Ahsante TCRA kwa kupunguza utitiri wa ving'amuzi

Realbest

JF-Expert Member
Aug 5, 2013
809
293
Mwananchi

TCRA yaja na king’amuzi kimoja
Friday February 7 2020
Miaka sita iliyopita, Tanzania ilishuhudia mabadiliko makubwa katika sekta ya matangazo, mifumo ya analogia ilizimwa rasmi na kuanzishwa kwa matangazo ya dijitali.

Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), James Kilaba
BY Ephrahim Bahemu, Mwananchi ebahemu@mwananchi.co.tz

Advertisement
Dar es Salaam. Miaka sita iliyopita, Tanzania ilishuhudia mabadiliko makubwa katika sekta ya matangazo, mifumo ya analogia ilizimwa rasmi na kuanzishwa kwa matangazo ya dijitali.

Katika hatua hiyo, vituo vya televisheni vililazimika kurekebisha mitambo yake ya kurushia matangazo ili kuendana na mabadiliko hayo na wamiliki walilazimika kutoa mamilioni ya fedha ili kupata vifaa hivyo.

Baadaye lilikuja zoezi la kuzizima simu ambazo hazina viwango na lilifanyika hivyo na maelfu ya simu zilizimwa na hivi karibuni kulikuwa na uzimaji wa mamilioni ya laini za simu ambazo hazijasajiliwa kwa alama za vidole.

Hiyo ilikuwa ni hadithi fupi ya mabadiliko yaliyofanyika katika sekta ya mawasiliano katika kipindi cha chini ya muongo mmoja; mabadiliko bado yanaendelea.

Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), James Kilaba aliliambia gazeti hili jana kuwa kabla ya mwaka huu kuisha, mfumo wa ving’amuzi utabadilika na badala yake wateja wataweza kutumia king’amuzi kimoja kupata matangazo yoyote ya vituo vya televisheni.

Pia Soma
Serikali ya Tanzania yatumia Sh128 bilioni kuboresha elimu ya msingi
Uraia wenye mashaka wanyima vitambulisho maelfu ya wananchi Geita
Ujenzi reli ya kisasa Dar-Morogoro wafikia asilimia 70
Bunge la Tanzania laridhia azimio la kufuta madeni
Mteja hatalazimika kuwa na ving’amuzi (decorder) nyingi bali atalazimika kununua kadi ya kituo cha televisheni anachotaka na king’amuzi hicho kipya kitaweza kumpa matangazo hayo.

“Siwezi kusema hili litafanyika mpaka lini, lakini kabla ya mwaka huu kwisha litakuwa limefanyika,” alisema mkurugenzi huyo.

“Hili jambo ni mchakato, lazima ushirikishe wadau na wao waridhie. Ukisema uliharakishe utaharibu soko.”

Advertisement
Alisema jambo hilo ni lazima lifanyike kwa kuwa linajibu changamoto za watu wengi ambao wamekuwa wakilalamika mrundikano wa ving’amuzi nyumbani kwao na walikuwa wanalazimika kufanya hivyo ili kupata chaneli nyingi za maudhui wanayoyataka.

“Tupo kwenye advanced stage (hatua ya juu) ya mchakato na hatua hii itaondoa kilio cha watu wengi waliokuwa wanataka chaneli zinazoonyeshwa bure (FTA) kwa kuwa akiwa na kadi ya kisumbusi ambacho kinaonyesha FTA akitaka anachomeka tu kama unavyoweza kubadilisha laini ya simu,” alisema Kilaba.

Aidha mkuu wa Kitengo cha Leseni wa TCRA, Andrew Kisaka alisema mabadiliko hayo hayafanani sana na yale ya kutoka analogia kwenda dijitali kwa kuwa yanahusu upokeaji tu tofauti na awali wakati mabadiliko yalipohusu hadi mitambo ya kurushia matangazo.

Alisema kwa ving’amuzi, ambavyo pia vinaitwa visimbusi, itakuwa ni lazima lakini kwa TV ambazo zina uwezo wa kunasa chaneli litakuwa ni jambo la hiari.

Kisaka alisema kumekuwa na malalamiko ya muda mrefu ya kuwa na visimbusi vingi majumbani na shida inakuwa wakati mteja anapohitaji vipindi tofauti ambavyo vinapatikana katika visimbusi tofauti.

