Aibu - Embassy of Tanzania in Nordic & Baltic States | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Aibu - Embassy of Tanzania in Nordic & Baltic States

Discussion in 'Matangazo madogo' started by sakauye, Jun 6, 2008.

 1. s

  sakauye Member

  #1
  Jun 6, 2008
  Joined: May 20, 2008
  Messages: 27
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Leo nimepata aibu sana jamani. Kuna watu wanataka kwenda Tanzania kuona Simba.

  nikasema easy, tuma maombi sweden mara moja. kufungua mtandao wa embasy wameweka simu hii +46 8 732 24 30/31. kupiga ha! tunaambiwa leo tarehe 6 June 2008 ni sikukuu ya "January 12" hivyo ubalozi umefungwa mpaka jumatatu. kusearch search kwenye hii website yao nikaona simu hii Tel: 46 8 503 20600/1, piga piga na wewe hamna kitu kabisa.

  nikasema ngoja nimuulize katibu wa chama cha watanzania Oslo, Norway. akasema yeye ana "business card" ya embasy akanipa simu hizi +46-87322433/4. piga piga piga hamna kitu.

  ndo yalonikuta mwenzenu. web ya ubalozi ni http://www.tanemb.se
   
 2. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #2
  Jun 6, 2008
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,741
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Jokers,

  Balozi wao nani huko? Inabidi awajibishwe.Inaonekana kuna ujinga mwingi unaendelea hapo.

  Mwendo wa Zero Tolerance tu usawa huu.
   
 3. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #3
  Jun 6, 2008
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  ...subutuuuuu.... nani wa kumwajibisha???
  Pole sana SAKAUYE, hii ndiyo sera yetu ya chama chetu kutufu
   
 4. NaimaOmari

  NaimaOmari JF-Expert Member

  #4
  Jun 6, 2008
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 807
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  fisadi mwengine .... wrong people in wrong places .... atakuwa mtoto au mjukuu wa chama chetu huyo
   
 5. Kijakazi

  Kijakazi JF-Expert Member

  #5
  Jun 6, 2008
  Joined: Jun 26, 2007
  Messages: 3,546
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 135
  mimi sioni tatizo lipowapi kama kweli ni sikukuu sasa kwa nini wafungue ubalozi? kwani wao hawastaili sikukuu? labda unifafanulie zaidi lkni kama ndiyo hivyo nilivyoelewa mimi sioni tatizo kwani ni sikukuu na ubalozi umefungwa mpka j'tu kwa hiyo ulipaswa urudi j'tu kitu rahisi au?
   
 6. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #6
  Jun 6, 2008
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  I try to stay away from threads kama hizi as much as possible. Kwa sababu in the end mimi huwa naamini the buck stops with Membe na kuna watu wanaamini kuwa ninia personal vendeta na Membe
   
 7. Mwanamalundi

  Mwanamalundi JF-Expert Member

  #7
  Jun 6, 2008
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 3,034
  Likes Received: 396
  Trophy Points: 180
  Tatizo ni kwamba, sikukuu ya January 12, kama sikosei--mapinduzi ya zanzibar, inasherehekewa tarehe 6 juni katika ubalozi wa sweeden. Sasa kama wewe unaona hilo ni sawa, endelea kuona hivyo. Ni utashi wako.
   
 8. Kuhani

  Kuhani JF-Expert Member

  #8
  Jun 6, 2008
  Joined: Apr 2, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Dr. Ben Moses.

  Hakuna kingine chochote kinachojulikana rasmi kuhusu huyu Balozi.

  Website haisemi kitu kuhusu staff ya Ubalozi. Jina la Balozi wa Sweden utalipata kwenye orodha ya Mabalozi wa Tanzania iliyoko kwenye website ya Ubalozi wa Uingereza!

  Hakuna anaejua lolote rasmi kuhusu kiongozi yoyote wa Tanzania. Ofisi ya Rais haina Website. Kwa hiyo ukitaka kujua rasmi Kikwete ni nani, katoka wapi kikazi, familia yake, kasoma wapi, kafanya nini, inabidi uenda website ya Kikwete-Shein, ambako wanaweza kukupa wasifu propaganda, au uende kusiko rasmi, kama Wikipedia ambako unaweza kupewa "dataz" ambazo zinaweza kuwa zimeandikwa na some mysterious "Kuhani Mkuu"!

