Aibu: JB na Steve Nyerere wapigana bar karibu na msiba wa Kuambiana

Dr. Wansegamila

Verified Member
Feb 3, 2012
2,114
2,000
Katika hali isiyokuwa ya kawaida na kushtua wasanii Jakob Steven Jb na Steve Magele Nyerere wamepiga nguvu kavukavu karibu na eneo la msiba wa marehemu Adam Kuambiana huko Bunju huku kisa kikiwa kugeukana kwenye dili la matangazo.Habari za uhakika zilizotua mezani zilisema kuwa msanii Steve Nyerere ndiye aliyeanza kumchokoza msanii Jb kwa kumchana baada ya kumgeuka kwenye mchongo wa matangazo ya kampuni moja ya simu iliyopo maeneo ya Moroco Jijini Dar.

Habari zaidi zilisema wakati wasanii hao wakiwa baa wanakula kijala siku moja kabla ya mazishi ya msanii mwenzao Steve alimvamia Jb na kuanza kumchana na kumueleza jinsi alivyokuwa na roho mbaya kwa kumgeuka kwenye mchongo wa mtangazo ya simu pale Moroco na kusema ndiyo maana anaroho mbaya.

Majibizano hayo yalidumu kwa muda mrefu sana huku Jb akiwa kimya kwani Stevu alionekana kuumizwa na jambo hilo kwani inadaiwa zile picha za Jb kwenye mabango ya mtandao huo wa simu mchongo alipewa na Steve lakini baadae Jb alimgeuka na kwenda kupiga mchongo kimaya kimya na kumuacha Steve akishangaa.

Hata hivyo Steve aliendelea kusasambua Jb mbele ya watu hali hiyo ilimfanya Jb kunyanyuka na kuanza kufokea nae huku akimtahadharisha kama atamfinyangafinya na ufupi wake ndipo Steve Nyerere aliyekuwa ameshika chupa ya kilaji aliruka kichwa kimoja kilichompiga Jb kifuani na kupepesuka.

Wakati watu akijianda kwenda kuamulia basi Steve ambae aliwahi kucheza ngumi miaka ya nyuma alimshindilia Jb ngumi kama tisa za harakaharaka sehemu ya tumbo iliyomfanya Jb kudondoka chini na kushindwa kupumua kwa dakika tano kisha alinyanyuka na kukalia kiti.
 

Attachments

 • Mskanibongotz msanii Jb.jpg
  File size
  66.9 KB
  Views
  1,776
 • steve nyerere maskanibongotz.jpg
  File size
  42.7 KB
  Views
  1,847

FYATU

JF-Expert Member
Dec 7, 2011
5,364
2,000
Kwa nini huwa hamna uwezo wa kulinganisha vichwa vya habari na habari iliyopo ndani ?

Wakati maelezo yanaonyesha JB ndiye aliyetandikwa na hata kuanguka na kushindwa kupumua...kichwa cha habari kinasema WAMEPIGANA
 

maiye

JF-Expert Member
Dec 16, 2013
880
1,000
JB alipigwa ngumi 9 za haraka-haraka, ama kweli ukubwa wa pua si wingi wa kamasi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom