Da'Vinci
JF-Expert Member
- Dec 1, 2016
- 35,675
- 106,781
THE POWER OF BEING THANKSFULL
Habarii..
Katika maisha yangu ya kila siku hua nayaweka mbele maneno haya matatu ambayo ni Pole, samahani na Ahsante. Leo nitazungumzia neno Ahsante, ni neno dogo lakini lililojaa Nguvu kubwa sana kiroho..upande wangu hajalishi nimepewa nini lazima nitoe shukrani kwa kile nilichofanyiwa na hua naona neno ahsante pekee halitoshi. Hata kama nimekula kwa mama ntilie lazima niseme ahsante tena nitoe na vyombo. Ifuatayo Ni mifano ya ukweli ya faida niliyopata kwa kupenda kutoa shukrani kwa kile nilichopatiwa au kukiona kikanifurahisha.
Biblia inatuambia nini………….??????
Kwakutumia mifano na mafundisho ya kibiblia hebu tuangalie jinsi mtu mmoja alivyopata neema ya wokovu kwa kusema tu ahsante, alimshukuru Yesu baada ya kumtibu magonjwa aliyokua nayo
Luka 17:13-19
“………Alipokua aaingia katika kijiji kimoja, watu kumi wnye ukoma walikutana nae wakasimama kwa mbali, wakapaza sauti yao wakisema Yesu mwalimu tuonee huruma! Alipowaona akawambia nendeni mkajionyeshi kwa makuhani, basi ikawa walipokua wanakwenda wakatakasika na kupona ukoma wao, mmoja wao alirudi na akamtukuza Mungu kwa sauti kubwa. Akajitupa chini mbele ya miguu ya Yesu huku akimshukuru, huyo alikua msamaria. Hapo yesu akasema Je , si watu kumi walitakaswa? Wale tisa wako wapi? Hakupatikana mwingine aliyerudi kumtukuza Mungu? Kisha akamwambia huyo mtu Simama nenda zako imani yako imekuponya.”
Wakuu kama tulivyoona hapo kwenye andiko yaani kati ya watu 10 waliopokea uponyaji ni mmoja tu aliyerudi kumshukuru yesu na kusema ahsante, hii ni ajabu! Mtu umepokea uatakaso lakini unashindwa kushukuru kwa neema hiyo.
Hata katika maisha ya kawaida watu wanafanyiwa mema lakini wanasahau kutoa shukrani tena wanaweza hata kulipa mabaya badala ya shukrani, mfano unalala usiku mzima hujui kinachoendelea pembeni yako! Mungu anakulinda usiku mzima na kukufikisha asubuhi salama lakini ukiamka tu unaamka kama mbuzi cha kwanza unafungua simu kuchungulia JF na mitandao ya kijamii mingine unasahau hata kumwambia Ahsante Mungu kwa kuniamsha salama. Unajiikia vibaya ukimpatia mtu msaada hafu asikushukuru, si ndio? Bas hivyo mdivyo ilivyo hata kwa Mungu! Anfurhi kuona watoto wake wanamshukuru….Imagine ulikua hufahamu kitu Fulani unafungua JF unakuta hiko kitu/mada unaisoma unavutiwa nayo unashindwa kumshukuru kwa kukuelimisha lakini hata kama huto mshukuru mpongeze tu au like post yake itamfanya atabasamu.
Kama mlivyooa hapo juu ni neno la shukrani tu ndio lilimfanya mkoma Yule apate neemaya utakaso! Ngugu yangu mm nawewe ni nani mpaka tushindwe kusema neno ahsante??? Haigharimu kitu kusema ahsante… kwanini usimshukuru Mtu aliyekusaidia jambo,Mungu aliyekulinda siku nzima?
“Sema ahsante kwa Yule aliyekufanyia jambo linalokufurahisha usiposema atakata tama kufanya lile linalokufurahisha”
Imeandikwa na:-
~Da’Vinci
JF Expert Member
Tchao

- Kukutana na mwandishi wa vitabu Dar es Salaam
- Nilivyokutana na Mwalimu wa Lugha ya Kihispania