Aibu gani hii!

Dua

JF-Expert Member
Nov 14, 2006
3,229
662
Aibu gani hii! Hivi ni nili tutaacha tabia kama hizi katika karne ya 21?

mkjjudsmbm4.jpg

Askari kanzu wa Kituo cha Polisi Wazo Dar es Salaam
akimkimbiza mwanamke huku akimcharaza viboko baada ya watu
zaidi ya 100 kuandamana hadi kwenye kituo hicho wakitaka
wenzao watano waliokamatwa juzi katika Kijiji cha Madala Kati waachiwe huru.
(Picha na Yusuf Badi).
 
Halafu viongozi wakisimama majukwaani wanasema tanzania kuna amani na nchi inafuata utawala wa sheria.
 
siku zote serikali inajiona kuwa haikosei! wao kitu sahihi ni kile ambocho wao watakifanya au kukisema ukihoji wanaanza ubaguzi! mara ooohh we ni mpinzani!oooooohhh we unaniambaya kwa nchi yetu!!oooohh unataka kuichfua serikali!!!! na upuuzi mwingine mwingi! ni nani anaye kataa kuwa serikali ya tanzania haiwajali watu wake? picha ndo hizo acha zile tuhuma za watu kufa migodini,nyamuma-serengeti, kuhamishwa wahedzabe kupisha wawindaji wa kiarabu, kuhamishwa kwa wachimbaji wadogo kupisha makampuni makubwa ya uchimbaji(afgem,ashanti etc), zanzibar na ukatili mwingine mwingi! halafu wanajitamba kuwa wanawajali watanzania? wanafiki wakubwa.......!! ila siku yenu yaja
 
Hiyo ndio Tanzania yetu tunayojivunia.Ni bahati mbaya tu kuwa tukio hilo limetokea Dar na wapiga picha wameliwahi na kulitoa sio kama yale yanayotokea vijijini yasiyoonwa. Amani na utulivu ????
 
Askari anaonekana kashiba vizuri sana. Tena amekasirika. Dada anayekimbizwa anaonekana kusikitika zaidi ya kuogopa. Anasikitika kwamba hali ya kuheshimiana imeshuka kiasi hiki nchini kwetu.
Askari kabeba bunduki mkono mmoja, ili Dada akiamua kumgeukia kumkwida basi ajiokoe kwa mtutu.

Yaliyotokea ni kwamba serikali imechukua ardhi ya watu na kukipa Kiwanda Cha Sementi Wazo Hill ili kijipanue. Kilichohitajika, ni fidia ya kutosha na mazungumzo hadi makubaliano yapatikane.

Ni kosa kubwa serikali kuchukua ardhi ya wananchi kwa nguvu. Ilibidi kizungumzwe mpaka kikubalike. Kama fidia ya kutosha ingetolewa lazima wenye ardhi, kwa pamoja, wangekubali. Kuchukua ardhi kwa nguvu ya mtutu ni AIBU
 
Ndio akina ditopole hao akija kushtakiwa Mkono anaingilia kati unamuona keshatolewa...lakini itafikia kipindi tutachoka nakuambia patakua hapatoshi maana tutakua kama iraq Usawa Huu!! wa kunyanyasa mama tena na khanga hajavaa bukta!!
 
kwa kweli haya yanasikitisha sana,hivi kwa nini wananchi hawaungani na kudai haki yao kwa pamoja ?Huu ni wakati wa mabadiliko kwa watanzania,tunaitaji tanzania mpya yenye mwelekeo mpya kwa wananchi wote
 
Aibu gani hii! Hivi ni nili tutaacha tabia kama hizi katika karne ya 21?

Askari kanzu wa Kituo cha Polisi Wazo Dar es Salaam
akimkimbiza mwanamke huku akimcharaza viboko baada ya watu
zaidi ya 100 kuandamana hadi kwenye kituo hicho wakitaka
wenzao watano waliokamatwa juzi katika Kijiji cha Madala Kati waachiwe huru.

