Aibiwa Mumewe, Aenda Mahakamani, Alipwa Fidia Dola Milioni 9;sheria aipo tanzania?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Aibiwa Mumewe, Aenda Mahakamani, Alipwa Fidia Dola Milioni 9;sheria aipo tanzania??

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by major mkandala, Mar 23, 2010.

 1. m

  major mkandala Member

  #1
  Mar 23, 2010
  Joined: Mar 6, 2010
  Messages: 74
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  [​IMG]
  Bi. Cynthia Shackelford akiwa na mbwa wakeTuesday, March 23, 2010 2:53 AM
  Mwanamke wa nchini Marekani aliyemfikisha mahakamani mwanamke aliyempora mumewe, ameshinda kesi aliyomfungulia mwanamke huyo kwa kumuibia mumewe na atalipwa fidia ya dola milioni 9.Cynthia Shackelford mwenye umri wa miaka 60 aliiambia mahakama ya North Carolina kuwa aliacha kazi yake ya ualimu ili kulea watoto na kumsaidia mumewe Allan katika kuziendeleza shughuli zake za kisheria.

  Kwa kutumia kipengele cha sheria ambacho huwa hakitumiki sana, Bi Cynthia alisema kuwa mumwe alikuwa ni mtu mwenye furaha na mwenye kuonyesha mapenzi kwake kabla ya bi Anne Lundquist, 49, kuuingilia uhusiano wao na kuanza uhusiano na mumewe.

  Baada ya siku mbili za kuisikiliza kesi hiyo, majaji waliamuru bi Cynthia alipwe fidia ya dola milioni 9 baada ya bi Cynthia kuithibitishia mahakama jinsi mapenzi yao yalivyokuwa motomoto kabla ya Anne kuanza uhusiano na mumewe.

  Mahakama ilitaka bi Cynthia alipwe fidia kwa kitendo cha mumewe kutembea nje ya ndoa yao na kumuumiza kihisia bi Cynthia.

  Anne ambaye hivi sasa anaishi na Allan, alisema kuwa atakata rufaa kupinga hukumu hiyo akidai kuwa alianza uhusiano na Allan baada ya ndoa ya Allan na mkewe kuvunjika.

  Jimbo la North Carolina ni miongoni mwa majimbo machache ya Marekani ambayo yanaruhusu wanandoa  watanzania tunaomba hii sheria ianzishwe haraka kulinda ndoa za watu wezi wamekuwa wengi sana mijianaume sasa hivi airtaki kuoa inasubiri kulelewa wanawake nao wanasubiri kutunzwa awataki kuolewa ati kuzeeshana loh!!!

  sheria ije haraka MH SITTA TUSAIDIEN KABLA AMJAONDOKA JAMANI
   
 2. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #2
  Mar 23, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Mh.Sitta akufanyie nini? Sheria hii mbona ipo..ni wewe tu huijui au hujui namna ya kuitumia! Uliza ujuzwe
   
 3. m

  major mkandala Member

  #3
  Mar 23, 2010
  Joined: Mar 6, 2010
  Messages: 74
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nashukuru iko kipande ipi??nashukuru kwa ujulisho..
   
 4. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #4
  Mar 23, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Alienation of affection tunayo Tanzania? I mean sheria yake....
   
 5. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #5
  Mar 23, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Right to consortium, committing adultery with somebody's wife/husband is also actionable and you can claim damages ( by implication its tantamount to allienation of affection so to speak.)
  The problem is people are not that keen to pursue this cause of action.....( those who know the existance of such remedies).Besides wenye nazo za kutosha kumletea mtu kiwango kikubwa cha fidia wanajua namna ya ku handle mambo yao au they are too proud kujipeleka kujianika mahakamani kuhusu private lives zao and hence not ready for that drama. Wenye muda wa kushinda mahakamani ni wale hata wakiamriwa kulipa fidia hawana kitu!
   
 6. M-bongotz

  M-bongotz JF-Expert Member

  #6
  Mar 24, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,732
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Kwa kuongezea tu alishosema WoS ni kwamba kwa wanandoa adultery ni offence ambayo remedy yake ni damages.,wabongo wengi hawajui kuwa hii kitu ipo kwenye sheria yetu ya ndoa au hawataki kuanika mambo yao ya binafsi kwa kuchelea aibu, kifungu cha sheria kinachohusika ni hiki FYI..
   
 7. Nyabwire

  Nyabwire Member

  #7
  Mar 24, 2010
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 40
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  sasa jamani...mmefanya vizuri kumweleza rafiki yetu kuwa sheria ipo,sasa ataipata wapi??????
  ok,labda na mimi nisaidie hapo,ni The Law of Marriage Act, Act No 5 ya 1971.
   
Loading...