Ahukumiwa kifungo kwa kosa la kuiba nguvu za kiume za mpenzi wake

izo biz

JF-Expert Member
May 3, 2022
2,004
3,219
Mwanamke huyo mkazi wa ujerumani mwenye miaka 39, aliyekuwa kwenye mahusiano na mwanaume mwenye miaka 42 ameshtakiwa kwa kosa la wizi wa mbegu za kiume na kuhukumiwa kifungo cha miezi 6 jela!

Jaji wa mahakama ya magharibi nchini humo, Astrid Salewsky amesema kuwa, wizi huo wa mbegu za kiume ulifanywa pale mwanamke huyo alipotoboa vitundu kwenye kondomu za mwanaume huyo ili watakapofanya mapenzi, mbegu hizo zipitilize kuingia ukeni!

Uamuzi huo umetolewa katika mahakama ya kikanda ya mji wa magharibi ya ujerumani, Bielefield!
 
izo biz

JF-Expert Member
May 3, 2022
2,004
3,219
Chanzo kimebainikika kuwa, mwanamke huyo alifanya hivyo ili apate ujauzito kwa sababu alifahamu fika pindi atakapomuomba huyo mwanaume ampatie ujauzito, asingekubaliwa ombi lake! Hii ni kwa sababu alitokea kumpenda sana mwanaume huyo! Hivyo alihitaji kupata mtoto kutoka kwa huyo mwanaume!
 
masopakyindi

Platinum Member
Jul 5, 2011
17,107
11,920
Chanzo kimebainikika kuwa, mwanamke huyo alifanya hivyo ili apate ujauzito kwa sababu alifahamu fika pindi atakapomuomba huyo mwanaume ampatie ujauzito, asingekubaliwa ombi lake! Hii ni kwa sababu alitokea kumpenda sana mwanaume huyo! Hivyo alihitaji kupata mtoto kutoka kwa huyo mwanaume!
Badilisha mada, nguvu za kiume na mbegu za kiume vitu viwili tofauti.
 
izo biz

JF-Expert Member
May 3, 2022
2,004
3,219
Badilisha mada, nguvu za kiume na mbegu za kiume vitu viwili tofauti.
Dah! Keyboard Auto correction mkuu,
Nilitype Mbegu za kiume, kumbe kwenye simu kuna neno Nguvu za kiume cramed! Nilivyokuwa naandika neno Mbegu, nikiongeza neno "za kiume", neno Mbegu linabadilika kuwa "Nguvu" Sikupitia tena kabla ya ku post!
Sorry wakuu!
Cc Moderator ,just edit heading iwe mbegu badala ya nguvu
 
3 Reactions
Reply
Top Bottom