Ahsante Mungu kwa kunipa nafasi ya kuchangia damu ya ukombozi wa taifa langu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ahsante Mungu kwa kunipa nafasi ya kuchangia damu ya ukombozi wa taifa langu!

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by nsami, Apr 2, 2012.

 1. n

  nsami Senior Member

  #1
  Apr 2, 2012
  Joined: Jun 11, 2010
  Messages: 175
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Leo, moyo wangu umejaa furaha kubwa baada ya kuchangia tone la damu yangu katika bakuli la sadaka ya damu ya ukombozi wa taifa hili, likitanguliwa na ukombozi wa Arumeru mashariki!

  Nikiwa katika mkakati wa tafuta kura, piga kura na linda kura-mkakati ambao umetuzalia matunda mema na kutoa ujumbe kwa taifa zima kile alichosema Dr. Lwaitama wa UDSM katika makala yake iliyobeba kichwa cha habari "CCM sells by date can not be extended" ilikuwa ni katika gazeti la The Citizen katika forum yake ya thinking critically! Nimejikuta nikishangilia matokeo hayo nikiwa katika chumba maalum cha kuhifadhia wahalifu maarufu kama sero kwa zaidi ya masaa 16 hivi mjini Arusha nikiwa na wenzangu 59 kwa pamoja tukifanya watu 60 baada ya afande mmoja kututangazia rasmi kuwa CDM imetangazwa mshindi Arumeru Mash, na kusababisha kelele za kushangilia zikisikika kutoka kila chumba cha mahabusu!

  Ni baada ya kutimuliwa katika eneo la kutangazia kura nikipita uchochoro fulani hivi nikilenga kutokea leganga, mara nikajikuta niko katika geti la Gateway lodge, Mungu wangu wee sikujua kama CCM walikuwa wakiishi hapo tangu kampeni zianze na kikosi maalum kiitwacho green guard wakiwa wakitusubiri hapo mithiri ya simba mwenye njaa aonapo kitoweo pengine ni kutekeleza amri waliyopewa na wakuu wao huku wakiwa na mapanga, shoka, viboko, fimbo na silaha za kila aina niliona kama mafuta ya petrol (sina uhakika) maana hata hivyo haikutumika, walituteka nakutupiga mapanga na kila walichojisikia na kisha wakatusachi na kuchukua kila walichoona kinawafaa!

  Baada ya kuridhika wakawapigia polisi wakaja kutuchukua! Mambo kadha wa kadha yalikuwa dhahiri katika tukio hilo

  1. Polisi watakuwa wanawafahamu watu hao maana hawakuchukua hatua yoyote ya kutaka japo waondoke na mmojawao ili akatoe ushahidi/maelezo ya uhalifu tulioufanya pamoja na kwamba waliwakuta hapo! Hivyo napata nafasi ya kuhisi walifanya kazi kwa ushirika!

  2.Wale watu walitumwa na CCM kulingana na kauli walizokuwa wakitoa kama, ninyi ndio mnajiita people people kitu gani, mmesoma shule za CCM halafu mnatuambia people hapa!

  Shukurani
  Napenda kutoa shukrani zangu za dhani kwa waheshimiwa viongozi wa CHADEMA kwa kutuhangaikia mpaka hivi sasa napata fursa ya kuandika thread hii nikiwa nyumbani baada ya kukandwa majeraha na kuwaona tena familia yangu ikiwa ni baada ya kushinda mauti yaliyotuvamia masaa takribani 18 yaliyopita. Tulimuona mhe. Mbowe usiku ule pale USA akihangaika na baadae tukahamishiwa mjini napo tumemuona Dr. Slaa na makamanda wengine waliofanikiwa sisi kupata dhamana!

  Pia namshukuru Mungu mweza yote aliyenipa fursa hii ya kutoa mchango wa damu ya ukombozi huku akitunza nafasi ya uhai wetu ili kunipa nafasi tena ya kushuhudia. Uhimidiwe Mungu wangu!

