Ahsante TBC kwa kutuonesha mmiliki wa ambulance na vichwa vya treni

Whitesmith

JF-Expert Member
Aug 12, 2017
362
500
Jana kwa wale wenye mioyo migumu tunaoangalia TBC kulikuwa na kipindi ambacho walialika maafisa wawili wa mamlaka ya bandari TPA kuzungumzia maswala mbalimbali.

Mmoja wa watazamaji alipiga simu nakuulizia kwann wanashindwa kudhibiti hadi raisi anakuja kuvumbua madudu?(nukuu isiyo rasmi)

Afisa wa TPA; alijibu kuwa wao ndiyo waliompa Raisi taarifa kuwa scanner yao imeona container ya mitumba ambayo ndani yake kuna magari na siyo raisi ndiyo aliyevumbua hayo in scanner za TPA, akaendelea zaidi kuwa wanampango wakufunga scanner zingine.

Mtazamaji mwingine: aliulizia kuhusu ambulance na vichwa vya treni.

Afisa wa TPA: Mizigo yote inayokuja bandarini ina manifest inayoonesha inatoka wapi na final destination(mmiliki) ni wapi, kuhusu ambulance manifest inaonesha ziliagizwa kutoka ofisi ya raisi na ndicho afisa wa TPA alichomweleza raisi na baada ya hapo raisi aliunda tume ya kuchunguza the same thing na vichwa vya treni ina manifest take.

Haya sasa, maswali ya kuchokoza mada;
1. Mkulu alipokuwa ziara mikoa mbalimbali refer mererani aliahidi ambulance wakati anazindua barabara, akasema atabanabana huko alete ambulance, Je inawezekanaje katika zama izi zakutumbua afisa ugavi ofisi ya mkulu aagize ambulance bila idhini?

2. Vichwa vya treni, Je?, inawezekana km mkulu aliagiza km alivyoagiza ndege mpya bila kufuata budget na kwasababu wadau wengi walimkosoa kuwa hafuati budget ameamua kuvumbua madudu bandari???then kuwakabidhi TRL

Nawaza tu???
Je, kuna uwezekano km ndege zingekuwa zinapitia bandari, angevumbua ndege mpya tano zilizotelekezwa bandarini na kisha kuwakabidhi ATCL?

Kwa wale wanaosubiri kuambiwa mmiliki wa vichwa vya treni na ambulance, tuwe na imani km ya wakristu kuwa Yesu atarudi.
 

Castr

JF-Expert Member
Apr 5, 2014
19,937
2,000
Huyu Afisa wa TPA huyu itakua ameshuka toka Malawi alipokua anaishi kwa miaka sita, kadakwa juu kwa juu kapelekwa kwenye kipindi, asingejibu hivi.

Na kama kuna registry za kuonyesha kitu kinapotoka na kinapoenda kwanini walivyoona hivyo vitu wakaviripoti kwa rais wakati registry ipo?
 

Lupweko

JF-Expert Member
Mar 26, 2009
13,689
2,000
Afisa wa TPA; alijibu kuwa wao ndiyo waliompa Raisi taarifa kuwa scanner yao imeona container ya mitumba ambayo ndani yake kuna magari na siyo raisi ndiyo aliyevumbua hayo ni scanner za TPA, akaendelea zaidi kuwa wanampango wakufunga scanner zingine.
Huyo afisa hajitakii mema kuwepo kazini, maana anataka kugeuza upepo wa sifa zote uliomuangukia mtukufu ubadilike kwenda kwa TPA
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom