Ahsante wana JF

Invisible

JF Admin
Feb 26, 2006
16,294
8,334
Ilikuwa ni safari ya kifo cha uhuru wa habari Tanzania lakini sasa uhuru umerejea. Ni ushindi wa wana JF (wasomaji na waliojisajili) wote.

Naomba kutoeleza chochote zaidi lakini nipeleke shukrani zangu za kipekee kwa wana habari wote: Magazeti ya HabariLeo, Mtanzania, ThisDay, Kulikoni, Tanzania Daima n.k. Pia blog mbalimbali ambazo nimezipitia ikiwa ni pamoja na KLH News, Michuzi, eThinkTank na wengine wengi. Ukweli ni kuwa bila ninyi kuliweka wazi suala hili basi tulikuwa kwenye wakati mgumu sana.

Aidha niwashukuru watu binafsi ikiwa ni pamoja na Mwanakijiji, Mhariri wa ThisDay, Zitto Kabwe, John Mnyika, Tundu Lissu, Wakili Armao, Mchumba wangu (namhakikishia ndoa ipo tu July), Mbaraka, W. Malecela, Andrew, Abdallah, na watanzania wote ambao kwa namna moja ama nyingine walihakikisha wanapiga simu kwa DCI Manumba na kwingineko kuhakikisha wanaweka wazi kazi inayofanywa na JF.

Mwisho nawashukuru wenzetu William Mushi na Yona Fares Maro kwa jitihada zao.

Wana JF, tulikubali kuwa na collective responsibility kwa ajili yenu tukiamini nanyi hamtotutupa katika hali hiyo. Tulilazimika kubeba kila aina ya lawama kwa ajili yenu. Vitisho kwetu vimeendelea kuongezeka na usalama wetu unazidi kuwa mdogo. Tuombeane uzima tu.

Niseme kuwa tukubaliane kwamba Tanzania ni yetu sote na watu wachache wanaotaka kuzimika kwa harakati za kuisafisha wasipewe nafasi. Pia wanachama hapa tuache kabisa kuandika habari zisizo na uthibitisho ama zenye dhamira ya kulichafua taifa ambazo chanzo chake kina utata ama hakuna kabisa. Zitapelekea wakati mwingine watu kama FD ama Mnyika nao kukamatwa. Huenda nao wakakubali wao kuwa Invisible.

Kisha nadhani kuna watu wana wasiwasi kuwa kuna kitakachofutwa, sijaona kilichofutwa zaidi ya kuona vilivyohamishwa. Hiyo inamaanisha kuwa kila kitu kipo kama kilivyokuwa. Shukrani kwa moderators.

Namshukuru Invisible kwa kuniruhusu kutumia nickname yake kuweza kuwasilisha maoni haya kwa sasa na kuomba ushirikiano naye pindi mambo kama haya yanapotokea.

Sina mengi ya kuandika zaidi ya kusema "Ahsante watanzania, pamoja tutafika mbali".

Nitaendelea kuwawekea nafasi za kazi kadiri ninavyozipata.

Mac
 
Mac pole sana,

......binafsi ilinia-affect sana baada ya kuona mshikaji anyetuwekea mambo ya kazi mtandaoni eti amezuiliwa na polisi na kuhojiwa....................trust me we are together and we will be........long live JF!!
 
Ukweli siwezi kuwataja nyote mliohusika kwa namna moja ama nyingine. Bloggers wengi wamesaidia katika kuhakikisha wanalipigia kelele hili, magazeti mengi ambayo hata sikupata nakala zake yamesaidia. Watanzania wengine walinipigia simu wakiniambia wako nyuma yetu. Namshukuru askofu mmoja kwa namna ya kipekee ambaye alihangaika kuipata namba yangu na kunipigia akaniombea kwa dakika 2. Ni jambo lililonipa faraja zaidi.

Ahsante watanzania, ndilo ninaloweza kusema.
 
Bro Mac, Pole sana na masibu yale yaliyowapata wewe na Mike!! Pamoja na kutoa pia shukurani kwa wote waliop[elekea mambo kunyooka naomba nikuambie kuwa usalama wako ni kitu namba moja na hakuna fisadi yoyote atakayeweza kukugusa..... Sala na duaa zetu zipo nawe na Mods wote na wanaJambo wote na familia, ndugu na jamaa zao.....

Kwenye ukweli hata baraka za Mola zinakuwepo!!!

Long live JF, Long live WaTanzania safi, Aluta Continua!!!
 
Mac,

Pole sana kwa matatizo. Uhuru wetu na Utaifa wetu hautakamilika kama hatutapitia misukosuko kama hii na kuthibitishia tabaka la watawala kuwa sisi kama Jamii, tupo pamoja na tunaishi kwa umoja.

Vita ya kulikomboa Taifa kutoka ufidhuli na uhujumu na kudai uongozi bora bado vinaendelea.

Nakutakia afya njema ya mwili na roho!
 
Mac,

Pole sana kwa matatizo. Uhuru wetu na Utaifa wetu hautakamilika kama hatutapitia misukosuko kama hii na kuthibitishia tabaka la watawala kuwa sisi kama Jamii, tupo pamoja na tunaishi kwa umoja.

Vita ya kulikomboa Taifa kutoka ufidhuli na uhujumu na kudai uongozi bora bado vinaendelea.

Nakutakia afya njema ya mwili na roho!

Rev.

Tunashukuru, nimepata taarifa za wewe na Morani kusaidia kwa kiwango kikubwa. Nawashukuru sana pia. Siwezi kuwataja mmoja baada ya mwingine. Nimepewa dakika chache kutumia nick ya Invisible. Naondoka kwa nick hii naingia kwa ya kwangu nitaendelea kutoa maoni yangu kama mtanzania. Mimi si mwanasiasa, mimi napenda kuwawekea wenzangu nafasi za kazi pindi nizipatapo.

Kuna mtu alikuwa ananiuliza 'Hujawambia mimi ni nani'? Nakumbuka waliniuliza 'kichuguu' ni nani nikawambia ni 'kichuguu' tu. Hakukuwa na maswali zaidi kwani tuliwambia kuwa ni vigumu kumjua mtu mwenye pen name. Nashawishika kufikiri kuwa nilitumia jina langu kamili na imenigharimu. Kuna raha ya kutumia pen name.

Ahsanteni wote kwa ushirikiano
 
Wale wanaoteseka kutokana na msimamo wao wa kuendeleza UWAZI nchini kwetu ni MASHAHIDI wa demokrasia ya Tanzania. Ni miamba ya Historia ya Tanzania.

Kwa niaba yangu na ya wenzangu wote wanaotaka UWAZI uwepo Tanzania, naomba niwape pole mliosumbuliwa na Polisi, na niwashukuru sana wale waliowasaidia katika kipindi hicho. Mungu abariki kazi zenu.

Madikteta wanaotumia vyombo vya serikali kama Polisi kukandamiza uwazi na demokrasia watakumbukwa kama MAHAINI katika Historia yetu.
 
Hi Mac ... Kwa dhati kabisa Pokea pole na Moyo wa uwezo wa kuhimili pia kusahau kipindi hikicha muhimu kwenye maisha yako:

Si masiha yako pekee, ushahidi unao, itakuwaje maisha yako pekee, Ona magazeti yote yalivyo simama nawewe..ona radio mbalimabali szilivyosimama na wewe, ona BBC walivyosimama na wewe, ona Wanaharakati walivyosimama na wewe, ona simu mabalimbali zivyokufikia na kuona kuwa haupo mwenyewe.

Ona Tanzania ilivyobadilika wka kipindi kifupi baada ya tukio. Nasikia watoto wa jirani hapo wametunga wimbo wa kizalendo na Kitaifa kusifia JF. Si unaona bwana...!

Sisi ni nani tusiwe pamoja.

Tanzania is our country.

Sio ya mtu moja ua Kikundi kimoja. Tunatakiwa na Kitiba kulisimamia Taifa hili kwani tunawajibika sio kikaba tu bali zaidi Tunamuogopa MUNGU yule tunayemuimba kwenye wimbo wa Taifa..atatuuliza..tulikuwa wapi mambo yakiharibikana huku tunajitia kuwania kuziona mbigu? No..no!! its impossible; KUJITOA lazima kuwepo ..Hi Mac you just represented BOTH OF US.

