Lizaboni
JF-Expert Member
- Feb 21, 2013
- 33,894
- 20,372
Wadau, amani iwe kwenu.
Hakika haikuwa lelemama kwa mradi wa Mabasi yaendayo Haraka kuanza kazi. Zipo changamoto za msingi ambazo zilijitokeza ambazo kwa hakika zilihitaji ufumbuzi wa lazima. Moja ya changamoto hizo ni suala zima la gharama za nauli ambapo awali nauli iliyokuwa imetangazwa haikuwa rafiki kwa wana Dar es Salaam. Nimpongeze Waziri Mkuu kwa kulisimamia hilo na kwa hakika wana Dar es Salaam wana kila sababu ya kumshukuru.
Pamoja na zile changamoto za msingi, mradi huo ulikuwa na figisu figisu nyingi huku vijana wa UKAWA wakijipanga kwa zamu kuhakikisha kuwa wanaweka mitandaoni kila aina ya uzushi wakilenga kuupinga mradi huo. Miongoni mwa uzushi huo ni pamoja na aina ya mabasi yaliyoagizwa kwamba hayana milango ya kutosha na milango yake haijakaa sawa kwa madai kuwa milango ipo juu mno. Kwamba mabasi hayo hayana ubora wowote na hayafai. Kwamba kuna harufu ya ufisadi kwenye mradi huo.
Wengine walikuja na hekaya kwamba mradi huo ni mali binafsi ya familia ya Jakaya. Wengine wakaja na hekaye eti muda unaotumika kwa magari hayo hauendani na dhana kuwa ni mabasi yaendayo Haraka.
Muda sasa umepita na changamoto za msingi zimepatiwa ufumbuzi. Hata wale ndugu zangu waliokuwa wanaukebehi mradi huo wameacha kuanzisha mijadala ya kipuuzi. Kwa ujumla wameukubali na wanakubaliana na Mzee Mwinyi kuwa Mabasi hayo ni URODA.
Niwaombe sana ndugu zangu wa UKAWA ambao mnapinga kila kitu. Kwamba, wakati ndio huamua siku zote. Kelele zenu na majungu yenu huwa yanafika wakati yanashindwa kufanya kazi. Oneni sasa mnavyoumbuka. Mradi huooooo unafanya kazi na una manufaa makubwa kwa wana Dar es Salaam.
Lazima tuheshimiane.