Aibu! Angalia jinsi serikali ya CCM inavyowekwa mifukoni na wenye jeuri ya pesa!

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
233


Matukio mawili yafuatayo ya hivi karibuni yanaiabisha sana serikali ya CCM, kwani yanaonyesha bila shaka yoyote udhaifu wa serikali ya CCM -- na kudhihirisha Watz kwamba kweli serikali hii ni porojo tupu, haiwezi kabisa kusimamia sheria, kanuni na maamuzi yake! Na yote haya bila shaka yanatokana na jeuri ya pesa ya waliyonazo ambao wanajisikia raha kuona inaweka viongozi wa juu wa serikali – hususan mawaziri -- mifukoni:


1. Zaidi ya wiki tatu zilizopita Waziri wa Ardhi Anna Tibaijuka alitangaza bungeni kutoa wiki moja jengo lile jingine la ghorofa 16 karibu na lile lilioanguka na kuua watu 34 kwamba livunjwe kwani nalo lilijengwa kwa kukiuka plan ya awali. Hadi sasa halijavunjwa na mama Tibaijuka yuko kimya! Kama si nguvu ya pesa ni nini? Jee jengo hilo likianguka na kuuwa watu, mama Tibaijuka atakuwa tayari kujiuzulu na kukabili firing squad?


2. Uongozi wa Star TV umegoma kabisa na kupuuza amri ya serikali kupitia TCRA kurejesha channel ya StarTV katika king’amuzi cha StarTimes. TCRA ilitoa masaa 24 Channel hiyo ya StarTV irejershwe ama sivyo hatua kali zitachululiwa zikiwemo kufungiwa liseni. Hadi sasa StarTV haijarejeshwa StarTimes na hakuna chochote kilichotokea!

Naoma muendeleze mifano mengine iliyotokea inayodhihirisha udhaifu wa serikali na kufyata mkia hasa mbele ya wenye fedha….



 
Makampuni ya simu binafsi na uchimbaji madini kukaidi kusajili makampuni yao DSE
 
Serikali ya CCM kushindwa kumpeleka mahakamani yule mwizi mkubwa wa EPA Rostam Azizi!
 
Wahindi na wachina kuja kufanya kaz bongo wakati wabongo wana uwezo wa kuzifanya na hawana ajira, hata umachinga!!!!
 
Hivi kweli inakuingia akilini kuona kwenye mikutano ya Mwigulu Mchemba watu wakikaa kwenye viti, wakati watoto wetu kwa maelfu kama sio mamilioni wanakaa chini wakiwa masomoni. Hivi hii ni akili kweli? Nadhani maono ya CCM yamefikia mwisho, kwa vile Maandiko Matakatifu yanatuambia kwamba, Vijana watapata maono na wazee wataota ndoto.

Kwa mwendo huu na umri wa CCM nadhani tuwaache waendelee kuota ndoto na wengine hawa wenye mawazo mbadala watuletee maono mapya.


 
Kampuni moja kubwa ya mafuta ( nimeisahau ) hapa nchini mwaka juzi iliongoza mgomo.Kama mnakumbuka kampuni za mafuta zilivyogoma kutoa mafuta
 
Kampuni moja kubwa ya mafuta ( nimeisahau ) hapa nchini mwaka juzi iliongoza mgomo.Kama mnakumbuka kampuni za mafuta zilivyogoma kutoa mafuta

Mkuu ilikuwa na BP na waligoma hapohapo serikali ikiwa na hisa 50 percent kwenye BP.
 
Waziri mkuu alisema mafisadi anawajuwa ila ili kulinda usalama wa nchi inatubidi tufunge mabakuli yetu
 
Back
Top Bottom