  Free at last! free at last! thank you God Almighty I am free at last!
   
 2. Ta Muganyizi

  Ta Muganyizi JF Gold Member

  #2
  Apr 2, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 5,134
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  Pole sana kwa yaliyokupa pia hongera kwa damu hiyo japokuwa bado uko hai..............Mungu akuzidishie neema na ujasiri ili uwe shuhuda wa mapinduzi yajayo. Asante
   
 3. RUMANYIKA

  RUMANYIKA JF-Expert Member

  #3
  Apr 2, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 315
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Duu! Nchi hii ni zaidi ya tuijuavyo. Pole sana na kila lenye heri lina ubarikio wake.
   
 4. e

  eng_stan Member

  #4
  Apr 2, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  pole sana. Mapambano dhidi ya ufisadi yana gharama. Damu yako ni chachu ya mapinduzi halisi
   
 5. S

  SUWI JF-Expert Member

  #5
  Apr 2, 2012
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 548
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Hongera sana... Mungu aendelee kukutia nguvu na ujasiri wewe pamoja na WT wote wanaokutana na hali kama hii.
   
 6. luhala

  luhala JF-Expert Member

  #6
  Apr 2, 2012
  Joined: Feb 25, 2012
  Messages: 412
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  Kitendo hicho kingefanywa na wafuasi wa CHADEMA jambo hilo lingetangazwa wiki nzima na vilaza wao TBC, Clouds na wengineo, lakini tuseme nini basi? Ukiwa mwana CCM (Chama Cha Majambazi) ni ruksa kutenda lolote na Polisi itakulinda tu. Ziko wapi propaganda za eti CHADEMA ni chama cha vurugu? waliowajeruhi wabunge Mwanza ni CHADEMA? Na hawa waliowajeruhi kwa mapanga wananchi wasio na hatia kule Arumeru nao ni CHADEMA? Ziko wapi kelele za kulaani? Hakuna ila zitasikika kwa nguvu kama wafuasi wa CHADEMA watalipiza kisasi kwa kufanya hivyo kwa viongozi wa CCM hata kama watakuwa wamemwagia michanga tu itatangazwa mwezi mzima.
  Kama Jeshi la Polisi na vyombo vya dola vitashindwa kuwapata wahalifu hawa na kuwachukulia hatua, wana CHADEMA tutakuwa tayari kujichukulia hatua mikononi ili haki itendeke. Mnaonaje?
   
 7. Goodrich

  Goodrich JF-Expert Member

  #7
  Apr 2, 2012
  Joined: Jan 29, 2012
  Messages: 2,050
  Likes Received: 632
  Trophy Points: 280
  Pole sana Mkuu. Pia Hongera sana, maana kazi tunayoifanya leo ni kwa manufaa ya wajukuu zetu. Mbegu huwa inakufa ndio yanatokea mazao mapya !!!
   
 8. n

  nsami Senior Member

  #8
  Apr 2, 2012
  Joined: Jun 11, 2010
  Messages: 175
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nawashukuruni sana wana JF kwa kunitia moyo!

  I don't blame anybody! All I know is, every changes must be accompanied by some related cost and some are life threatening.
   
 9. Idimulwa

  Idimulwa JF-Expert Member

  #9
  Apr 2, 2012
  Joined: May 27, 2011
  Messages: 3,384
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  So sad...!!!Pole sana kiongozi...Lakini yote yana mwisho.
   
 10. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #10
  Apr 2, 2012
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Nkunya, your pains and suffering will not be in vain.
  Those lives that were lost in Soweto, the suffering and embarrassment that was subjected to the likes of Madiba, helped cleanse the continent of Africa of the most inhumane governments of our times. If only if there were not brave brothers and sisters to support the course . Madiba would still be classified as a terrorist, not the great statesman he is today.
  Aluta Continua
   
 11. Shapu

  Shapu JF-Expert Member

  #11
  Apr 2, 2012
  Joined: Jan 17, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 240
  Trophy Points: 160
  i can see more lights at the end of the tunnel! kati ya kosa kubwa ccm walilofanya ni kuruhusu huu uchaguzi washindwe!! Impact ni kubwa kuliko!!
   