Nimshukuru sana pia INVISIBLE kujitolea kukuwezesha kutufikia kupitia kwake.

God bless you, God bless TZ
 
Mac,

Tunashukuru sana kwa kuwasiliana na pole kwa matatizo yote mliyokumbana
ambayo kwa wengi wetu ni makubwa mno na yasiyoweza kuvumilika.

Umenichekesha kwamba walikuwa wanauliza Kichuguu ni nani? Kuna jamaa yangu pia huwa nampelekea baadhi ya mijadala ya JF, aliwahi kusema ameipenda kweli nickname ya Kichuguu (nyumba ambayo nguchiro na mchwa wanaishi bila kugombana). Naona prof. Kichuguu inabidi ulisajili hilo jina.

Muhimu kwasasa ni kusonga mbele na kuangalia namna ya kukiendeleza hiki chombo chetu kwa ufanisi mkubwa.

Kama nilivyoandika jana, mimi sikutegemea hizo positive responses kubwa za watu mbalimbali pamoja na vyombo vya habari. Kama hata askofu aliamua kuwaombeeni na kuiombea JF basi hayo ni mafanikio makubwa sana.
 
Nimefarijika sana kuipata hewani Jf na hakika nitanenepa zaidi na zaidi.
Ninawapongeza saaana woote waliojitolea kuhakikisha wanalinda IP zetu na ninashukuru uaminifu wa Invisible wa kuamua kuwa makini zaidi na pia alivyokuwa anajitahidi kuiweka hewani JF. Pia bila kuwapa hongera wale wenzetu Premium Members nitakuwa nakosa shukrani. Na sana sana wale wooote walioamua kukwangua pockets zao kuturudisha hewani. Waaama endapo JF ingekuwa ni ya kulipia basi leo mafisadi wasingejiuzulu na ukweli ungekuwa ni gharama sana.

Naomba msinipe pogezi zozote kwani sijachanga chochote zaidi ya kutoa pole na shime kwa wenzetu waliokuwa mstari wa mbele kufuatilia JF yetu.

Ila angalizo dogo tu. Inabidi moderators wetu wawe tahadhari sana na serikali, msikubali offer yeyote kwani mtego hunasa hata mtegaji. Vita dhidi ya ufisadi idumishwe hadi watokomezwe
 
Pole kwa misukosuko, huo ndio ukuaji wa JF na gharama ambayo Mac na Mike mmeanza kuipata kwa uchungu mkubwa.

Kwanza nakupa hongera kwa kuweza kutobadili msimamo wako wa kupata Jiko hapo July na karibu sana kwenye members club huenda ukapunguza kuishi ndani ya hii JF .... .... haha ahaaaaa.

Tanzania ni ya Watanzania na Jeshi la polisi kazi yao ni kuwalinda WTZ na mali zao kwa kufuata katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Viongozi wanapopewa dhamana ya kuongoza ni lazima wafanye hivyo kwa mujibu wa katiba na kuona haki inatendeka bila kujali swala lolote lile ambalo halina msingi katika maamuzi yao. Inatia aibu kuona vyombo vya usalama vinawanyanyasa wale wanaolipa kodi ambao ndio wanahakikisha uwepo wao kwenye shughuli hizo.

Serikali ni lazima ichukue hatua kali kwa wale wote ambao kwa njia moja au nyingine wanajaribu kuzuia uhuru wa maoni au mawazo ambayo ni haki ya kikatiba. Je, waliofanya hivi wamechukuliwa hatua gani na serikali?
 
Mac , Mike na wana JF
Kwa wale walio wakristo nitasema hadithi ya Biblia na wewe Rev.Koshoka utasema zaidi .Tuna amini kwamba Christ died for us .We sinners .Tunajua mashahidi wa Uganda walikufa kwa ajii ya walicho kiamini .Waliunguzwa hadi majivu lakini their souls and voice remained standing and praising the Lord . Wote mnajua akina Kalolzi Lwanga, Kizito na wengineo ni Watakatifu hawa wafia dini .