Wakuu, heshima mbele lakini pole pole huyu mama tunajua alichofanya? Vipi kama aliwatishia askari huko ndani an bastola? I mean what is going on wakuu mbona tunaanza kuwa too emmotinal na none-ishus? Hii ni picha tu iliyotolewa na mpiga picha ambaye hatujui kama ni mfuasi wa chama cha siasa au mtandao, au asilia au upinzani, maana asingekuwa, angetuwekea all the facts ambazo ukweli zinaonekana ku-miss ili tuweze kutoa uchambuzi, exactly hii picha inasema nini? eti huyo mkuu ni askari kanzu kweli? Hivi ni kweli kwa hii picha unaweza ku-conclude kuwa anamfukuza huyu mama na kumchapa viboko?

Hivi hawawezi kuwa wanancheza mchezo wa kujificha? Anyway, heshima mbele kwa kutuletea picha hiii!
 
Kweli wewe Field Marshall,Maana mtu anakutisha na bastola wewe unatumia fimbo kumchapa,nimekuamini mkuu.
 
Field Marshal,Heshima mbele ila Chakaza nakusalute mkuu.Maana umeandika kama mzaha lakini ujumbe wake mzito.Imenibidi nicheketu.Ila kweli unaweza kutisha kwa bastola halafu ukakimbizwa kwa fimbo?? Na hiyo bastola kaitupa waåpi sijui
 
Ukii-study vizuri picha hiyo, utagundua kuwa the only msaada wa huyo mama ni miguu yake na kaamua kuitumia kukimbia, kama msaada wake ungekuwa bastola nadhani hapa tungekuwa tunazungumza LUGHA TOFAUTI KABISA.........................hata waandishi wetu wangeandika........wananchi waenda na silaha.....and things of that nature

Tumeambiwa kuwa wameenda na sauti zao na miguu yao, walichokutana nacho ni MIRINDIMO YA RISASI HEWANI ili kuwatawanya.

Colonel Massawe kasema vema sana.....ya kwamba kuna utaratibu wa kuwakilisha malalamiko...................hata hivyo yeye akiwa mkuu wa Wilaya ktk hali kama ile ilitakiwa awape audience walau ya Dakika moja au mbili tu na kuwaeleza hilo....ya kwamba wapeleke malalamiko yao kwa ngazi husika na yeye atafuatilia........period, SIDHANI kama wananchi wasingemuelewa ilhali walikuwa na viongozi wao.

Otherwise hii thinking ya mama kuwa na bastola...........its very entertaining!!!!
 
Field Marshall ES said:
Wakuu, heshima mbele lakini pole pole huyu mama tunajua alichofanya?

Twambie mkuu alichofanya?

Field Marshall ES said:
Vipi kama aliwatishia askari huko ndani an bastola?

Ukitishwa na bastola anatoka na bakora Eh? Pamoja na bunduki?

Field Marshall ES said:
I mean what is going on wakuu mbona tunaanza kuwa too emmotinal na none-ishus?

Tuletee picha kama hii popote utakapoiona itakuwa kule Barma, Somalia au Iraq. Je Tanzania kwa nini tuna picha kama hizi? Maelezo ya mpiga picha hapo chini hayatoshi?

Field Marshall ES said:
Hii ni picha tu iliyotolewa na mpiga picha ambaye hatujui kama ni mfuasi wa chama cha siasa au mtandao, au asilia au upinzani, maana asingekuwa, angetuwekea all the facts ambazo ukweli zinaonekana ku-miss ili tuweze kutoa uchambuzi, exactly hii picha inasema nini?

Hiyo picha ipo kwenye Gazeti la Habari Leo pengine sasa unaweza kutueleza kilichojiri, Yaani hadi uwe CCM au CHADEMA? Taifa liko njia panda na huu unazi ni hatari kubwa kwa maendeleo yetu.

Field Marshall ES said:
eti huyo mkuu ni askari kanzu kweli?

Kutokana na mpiga picha wa Habari Leo.

Field Marshall ES said:
Hivi ni kweli kwa hii picha unaweza ku-conclude kuwa anamfukuza huyu mama na kumchapa viboko?

Ndio Gazeti la Chama hili lililosema hivyo. Na vile vile unaweza kujionea mwenyewe, yaani huamini tu? Ama kweli mwenye macho haambiwi tazama.