 12. m

  maramojatu Senior Member

  #12
  Apr 2, 2012
  Joined: Mar 16, 2012
  Messages: 145
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Nataka kukutia moyo kwamba sio wewe peke yako uliyechangia damu tupo wengi na nafikiri hili litatuunganisha kwenye kuhakikisha mgonjwa wetu tanzania anapona. Cccm inapita lakini tanzania itabaki milele. Mungu ibariki tanzania mungu wabariki watanzania
   
 13. Gwankaja Gwakilingo

  Gwankaja Gwakilingo JF-Expert Member

  #13
  Apr 2, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 1,963
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Pole sana Comrade hakika damu uliyoimwaga pale Arumeru itamea na kuzaa matunda ya ukombozi wa Watanzania wote ambao wananyanyaswa na kuonewa,"Comrade the jouney is not long when freedom is the destination"amini kwamba wewe na wenzako ni kitovu cha vuguvugu la ujombozi utakaotapakaa tanznia nzima,USIKATE TAMAA tuko pamoja
   
 14. m

  madam wasatu Member

  #14
  Apr 2, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  machozi yamenitoka, pole sn kaka yangu.Mungu akupe neema ya kuona siku cdm tutakapoikomboa nchi na udhalimu wa ccm.itakuwa ni furaha kuu, hakika utafutwa machozi
   
 15. d

  dada jane JF-Expert Member

  #15
  Apr 2, 2012
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 566
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Pole sana lkn ukombozi una gharama kubwa hata Mungu mwenyewe ili awakombea wana wa Israel Misri ilibidi damu ya kila mzaliwa wa kwanza imwagike na pia ili wanadamu wote tukombolewe ilimwagika damu za Yesu kristo imwagike. So umefanya jambo zito. Ubarikiwe.
   
 16. M

  Melanoxylon Member

  #16
  Apr 2, 2012
  Joined: Nov 13, 2011
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Pole sana kamanda freedom is comming 2mor. Ki ukweli inatia uchungu
   
 17. Amani Nyekele

  Amani Nyekele Senior Member

  #17
  Apr 2, 2012
  Joined: Jul 8, 2011
  Messages: 159
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  pole sana!! huruma imeniingia kwa mambo mabaya uliyofanyiwa...!!! nakupa sana pole ndugu yangu...!! Mungu yupo upande wako...! Binafsi sifurahii kabisa tabia ya kujichukulia sheria mkononi....!!
   
 18. marejesho

  marejesho JF-Expert Member

  #18
  Apr 2, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 6,539
  Likes Received: 830
  Trophy Points: 280
  Pole sana ,na pia HONGERA SANA!!!!
   
 19. k

  kajunju JF-Expert Member

  #19
  Apr 2, 2012
  Joined: Jun 30, 2011
  Messages: 986
  Likes Received: 79
  Trophy Points: 45
  Pole sana. Shetan ameshndwa na mungu amefanya kazi yake.kuna rafiki yangu murundi alipigana vita ya msituni. Baada ya kushnda cdd fdd yeye akawa meya. Nilimuuliza maoni yake ikizingatia angeweza fia vitani. Alisema 'unaweza usiende kwenye mapambano lakini ukafa,baada ya machafuko kuanza na damu yako ikanywewa na mbwa lakini ukipigania nchi ata ukifa tone la damu linamwagika kwa ajiri ya ukombozi wa nchi'. Mungu yu pamoja nawe!
   
 20. 3D.

  3D. JF-Expert Member

  #20
  Apr 2, 2012
  Joined: Sep 7, 2010
  Messages: 1,022
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Pole sana Mkuu M. M. Nkunya kwa yaliyokupata. Hongera kwa ushujaa na Mwenyezi Mungu akuzidishie mara dufu.
   
Loading...