  Ubalozi wetu Marekani umejitahidi katika kueleza Balozi ni nani na ametokea wapi kikazi. Bahati mbaya, Bio fupi ya Balozi Semfue imemtaja Mkapa mara saba, kana kwamba ni sifa kuwa entourage of an ex-President under a cloud of corruption and abuse of office.
   
 9. W

  Wandugu Masanja JF-Expert Member

  #9
  Jun 6, 2008
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 1,535
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  unajuwa wajameni kutoka Sweden mpaka Tanzania ni masafa marefu, wakati wa sherehe ya mapinduzi kule Zenj hapa Sweden ilikuwa bado na baada ya miezi mitani ndio imefika hapa,
   
 10. Kilinzibar

  Kilinzibar Senior Member

  #10
  Jun 6, 2008
  Joined: Mar 6, 2008
  Messages: 125
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ndugu zetu wa kule magharibi wanaseme NONSENSE!!!
   
 11. Augustoons

  Augustoons JF-Expert Member

  #11
  Jun 6, 2008
  Joined: Oct 31, 2007
  Messages: 410
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Mkuu sekauye
  mie sikawizi nishawatumia e-mail pale kwenye contact zao kuwaponda watueleze kulikoni?Huyu Daktari Moses vipi au kaitwa emergency?
   
 12. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #12
  Jun 6, 2008
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,741
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Ben Moses naye ni mmoja wa Mkapaites, alikuwa Canada kasauliwa miaka kibao!

  Washajisahau kama wana kazi za kufanya, ina maana hawapigi simu ofisini au vipi? Au ilikuwa wamekuwa technically challenged na switchbox kwa siku hiyo moja, jamani Januari 12 ni nusu mwaka sasa umepita!
   
 13. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #13
  Jun 6, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,385
  Trophy Points: 280
  Kwani mmejaribu kupiga ubalozi wenu kule DC.. inakuwaje?
   
 14. Kuhani

  Kuhani JF-Expert Member

  #14
  Jun 6, 2008
  Joined: Apr 2, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Lakini tatizo la simu lililoongelewa si ni ubalozi wa Sweden? Haya ya Ubalozi wa DC, ni nyongeza tu, hayakuhusiani na simu au?

  (japo wameshanizingua sana kwenye simu wakati ule wa sakata la Pasi. Simu inaenda kwenye voice mail halafu hawarudishi simu)
   
 15. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #15
  Jun 6, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,385
  Trophy Points: 280
  point yangu ni kuwa ni rahisi kusema hilo la Sweden ni "Isolated incidence"... naamini there is a pervasive pattern of irresponsibility and accountability..
   
 16. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #16
  Jun 6, 2008
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Inna maana mabalozi wanapoteuliwa wapelekwe NGURUDOTO???? au hawana instruments (schemes) za majukumu ya kibalozi??

  Ni mabalozi wa serikali hii hii ya chama changu cha CCM??? aibuuuu
   
 17. U

  UniqueTanganyika New Member

  #17
  Jun 7, 2008
  Joined: Mar 21, 2008
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
   
 18. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #18
  Jun 7, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,572
  Likes Received: 82,082
  Trophy Points: 280
  Pamoja na kuwa kateuliwa na JK inasemekana kwa ombi maalum la jamaa ili 'akaangalie' biashara zake na jamaa hayuko madarakani miaka zaidi ya miwili bado kaona amtaje jamaa mara 7!!!!! Balozi wa Sweden kama sikosei ni somebody Moses hawa wote inasemekana 'wameoa' nyumba moja na Mkapa.
   
 19. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #19
  Jun 7, 2008
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,434
  Likes Received: 2,304
  Trophy Points: 280
  Balozi wa tz Sweden ni swahiba mkubwa wa Mkapa... na alimpa huo ulaji wakati anafungasha virago ikulu... Anyway Ubalozi huu nadhani ndio unaoongoza kwa uzembe kati ya balozi zote. Hata wakati wa kubadilisha passport waliwaliza wabongo hela nyingi tu i.e. walitoza gharama za juu kulinganisha na gharama halisi
   
 20. Kijakazi

  Kijakazi JF-Expert Member

  #20
  Jun 7, 2008
  Joined: Jun 26, 2007
  Messages: 3,546
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 135
   
Loading...