Pia kila mwata Feb 14 tunaimba Valentine Day .Tunajua Fr.Valentine ni mfia dini Mkatoliki wa Roma na mifano ni mingi sana naweza kutoa .Mwalimu alikosana na Wazungu wa Westn kw aalicho kiamini ni Udhalimu na nyie ni lazima mna mifano mizito labda zaidi ya hii .

Wana JF wote nawapa hongera sana . Mike , Marc, Kishoka , Invisible,na wale ma coordinators siwezi kuwataja hapa kwa jinsi mlivyo hangaika na hasa kwa wale walio tiwa nguvuni kusema Kichuguu ni Kichuguu imethibitisha imani yenu kwa Tanzania na JF ndiyo njia na chombo cha kuweza kuisadia Tanzania kuwa tunapo itaka iwe kesho tukiwa hai ama baadaye kidogo baada ya sisi kuaga Dunia.Tutasimama na Mungu atasaidia kuwavunja nguvu madhalimu wote .
 
Nashawishika kufikiri kuwa nilitumia jina langu kamili na imenigharimu. Kuna raha ya kutumia pen name.

Ahsanteni wote kwa ushirikiano

Pole sana mkuu Mac! Yaani hapo umekuwa kama Yesu maana walitaka kukupeleka kwa pilato kwa kuwapa watu wenye njaa mikate na samaki... kazi kwelikweli yani hawataki uwape watu taarifa za nafasi za kazi, hawa jama wanataka kutupulizia hewa ya sumu nini?!!!

Nijuavyo mimi kazi kubwa ya JF ni kuleta maisha bora kwa kila mtanzania.

Maisha bora ni pamoja na uhuru wa kutoa maoni bila kubugudhiwa, kuwa na uhuru wa kupata taarifa bila kubughuziwa sanasana taarifa zinazohusu maslahi ya umma na ya Taifa.

Kuna mtu alitoa point kali sana jana sijui ni thread gani. Alisema JF inaonekana ni ya wapinzani sababu CCM hawaji kujibu hoja humu ndani. Hii ni kweli kabisa sababu kuna watu wengine kama sisi hatujawahi kuwa na kadi ya siasa ya chama chochote. Japo madingi wetu ndio wametuharibia nchi. Ni watu tunaoipenda nchi yetu tu....Full stop!!!!Nijuavyo mimi hata Hon. Yusuph Makamba akitaka kuwa member humu anaweza.

Ni kweli leo tunatumia haya majina ya kijiweni lakini ipo siku tutatokeza nje ya pazia la woga. Mzee Mac umelipa gharama kubwa sana kwa kutumia jina lako. Lakini pia hata kwa kutumia majina ya barazani pia kuna gharama. Wengi wetu tungependa tufahamiane na kuongea kwa ukaribu zaidi lakini tunashindwa. Wakati mwingine humu unaweza kujibizana na baba yako au mama yako bila kujua. Wapinzani wa JF lazima wajue kuwa tunalazimika kutumia haya majina sababu tunajua nchi haina uhuru wa kutosha kuelezea hisia na fikra zetu. Watawala wengi wanapenda uongee lugha za kuwasifu na kuwapamba hata kama wameshindwa kutimiza wajibu wao. Wengi hawajui kama kukosolewa ni opportunity ya wao kuwa viongozi bora zaidi.

NI kweli wakati mwingine tukiwa barazani tunajikuta tunataja mambo binafsi ya watu, lakini nafikiri ni jazba ambayo hata watawala huwa wanakuwa nayo na yao ni mbaya zaidi sababu wakati mwingine wanaua kama walivyofanya huku Zanzibar. Sio nia yetu kumshambulia mtu au kumdhalilisha mtu. Sio nia yetu kuongea pumba na kuleta uchochezi usio na maana. JF sio kijiwe cha wahuni kama ilivyofikiriwa mwanzoni. Mimi binafsi tokea nimeingia humu nimejikuta naipenda zaidi nchi yangu. Hamu ya maendeleo na kuboreshwa kwa maisha ya mtanzania imeongezeka.
 
