Ahukumiwa miaka 20 jela kwa kupatikana na nyara za serikali

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,658
55,485
Mahakama ya Wilaya ya Mlele, mkoani Katavi imemuhukumu Roza John kwenda jela miaka 20 kwa kupatikana na tuhuma za kumiliki nyara za serikali kinyume na utaratibu.

Akisoma mashtaka hayo, Hakimu Teotimus Swai, alisema licha ya kuwa mshtakiwa alikiri kosa, Mahakama imetoa adhabu hiyo ili iwe fundisho kwa wote wenye nia ya kutenda kosa kama hilo.

Mwendesha Mashtaka, Jamila Mziray alieleza mahakamani hapo kuwa, mshtakiwa alitenda kosa hilo Septemba 11, 2016 kijijini Mkuyuni, Wilaya ya Mlele.

Mshtakiwa huyo ambaye ni mkazi wa Kijiji cha Mkuyuni, Tarafa ya Majimoto alitiwa hatiani baada ya kupekuliwa na Askari Polisi na kukutwa akiwa na ngozi mbili za mnyama aitwaye kano na ngozi moja ya pakapori zenye thamani ya shilingi milioni 1.5
 
Huyo kano simfahamu kuwa ni mnyama gani.
Lakini paka pori ama kimburu, anafanana kila kitu na paka wafugwao na waki-"met" wanazaa kama kawaida.
Nachojiuliza kukutwa na ngozi ya paka, kunautaalamu gani wa kutofautisha kuwa huyu ni paka aina gani?
 
Mama wa watu anakula miaka 20 wakati mdanganyifu Bashite analindwa na polisi na JWTZ....
This is not fair.
 
Back
Top Bottom