katika shule ya Mjimwema.

Nikuombe "Nivea", Mimi na wewe tuunganishe nguvu katika kutatua tatizo hili. Kwa Pamoja tunaweza kuleta "Maendeleo" na "Mabadiliko" ya kweli. Nimekutumia namba yangu kwa PM.
Nawatakia wadau wote uchaguzi mwema siku ya Jumapili.
Asanteni
Dkt Faustine Ndugulile

Dr Nimekubali response yako, umekubali . Ni kweli huwezi kutoa fedha mfukoni ukanunua madawati.
Nawasihi wanakigamboni wakuchague.
Ila uwe una respond hata baada ya uchaguzi uwe unawapa namba zako wananchi wako. Ni uhakika huyu nivea lazima atakupa kura yako.
KiongoZi ukikaa kimya au ukipuuzia jambo unasababisha wananchi wa define jambo wanavyotaka wao.
Kila la kheri Mbunge
 
Kma unajua kuwa anakaa 6km toka shule ilipo
kwanini ushindwe kujua ofisi yake ilipo..??\
au umetumwa kumsakama na kumtia kimavi
ndugu faustine NDUGULILE...??

Kwanini mnapenda kujitoa ufahamu na uelewa wenu??? Hyo gharama ccm wanatumia kwenye kampeni wangetumia nusu yake tuu zingetosha madawati na kuboresha huduma za afya
 
huyu katumwa,
kama nimetumwa twende tuongozane mpaka kwenye ile shule tukikuta ninachokiongelea ni uongo basi niadhibu
UMEONA MBUNGE MWENYEWE KAKUBALI HAMNA MADAWATI WATOTO WANAKAA CHINI WEWE UNASEMA NIMETUMWA?
 
Nimesoma bandiko lako. Nakushukuru kwa kuonyesha concern. Nianze kwa kukusahihisha kidogo. Bei ya dawati si chini ya Tsh 100,000 kwa hapa mjini na sio Tsh 20,000.
Binafsi, nimechangia madawati takribani 5000 ndani ya miaka mitano. Ila bado natambua changamoto ya upungufu wa madawati bado ni kubwa. Bado tuna upungufu wa madawati 20,000. Wastani wakuandikisha darasa la kwanza kila mwaka ni 150-300. Hivyo kila mwaka shule inahitaji madawati mapya 50-100 kwa wanafunzi wa darasa la kwanza.

Pamoja na juhudi za Halmashauri, bado mchango wa wadau binafsi unahitajika. Kupitia wadau wa Social media (Twitter) tumeweza kuondoa tatizo la madawati katika shule ya Mjimwema.

Nikuombe "Nivea", Mimi na wewe tuunganishe nguvu katika kutatua tatizo hili. Kwa Pamoja tunaweza kuleta "Maendeleo" na "Mabadiliko" ya kweli. Nimekutumia namba yangu kwa PM.
Nawatakia wadau wote uchaguzi mwema siku ya Jumapili.
Asanteni
Dkt Faustine Ndugulile
uLIKUWA UNATAMBUA KUWA WALE WANAFUNZI WA DARASA LA 1-3 NILIOSHUHUDIA WANAKAA CHINI MHESHIMIWA?ULICHANGIA MADAWATI KWENYE HII SHULE?? KWANINI KAMA MMBUNGE USIWEKE MKUTANO UPITISHE HARAMBEE TUCHANGIE WALE WATOTO WANAOKAA CHINI??
 
Nimekusikia. Nimekuelewa. Niunge mkono siku ya Jumapili. Nitalisimamia suala la madawati Kibada S/M. Asante.
 
huo ndio ukweli. Kwa ujumla ndungulile hajaitendea haki kigamboni.kazi yake kubwa ilikuwa ni mji mpya wa kigamboni. Kasoro zake ni hizi.
1. Haishi kigamboni anayeishi huko ni mama yake na yeye aliishi zamani
2. Haitishi vikao vyovyote jimboni mwake kuhusu shughuli za maendeleo ya jimbo zaidi ya pilika za mji mpya
3. Hashiriki shughuli za maendeleo mfano aliwahi kuombwa kuchangia kituo cha polisi kibada, ukarabati wa zahanati ya kibada, ukarabati wa zimamoto nk. Akaahidi kutoa michango lakini akatokomea bila kutoa chochote na yote hayo wamefanya wananchi kwa kushirikiana na diwani. Zipo ahadi zake nyingi ambazo ameshindwa kutekeleza yeye anazifahamu.
4. Fedha ya mfuko wa jimbo haina report wala maelezo kwa wananchi. Kama sikosei hii kaipiga yote kimya.
5. Kazi zake anazifanya kwa simu hata sisi huwa tunamwona bungeni na wananchi wake wengi hawamfahamu hata kwa sura waikutana naye barabarani.
6. Wananchi waliwahi kuchukuliwa ardhi yao kwa tzs. 2m kwa ekari wakaomba awasaidie akagoma lakini kwenye mji mpya wakiwa tayari kulipwa tzs. 140m kwa ekari aligoma akidai wananchi hawajashirikishwa wakati wao waliridhia na vikao vilifanyika.

