Leo, moyo wangu umejaa furaha kubwa baada ya kuchangia tone la damu yangu katika bakuli la sadaka ya damu ya ukombozi wa taifa hili, likitanguliwa na ukombozi wa Arumeru mashariki!
Nikiwa katika mkakati wa tafuta kura, piga kura na linda kura-mkakati ambao umetuzalia matunda mema na kutoa ujumbe kwa taifa zima kile alichosema Dr. Lwaitama wa UDSM katika makala yake iliyobeba kichwa cha habari "CCM sells by date can not be extended" ilikuwa ni katika gazeti la The Citizen katika forum yake ya thinking critically! Nimejikuta nikishangilia matokeo hayo nikiwa katika chumba maalum cha kuhifadhia wahalifu maarufu kama sero kwa zaidi ya masaa 16 hivi mjini Arusha nikiwa na wenzangu 59 kwa pamoja tukifanya watu 60 baada ya afande mmoja kututangazia rasmi kuwa CDM imetangazwa mshindi Arumeru Mash, na kusababisha kelele za kushangilia zikisikika kutoka kila chumba cha mahabusu!
Ni baada ya kutimuliwa katika eneo la kutangazia kura nikipita uchochoro fulani hivi nikilenga kutokea leganga, mara nikajikuta niko katika geti la Gateway lodge, Mungu wangu wee sikujua kama CCM walikuwa wakiishi hapo tangu kampeni zianze na kikosi maalum kiitwacho green guard wakiwa wakitusubiri hapo mithiri ya simba mwenye njaa aonapo kitoweo pengine ni kutekeleza amri waliyopewa na wakuu wao huku wakiwa na mapanga, shoka, viboko, fimbo na silaha za kila aina niliona kama mafuta ya petrol (sina uhakika) maana hata hivyo haikutumika, walituteka nakutupiga mapanga na kila walichojisikia na kisha wakatusachi na kuchukua kila walichoona kinawafaa!
Baada ya kuridhika wakawapigia polisi wakaja kutuchukua! Mambo kadha wa kadha yalikuwa dhahiri katika tukio hilo
1. Polisi watakuwa wanawafahamu watu hao maana hawakuchukua hatua yoyote ya kutaka japo waondoke na mmojawao ili akatoe ushahidi/maelezo ya uhalifu tulioufanya pamoja na kwamba waliwakuta hapo! Hivyo napata nafasi ya kuhisi walifanya kazi kwa ushirika!
2.Wale watu walitumwa na CCM kulingana na kauli walizokuwa wakitoa kama, ninyi ndio mnajiita people people kitu gani, mmesoma shule za CCM halafu mnatuambia people hapa!
Shukurani
Napenda kutoa shukrani zangu za dhani kwa waheshimiwa viongozi wa CHADEMA kwa kutuhangaikia mpaka hivi sasa napata fursa ya kuandika thread hii nikiwa nyumbani baada ya kukandwa majeraha na kuwaona tena familia yangu ikiwa ni baada ya kushinda mauti yaliyotuvamia masaa takribani 18 yaliyopita. Tulimuona mhe. Mbowe usiku ule pale USA akihangaika na baadae tukahamishiwa mjini napo tumemuona Dr. Slaa na makamanda wengine waliofanikiwa sisi kupata dhamana!
Pia namshukuru Mungu mweza yote aliyenipa fursa hii ya kutoa mchango wa damu ya ukombozi huku akitunza nafasi ya uhai wetu ili kunipa nafasi tena ya kushuhudia. Uhimidiwe Mungu wangu!
Free at last! free at last! thank you God Almighty I am free at last!