Uchaguzi 2020 Ahsanteni Watanzania kwa kutuchagua ila tusisahau CCM bila Upinzani ni sawa na Dini bila Shetani, hakuna visingizio!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,780
141,667
Kwa upande wa udiwani matokeo yaliyokwishatoka yanaonyesha CCM ikiwa mbele kwa kuzoa kata nyingi.

Hata ubunge hakuna Mgombea wa Upinzani aliyetangazwa kushinda hadi sasa na tayari kiongozi mkuu wa CHADEMA ameshapoteza kiti chake cha ubunge kule Machame.

CCM tunawashukuru sana Watanzania kwa kutuchagua.

Angalizo kwa viongozi wa CCM waliochaguliwa ni moja tu kwamba CCM bila Upinzani ni sawa na Dini bila Shetani.

Hebu fikiria kidogo maisha bila shetani nani wa kumsingizia dhambi?

Maendeleo hayana vyama!

cc: Mzee Mgaya, Mchungaji Erasto
 
Na mkifika bungeni, napendekeza.

1. Upitishwe mswaada wa kufutwa vyama vya Upinzani, kibaki chama kimoja.

2. Rais Magufuli apewe Urais wa maisha. Yaani atawale mpaka siku atakapoingia kaburini.

Sababu
Kufanya uchaguzi huku kukiwa na matokeo tayari, ni upotevu wa rasilimali. Pesa zilizotumika kwa uchaguzi huu, bora zingejenga hata barabara, na wabunge walivyopita tu CCM ingeishia hapo.

Au wadau mnasemaje!
 
Mimi nlishauri siku za nyuma tukiwa kwenye kampeni kwamba wabunge hawa tume na Magu wahakikishe wanarudi bungeni hata kama watapata kura kidogo

1. Mbowe
2. Lema
3. Sugu
4. Mdee
5. Msigwa
6. Bulaya
7. Upendo peneza
8. Pr.j

Lakini BAVICHA kama kawaida yao wakanitukana. Ngoja tuwe na chama kimoja tu sasa maana hawajielewi hawa CHADEMA
 
Mimi nlishauri siku za nyuma tukiwa kwenye kampeni kwamba wabunge hawa tume na Magu wahakikishe wanarudi bungeni hata kama watapata kura kidogo,

1. Mbowe
2. Lema
3. Sugu
4. Mdee
5. Msigwa
6. Bulaya
7. Upendo peneza
8. Pr.j

Lakini bavicha kama kawaida yao wakanitukana. Ngoja tuwe na chama kimoja tu sasa maana hayajielewi haya machadema
Hii sio ya kushangilia hata kidogo, embu fikiria madudu mangapi ya serikali yakafichuliwa na upinzani? Na je sasa tutegemee nini baada ya kuwa na bunge la upande mmoja yaani watetezi wa serikali na sio watetezi wa wananchi😠
 
Tuna angalau siku 1825 mpka uchaguzi ujao. Anaye tujaalia Pumzi ndie ajuae siri ya nani atamaliza salama hizo siku.
Na mkifika bungeni, napendekeza.

1. Upitishwe mswaada wa KUFUTA VYAMA VYA UPINZANI kibaki chama kimoja.

2. Rais Magufuli apewe uRais wa maisha. Yaani atawale mpaka siku atakapoingia kaburini.

Sababu.
Kufanya uchaguzi huku kukiwa na matokeo tayari, ni upotevu wa rasilimali. Pesa zilizotumika kwa UCHAFUZI huu, bora zingejenga hata barabara, na wabunge walivyopita tu CCM ingeishia hapo.

Au wadau mnasemaje!
 
Si walituaminisha wapo mioyoni mwa watu. Kuna jamaa yangu yupo kagera amesimamia uchaguz na anasema hakuna wizi wowte lakn uraisi Lissu kura 3 , JPM zaidi ya 20.13K
 
Taarifa Za Kweli Zisizo Na Ukakasi Ziko Wazi

CCM Hii Hii Ambayo Ilikuwa Na Kile Inachotaka Kifanyike

Wakifika Bungeni, Wafanye Marekebisho Kwenye Sheria Ya 1992 Iliyoanzisha Vyama Vingi!!

Wafute Vyama Vingi Halafu Iwapo Mtu Anataka Kufanya Siasa Ataifanyia Ndani Ya CCM
 
Hii sio ya kushangilia hata kidogo, embu fikiria madudu mangapi ya serikali yakafichuliwa na upinzani??? Na je sasa tutegemee nini baada ya kuwa na bunge la upande mmoja yaani watetezi wa serikali na sio watetezi wa wananchi😠
Bunge la chama kimoja linakuwa kali kuliko bunge la upinzani wa ruzuku.

Wewe subiri tufike 2023 kuelekea 2025.
 
Back
Top Bottom