Field Marshall ES said:
Hivi hawawezi kuwa wanancheza mchezo wa kujificha? Anyway, heshima mbele kwa kutuletea picha hiii!

Nafikiri inabidi uwapelekee ujumbe. Link hii hapa kata ishu mzee huyu nyani hivi sasa amejeruhiwa na kiti yote inateleza ndio kumkoma nyani mwenyewe huku au ........ ..........................................

Soma hapa kabla hawajaiondoa
 
Mkuu ninawaona kama wanafanya mazoezi ya mbio za kupokezana vijiti, au?

Curiously, mbona wale wengine nyuma ya huyu askari kanzu wameachwa bila kula bakora?
 
Hakuna Noma mkuu tuendelee kumkoma Nyani Giladi.
 
Hakuna Noma mkuu tuendelee kumkoma Nyani Giladi.

Mkuu heshima mbele,

Twende mbele na nyuma, damn! hiyo picha mkuu hata kumkoma nyani nyuma mwanangu duh!

Yaani tungeweza kuwafukuza kina Karamagi, badala ya hawa kina mama ambao ni helpless, ingekuwa safi sana maana hiyo ya afande sio kumkoma nyani tena ila kumfukuza nyani mwanangu!
 
Mh. Field Marshal,mie kwa marienge yangu naona kuwa huyo mama wa nyuma usafiri wake haukuwa mzuri na kishatiwa mbaroni na huyo jamaa aliyenaye nyuma.Kazi ikabaki kwa huyo wa mbele.
 
Wakuu, heshima mbele lakini pole pole huyu mama tunajua alichofanya? Vipi kama aliwatishia askari huko ndani an bastola? I mean what is going on wakuu mbona tunaanza kuwa too emmotinal na none-ishus? Hii ni picha tu iliyotolewa na mpiga picha ambaye hatujui kama ni mfuasi wa chama cha siasa au mtandao, au asilia au upinzani, maana asingekuwa, angetuwekea all the facts ambazo ukweli zinaonekana ku-miss ili tuweze kutoa uchambuzi, exactly hii picha inasema nini? eti huyo mkuu ni askari kanzu kweli? Hivi ni kweli kwa hii picha unaweza ku-conclude kuwa anamfukuza huyu mama na kumchapa viboko?

Hivi hawawezi kuwa wanancheza mchezo wa kujificha? Anyway, heshima mbele kwa kutuletea picha hiii!

Heshima yako Mkuu...:) Acha hizo! hivi unafikiri huyu mama angekuwa ana chuma angeikimbia fimbo!? Si angefanya ala Mzuzuri style na kummaliza huyo njagu kinaa!?
 
hii picha ina watu wanne wawili wanaume na wawili wanawake.

inaonekana wanaume wote na askari, na askari mmoja wa nyuma na mwanamke wanaongozana kitaratibu, hawa wawili wa mbele wanafukuzana na askari inaonekana kakamata bakora au fimbo.

sasa tafsiri ziko nyingi huenda hawa wananchi walivunja utaratibu fulani polisi ikabidi iwashughulikie wengine walikubali kujisalimisha kiamani amani na wengine walitaka kukimbia sasa huenda hapa huyu polisi yumo ktk kumdhibiti.

na pia inawezekana polisi kaamua kumtia adabu ili kuwatisha wengine wasicheze na dola.

tafsiri ni nyingi, sasa tujadilini pande zote tusiangalie view moja tu
 
Huyu askari na kitambi chake cha Maharage yaelekea mkewe heshi kulamba vibao kila uchao.

Hivi akimkamata huyu mama ataishia Kumchapa ufimbo tu au ataongea na ukuni juu?
Polisi wetu na vituo vya polisi wana vijambo kila siku,

Afande inaonekana kadhamiria kweli?

Mama malapa mkononi tayari kwa marathoni. Silaha yake kubwa hapo ni wepesi wa miguu yake tu.

Hii picha imenikumbusha ili Movie kabambe ya SARAFINA. Tena huyo mdada anafanana naye kweli!
 
Back
Top Bottom