kusema Kichuguu ni Kichuguu imethibitisha imani yenu kwa Tanzania na JF ndiyo njia na chombo cha kuweza kuisadia Tanzania kuwa tunapo itaka iwe kesho tukiwa hai ama baadaye kidogo baada ya sisi kuaga Dunia.
Shikamoo,

Mimi Mike, nashukuru kwa jinsi mlivyotusaidia na kushuhulikia kutoka kwetu na hasa mac kunipa courage nisiogope kuwa ni gharama za demokrasia. waliniuliza kwanini najihusisha na siasa na sisomi, nikawambia ilikuwa ni mwanzoni na sasa nasoma niko shule na jf sijihusishi sana. Mimi ni memba kwa nick ya CMB.

Asanteni nyote kwa uhshirikiano
 
Tuwape pole wapendwa wetu wote!!!

Kimbunga hiki cha Katrina kilichotokea ilikuwa ni test ya kuonyesha namna gani JF iko strong.

Matokeo yake ni kwamba JF imeonekana kwamba kweli ni Strong Sana kuliko ilivyotegemewa... Lakini zaidi ya hapo ikapata fursa ya kujulikana kwa namna ya ajabu vile... (kwa maana nyingine serikali ilikuja kutambua kumbe JF ina full representation ya watu wa serikali, dini, scholars, haki za binadamu, celebrities etc.. etc..., chombo cha namna hii cha kupashana habari hakipo mahali popote Tanzania...)

Vyombo mbalimbali vya ndani na vya nje vikaweza kuijua JF. sitashangaa kuona kabla ya mwisho wa mwaka huu kuona member wamekuwa zaidi ya 8000.

Mwanasiasa mzuri anatakiwa aingie hapa kujiangalia kwenye kioo... ningekuwa mwanasiasa ningeweza hata kuanzisha thread ya kuni-jadili mimi binafsi ili nijue wananchi wana nifahamu vipi kabla ya kugombea... in short hii ni kama CC ya CCM ... ukitoka safi hapa then wewe ni kiongozi mzuri...

Wakati umefika sasa kulinda heshima tuliyopewa... coming 2010
 
Mac na Mike

Poleni sana kwa matatizo mliyoyapata sio nyie tu mlikuwa na matatizo hata sisi wanaJF tuliokuwa uraiani tulikuwa hatuna raha wala furaha kwa muda wote mliokuwa kizuizini kwani tulipatwa na shock kubwa sana.Tunamshukuru mungu sana mmerudi tena tuendeleze libeneke na kumchapa nyani giladi mchana kweupe.God bless Jamboforum and God bless watanazania wote.Amiin
 
Shikamoo,

Mimi Mike, nashukuru kwa jinsi mlivyotusaidia na kushuhulikia kutoka kwetu na hasa mac kunipa courage nisiogope kuwa ni gharama za demokrasia. waliniuliza kwanini najihusisha na siasa na sisomi, nikawambia ilikuwa ni mwanzoni na sasa nasoma niko shule na jf sijihusishi sana. Mimi ni memba kwa nick ya CMB.

Asanteni nyote kwa uhshirikiano


Hakuna neno kijana wangu .Niliugua when I learned that watu wangu wamekamatwa .Jirani yangu hapa Kijichi akaniita .Mzee Lunyungu nakuona leo kama huna furaha ? Nikasema ni kweli Mama Amina siko salama maana Mwema na JK wameamua kuingilia uhuru wa sisi kusema . Nikaishia hapo nikaingia kwenye gari hadi Kawe nikapewa habari rasmi kwamba mlikuwa ndani na kijana ambaye yuko pale Makao Makuu ya Poisi.Nikamuuliza kosa akasema wanatfuta nani anafadhili mtandao maana unaweza kuwa unatumiwa na wabaya wa Nchi na baadaye Nchi ikapata matatizo . Nikasema mbele yake BS.Nikauliza immidiate hatari ilikuwa ipi kati ya JF na akina Karamagi,Chenge, RA etc. Akakosa jibu nikaingia kwenye gari nikaondoka.
 
