AIBU: CCM Iringa wasomba wanafunzi kumpongeza Rais

tusionacho

JF-Expert Member
Nov 23, 2016
274
514
Wiki nzima hii wamechoma mafuta kutangaza eti ombi la wananchi la kumpongeza Rais limekubaliwa na mkuu wa mkoa Amina Masenza.

Hili tulijua ni mbinu chafu na hakuna watu waliotuma maombi kama hayo ila inafanyika hivyo zaidi kwenye halmashauri zinazoongozwa na UKAWA ili kuhadaa wananchi.

Leo asubuhi kwenye maandamano hayo kumekuwa na wanafunzi wachache ambao ni kidato cha nne na cha pili ambao bado wanaendelea na huku kidato cha kwanza na pili wakiwa likizo pia watumishi wachache waoga wa umma.

Hii iwe funzo na ni matumizi mabaya ya kodi za wananchi.
 
Wiki nzima hii wamechoma mafuta kutangaza eti ombi la wananchi la kumpongeza rais limekubaliwa na mkuu wa mkoa Amina Masenza hili tulijua ni mbinu chafu na hakuna watu waliotuma maombi kama hayo ila inafanyika hivyo zaidi kwenye halmashauri zinazoongozwa na UKAWA ili kuhadaa wananchi
Leo asubuhi kwenye maandamano hayo kumekuwa na wanafunzi wachache ambao ni kidato cha nne na cha pili ambao bado wanaendelea na huku kidato cha kwanza na pili wakiwa likizo pia watumishi wachache waoga wa umma hii iwe funzo na ni matumizi mabaya ya kodi za wananchi
Lumumba walishafilisika, wamebakiza maigizo na kutumia polisi.
 
Nipo Iringa hakuna hata maandamano ya maana.Nimewaona wafanyakazi wanne wa TTCL wakitoka na Bango nadhani walikuwa na meneja wao.Na wote ni wanawake.

Ukiona watu wako busy na biashara zao hayo maandamano sijui yamefanyikia wapi.
 
yaani hao wananchi wanaoandamana kumpongeza bwana mkubwa inaonekana wako vizuri. maisha magumu sana mtaani. huo muda wa maandamano wanaupata wapi?
 
  • Thanks
Reactions: Ftc
Haki ya Mungu mtu analazimisha watu kumpongeza, watumishi wananyimwa haki zao lakini wana lazimishiwa kuandama kumpongeza mtu? uonevu mkubwa sana.
 
W
Haki ya Mungu mtu analazimisha watu kumpongeza, watumishi wananyimwa haki zao lakini wana lazimishiwa kuandama kumpongeza mtu? uonevu mkubwa sana.
watu wabaya sana...Allah anawaona .yaani mtu mawazo yake anasema wengine ndio wamependekeza...Uzuri wake kaburini kila mtu ana maisha yake
 
Back
Top Bottom