Ahukumiwa kunyongwa kwa kumuua ‘mchawi’

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,696
2,253
kamba.jpg

MKAZI wa Kijiji cha Mesanga Mugumu Wilayani Serengeti mkoani Mara, Wambura Muhonyi (32) amehukumiwa kunyongwa hadi kufa baada ya kupatikana na hatia ya kushiriki katika mauaji ya Nyabaturi Matoto akimtuhumu kuwa mchawi.

Mugumu anadaiwa akiwa na wenzake wanne ambao wametoroka, walimuua Matoto ambaye ni mkazi wa kijiji hicho kwa kumpiga kwa fimbo na kumkata kwa panga.

Akisomewa hukumu hiyo juzi katika Mahakama Kuu kanda ya Mwanza katika kesi ya mauaji namba 48/2014 na Jaji Rose Ebrahim alidai kuridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa mashitaka ukiongozwa mwanasheria wa Serikali, Venance Mayenga na kuungwa mkono na mashahidi wengine watatu wa upande huo wa mashitaka akiwemo dada wa marehemu.

Awali katika kesi hiyo, mwanasheria wa serikali Mayenga alidai kuwa Julai 16 mwaka 2010, majira ya mchana mtuhumiwa Wambura katika kijiji cha Mesanga Mugumu Wilayani Serengeti, alishirikiana na kikundi cha watu katika kijiji hicho wakiwemo watuhumiwa wenzake waliotoroka.

Watuhumiwa waliotoroka ni Mirumbe Ngarita , Gekene Wambura, Machota Tatwi na Marwa Mwita. Walikuwa wakimtuhumu kuwa ni mshirikina na kwamba anamroga mke wa Wambura Wanchere kitendo ambacho marehemu alikana.

Jaji Rose alisema “katika makosa ya kuua kwa kukusudia chini ya kifungu cha sheria namba 196 ya makosa ya jinai sura ya 16, kinaangalia nia ya kutenda kosa, mtuhumiwa alishiriki kwenda nyumbani kwa marehemu kumchukua na kwenda kumsulubu hadi kifo chake kwa hali hiyo nia ovu ilikuwepo, silaha zilizotumika”.

Alisema mtuhumiwa alionyesha kudanganya mahakama kwa kudai hakuweka sahihi kitendo kilichodhihirishia mahakama kuwa maelezo yake yalikuwa ya uongo ukilinganisha na ushahidi.

Chanzo: HabariLeo
 
Back
Top Bottom