Shikamoo,

Mimi Mike, nashukuru kwa jinsi mlivyotusaidia na kushuhulikia kutoka kwetu na hasa mac kunipa courage nisiogope kuwa ni gharama za demokrasia. waliniuliza kwanini najihusisha na siasa na sisomi, nikawambia ilikuwa ni mwanzoni na sasa nasoma niko shule na jf sijihusishi sana. Mimi ni memba kwa nick ya CMB.

Asanteni nyote kwa uhshirikiano

Mike, pole na matatizo ndugu yetu..... Kaza uzi wa shule kwani ndio muhimu na ukumbuke kuwa mchango wako kuikomboa Tanzania na hili zimwi la UFISADI utaendelea kukumbukwa na kuihitajika (as and when needed)....

Shule njema, kazi njema na mafanikio!!

God bless
 
Mike na Mac, pole zangu kwa walioteswa bila sababu na laana zangu kwa wale waliojaribu kuteka uhuru wa JF.
Nimeamini kuwa pen name inalipa, laiti waJF wangekuwa wanatumia majina yao, mambo yangekuwa mengine sasa hivi

Sebene linaendelea
 
Pongezi sana kwa kazi mliyoifanya na mnayoendelea kuifanya mimi nilikuwa naisikia JF lakini mara nyingi nilikuwa sijaifuatilia sana kujua yanayojiri. Baada ya kusikia misukosuko iliyotokea na baada ya kusoma habari kupitia KLH news na kugundua kwamba imerudi hewani nimeamua kujisajiri ili nami niwe mwanachama na kuweza kuungana na wenzagu wanaoitakia mema nchi yetu nzuri ya Tanzania.

a) Pongezi za pekee kwa waanzilishi wa JF pamoja na Mwanakijiji na wengine kazi mnayofanya ni kubwa na inataka moyo sana. Kwa ilo ni naomba mpokee pongezi zangu.

b) Sasa tufanye kazi kwa bidii tufanyeni utafiti wa kina na tuwafikie hata wale watu wasio na uwezo wa kupata habari tuweze kuwafahamisha ni jinsi gani maisha yao yanadumazwa na mafisadi wasio na huruma hata kidogo.

c) Kama kuna michango inahitajika kuweza kuimarisha JF mimi niko tayari kuhamasisha na pia niko tayari kuchangia kwa hali na mali. Hivyo mwanakijiji na wengine iwapo kuna msaada utakaotakiwa tuwasiliane kwenye "PM".

d) Ikiwezekana tuwe na watu wa kutuletea habari toka pande zote za nchi. Wale ambao wana moyo wa kujitolea na ambao wanaweza kuwa wanakusanya matukio mbalimbali ambayo mara nyingi huwa hayawafikii watanzania walio wengi.

e) Tuna safari ndefu sana ya kuutokomeza UFISADI Tanzania. Sasa inabidi tuangalie nini mustakabali wa JF miaka 3, 5, 10, 15 ijayo mbele. Iwepo mikakati mizuri na ya hali ya juu katika kuhakisha kwamba JF unakuwa ni mtandao imara unaoweza kuwaunganisha wale wote wanaoitakia mema nchi yetu ya Tanzania.

f) Ebu jiulize wamarekani na hao wazungu toka nchi za dunia ya kwanza waliopo sasa kama si kuteseka kwa mababu zao unadhani wangekuwa wanafaidi...msingi mzuri kwao ulijengwa miaka 50, 100, 200 iliyopita na sisi sasa. Sasa Watanzania wenzagu tuamke na kuhamasishana ili wajukuu zetu na vitukuu waweze kuiona Tanzania nzuri. Hawa walioko madarakani sasa hawawezi kutufikisha popote...

Jamani wote tuamke sauti zisikike na tuijenge Tanzania kuanzia leo na si kesho...

Mungu ibariki Tanzania
Mungu ibariki JF
Mungu wajaze nguvu waanzilishi na wanachama wote wa JF ili waweze kufichua maovu..
 
Back
Top Bottom