Aibu aliyopewa Prof. Jay na CHADEMA ni bora angeachana nayo

Sijawahi kufanikiwa kuifahamu CHADEMA wala sijawahi kujua ndani ya CHADEMA ni nani anaweza kusaidiwa kwa michango pale anapopatwa tatizo. Nikikumbuka Tundu Lissu alipopatwa na tatizo alisaidiwa na chama chake kwa hali na Mali na hapo hakuwa na cheo chochote ndani ya CHAMA(Naomba kusahihishwa kama nimekosoa)

Kilichonisukuma Leo kutaka kuifahamu CHADEMA ndani ya suala hili la kuchangiana ndani la CHADEMA ni juu ya mjumbe wa kamati kuu ya chama hicho Prof Jay ambaye yupo mahututi ICU. Je michango inaangalia sura, umuhimu au mtazamo wa mwenyekiti?

Ninapokumbuka mjumbe wa kamati kuu ya CCM alipoanguka ghafla kule Lumumba si mwenyekiti wa CCM Taifa wala mjumbe wa shina la wakereketwa wote walienda kumuona. Yalioneshwa mapenzi makubwa na utu.
Acha wivu, mchango ule wa matibabu ndio unakutoa kamasi🤔
 
Umeshindwa kuona aibu ya chama chako unaona ya CDM? wewe mwehu kwelikweli!
Uonevu na ukatili unaofanywa na chama chako dhidi ya upinzani huoni!
 
Ni kweli kwenye janga mchawi ndio anakuwa wa kwanza kufika. Hata Tundu Lissu alivyopigwa risasi Magufuli ndio alikuwa wa kwanza kutoa salamu za pole na kumuombea apone haraka :D:D:D
 
Hiyo katiba mpya mnaitaka ili mpate uhuru wa kutukana mitandaoni?
Mtu akitukana mtandaoni kuna sheria ya kumwajibisha. Mtu anaweza kutoa maoni usiyoyapenda ukasema ametukana. Acha sheria ndiyo imhukumu usimnyime uhuru wa kutoa maoni
 
Back
Top Bottom