Zak Malang
JF-Expert Member
- Dec 30, 2008
- 5,404
- 233
Matukio mawili yafuatayo ya hivi karibuni yanaiabisha sana serikali ya CCM, kwani yanaonyesha bila shaka yoyote udhaifu wa serikali ya CCM -- na kudhihirisha Watz kwamba kweli serikali hii ni porojo tupu, haiwezi kabisa kusimamia sheria, kanuni na maamuzi yake! Na yote haya bila shaka yanatokana na jeuri ya pesa ya waliyonazo ambao wanajisikia raha kuona inaweka viongozi wa juu wa serikali hususan mawaziri -- mifukoni:
1. Zaidi ya wiki tatu zilizopita Waziri wa Ardhi Anna Tibaijuka alitangaza bungeni kutoa wiki moja jengo lile jingine la ghorofa 16 karibu na lile lilioanguka na kuua watu 34 kwamba livunjwe kwani nalo lilijengwa kwa kukiuka plan ya awali. Hadi sasa halijavunjwa na mama Tibaijuka yuko kimya! Kama si nguvu ya pesa ni nini? Jee jengo hilo likianguka na kuuwa watu, mama Tibaijuka atakuwa tayari kujiuzulu na kukabili firing squad?
2. Uongozi wa Star TV umegoma kabisa na kupuuza amri ya serikali kupitia TCRA kurejesha channel ya StarTV katika kingamuzi cha StarTimes. TCRA ilitoa masaa 24 Channel hiyo ya StarTV irejershwe ama sivyo hatua kali zitachululiwa zikiwemo kufungiwa liseni. Hadi sasa StarTV haijarejeshwa StarTimes na hakuna chochote kilichotokea!
Naoma muendeleze mifano mengine iliyotokea inayodhihirisha udhaifu wa serikali na kufyata mkia hasa mbele ya wenye fedha .