Aibu darasa la 7 kufanya mitihani wakiwa wameketi chini

Fidel80

JF-Expert Member
May 3, 2008
21,947
4,444
Sijui watawala watatuambia nini kwa hili yaani mwanafunzi wa darasa la 7 anafanya mitihani huku akiwa ameketi chini!! dah hii inasikitisha na hii imetokea kwenye roho ya Tanzania ni jiji la Dar es salaam je wanafunzi wa huko Sitimbi inakuwaje?

ssaba.jpg


Hapa wanafunzi wanapiga paper lao la mwisho maarufu kama LY wakiwa wameketi chini ya mchanga.

mtihani_2dfgf.jpg


Ticha hapa akimwelekeza mwanafunzi anae fanya mtihani wa Taifa.

Picha kwa hisani ya Darasa la saba wafanya mtihani wa taifa - Global Publishers

My Take;
Mwalimu J.K Nyerere alipanda misitu mingi hapa nchini mmoja wapo ule wa Sao Hill kwa nini serikali inashindwa kuvuna miti ile na kutengeneza madawati kwa ajili ya wanafunzi nchi nzima??? Tunaona ule msitu waKenya wanavyo fyeka miti kwa kushirikiana na wanao jiita wazawa leo hii ukipita Sao Hill Mafinga miti inazidi kupukutika ukienda kule Songea nako hali tete viongozi wa serikali wanauza kwa kasi ya ajabu. Alafu watoto wetu wanakaa chini hii ni aibu kwa kweli. Miti tunayo wajanja ndo wanao nufaika na viongozi. Inasikitisha sana.
 
Back
Top Bottom