“Watu wamekuwa wanahangaika huku na kule unakuta visimbusi vingine anavitumia kwa muda mfupi tu wakati mwingine mtu anatamani angeweza kukinunua kwa muda fulani tu,” alisema.

“Na tatizo hilo si la kwetu tu tayari lilishazitesa nchi za Ulaya ndipo wakaja na suluhisho la namna hiyo.”

Alisema kwa kutumia teknolojia ya CAM mtu atakuwa na kisimbusi kimoja, lakini anakuwa na kadi za kielektroniki za watoa huduma tofauti ambao akiweka anapata huduma zao hivyo hivi sasa watoa huduma watakuwa wanauza CAM na sio visimbusi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni kama inaingia akilini

Je tunaenda kuingia gharama nyingine kununua king'amuzi husika na baadaye kadi za watoa huduma au ving 'amuzi vya sasa vitaweza kupokea kadi za wraps huduma tofauti?
Wale wanaoitwa Tcra Ccc nafikiri hawatekelezi wajibu wao ipasavyo
 
Ni kitu kizuri lakini pia hiyo ya kuwa na kadi nyingi za watoa huduma ambapo mteja atalazimika (pengine) kuwa anachomoa kadi ya mtoa huduma huyu kutoka kwenye king'amuzi hicho ili aweze kuchomeka kadi ya mtoa huduma mwingine nako kunaweza kuwa ni mateso. Au hicho king'amuzi kipya kitaweza kuwa na sehemu kadhaa (mfano tano) za kuchomeka kadi za watoa huduma tofauti (makampuni) kwa wakati mmoja kwa hivyo inabaki kwa mtumiaji kubadili tu aina ya mtoa huduma kwa kutumia remote kama ilivyo kwenye AV selector?
 
TCRA WAMEAMUA KUFUMUA KILA KITU UPYA NASUBURIA WAANZE UHAKIKI WA IMEI ZA SIMU HALAFU UMILIKI WA LAZIMA WA LINE YA MTANDAO WA TTCL
 
Ni kitu kizuri lakini pia hiyo ya kuwa na kadi nyingi za watoa huduma ambapo mteja atalazimika (pengine) kuwa anachomoa kadi ya mtoa huduma huyu kutoka kwenye king'amuzi hicho ili aweze kuchomeka kadi ya mtoa huduma mwingine nako kunaweza kuwa ni mateso. Au hicho king'amuzi kipya kitaweza kuwa na sehemu kadhaa (mfano tano) za kuchomeka kadi za watoa huduma tofauti (makampuni) kwa wakati mmoja kwa hivyo inabaki kwa mtumiaji kubadili tu kadi kwa kutumia remote kama ilivyo kwenye AV selector?
Hivi vingamuzi vipya vitakuwa havina tofauti na machangudoa maana kanuni ni ile ile ya kuchomekewa chomekewa kila kitu
 
Mm nadhan hyo siyo suluhisho bado kutakuwa na usumbufu wa chomeka chomoa wa hzo kadi...mfano mm nyumban kwang nina ving'amuzi viwil na tv yang(smart tv) unaweza kutumia hata ving'amuzi vitatu kwa wakat mmoja coz ya three hdmi cable
So nikitaka kuangalia dstv naswitch hdmi1 nikitaka startimes naswitch to hdmi2 ambayo haina usumbufu kama hyo ya kuchomoa kadi na kuchomeka wakat mm nadili na remote tu...labda hvyo ving'amuzi viwe na uwezo wa kuchomeka kadi zaid ya moja ndo itakuwa suluhisho

Sent using Jamii Forums mobile app
 
TCRA WAMEAMUA KUFUMUA KILA KITU UPYA NASUBURIA WAANZE UHAKIKI WA IMEI ZA SIMU HALAFU UMILIKI WA LAZIMA WA LINE YA MTANDAO WA TTCL
Kipindi kile cha uhakiki wa IMEI/simu fake yule meneja wa mawasiliano wa TCRA wa wakati huo Bw. Mungy kila kona ya chombo cha habari aliyokuwa akipita alituaminisha umma wa watanzania kwamba baada ya kuzimwa simu fake wizi wa simu ungetoweka kwenye uso wa Tanzania. Je, huo wizi umetoweka kweli?
 
Eti ukienda police wanakwambia kesi za simu ni nyingi sana kwahiyo labda kama kuna mtu unamshuku umseme wakamkamate
 
Back
Top Bottom