Kwa ujumla anahitaji kupumzishwa na mabadiliko yafanyike. Tumchague lucy magereli wa chadema ni anayafahamu matatizo yetu na yuko tayari kutumika kwa ajili ya jimbo lake

kwa ujumla hafai tena kuwa kiongozi wa kigamboni. Suala la mji mpya linaendelea kwa namna nyingine hivyo hana propaganda nyingine za kufanya na yule hasimu wake waliyetofautiana hayupo tena
sipendi siasa na sikuileta hii mada kisiasa lakini nafikiri ndugu Dr F. Ndugulile ataelewa ulichozungumza hapo juu
 
Last edited by a moderator:
nimekusikia. Nimekuelewa. Niunge mkono siku ya jumapili. Nitalisimamia suala la madawati kibada s/m. Asante.
aisee nakuomba unijibu maswali haya hebu nitajie shule ulizochangia madawati katika jimbo lako!
Kigamboni tunahitaji mbunge kama filikunjombe na mbona yeye amechakarika vile na jimbo lake kwanini wewe umeshindwa mheshimiwa its only 12 km kutoka ikulu kweli watoto wanakaa chini??
Swala la kuchagua nani ni siri yangu kweli ulikuwa na kura yangu mpaka jana jioni nilipokwenda tu kuhakiki jina ile kura inayoyoma.
 
Hiyo ndiyo CCM katika uhalisia wake,halafu eti wanataka waendelee kutawala.Labda watawale misukule.

Nikuambie nini,ukimpata atakuambia mambo hayawezi kufanywa yote mara moja.Kila jambo kwa wakati.

Huwa wana majibu mepesi yakuudhi sana.
Leo asubuhi katika harakati zangu za kwenda kuhakiki jina langu kwaajili yakupiga kuranimejionea maajabu , nikasikitika sana, kweli hii shule iko Kigamboni, wilaya ya Temeke ni shule iliyopo barabarani kabisa, karibu kabisa na serikali ya mtaa. Nimesikitika kwakweli, 12km, je shule zilizopo huko vijijini ? N

Nimetafakari sana nikaumia sana, kweli seriakali inanunua magari 777 kweli, wanafunzi hawana dawati ambalo hata 20,000/- halifiki jamani.

Hapa tuna Mmbuge ndugu Faustin Ndungulile anakaa almost 6 km kutoka shule hii ilipo, na sasa hivi anagombea tena miaka mitano ijayo kwa ticket ya CCM.

Huyu Mmbunge yuko huku JF.

Nawaomba wanajamvi mnielekeze ilipo ofisi ya huyu mbuge ,au mwenye namba zake za simu nitumie hapa, huyu bwana sijaona la maana alilofanya kule Kigamboni, basi tu kuna barabara ambayo ameshindwa kuimalizia ya kisiwani imebaki kama 5km tu iungane na lami, nyingine aliahidi kuimalizia ila wapi. Lakini kwa hii shule hapana kabisa.

Mbona Filikunjombe aliweza kule Ludewa? Si chama chenu, wewe umeshindwaje hayo madawati na uko jikoni? Angekuwa upinzani ningeelewa kwa siasa za Tanzaniza!

Ambao wanakaa huko Kigamboni nendeni mkajionee, msiseme mimi naleta maneno ya uongo na nimemhoji mwalimu mkuu Mr. Komba akasema ndio hali halisi.

Nawasilisha wana jamvi.
 
Na watu tele wamejenga na kuishi Kibada
Simbachewene anaishi Kibada
Pinda kajenga shule yake mbele ya Kibada panaitwa Muongozo
Sophia Simba kajenga Kimbiji mbele kidogo ya Kibada

Wote hao hata Uchungu na waTanzania hawana! wao wana uchungu na matumbo yao tu!
 
kwani ulijiandikishia wapi kabla ya kwenda kuangalia jina lako hadi leo ndo ushituke hivyo:A S shade::A S shade:napita tu
 
Serikali ya mtaa iko karibu kabisa na hiyo shule na ni kijiofisi kidogo tu .majina ni mengi kwa hiyo wamebabdika kwenye milabgo ya hiyo shule yetu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom