Ahsante "Mr Clean" Mwamba wa Uadilifu, Hayati Benjamin Mkapa kwa kutuletea Rais John Pombe Magufuli

Leslie Mbena

JF-Expert Member
Nov 24, 2019
207
677
AHSANTE "MR CLEAN" MWAMBA WA UADILIFU,HAYATI BENJAMIN MKAPA KWA KUTULETEA RAIS JOHN POMBE MAGUFULI

Leo 12:45pm 25/07/2020

Ni huzuni kubwa kwetu Watanzania kuondokewa na Rais Mstaafu Benjamin William Mkapa,Shujaa wetu na Mwamba wa fikra na mawazo yaliyofumbatwa na uadilifu, bidii, usawa, mshikamano na uvumilivu.

Akiwa Rais Mstaafu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,tutamkumbuka Hayati Benjamin William Mkapa kwa utendaji wake wa kazi uliosadifu kwa dhati fadhila na tunu za msingi kwa maisha ya Watanzania,

Tutamkumbuka Rais Mstaafu Benjamin William Mkapa kwa Uzalendo uliotukuka kwa Taifa la Tanzania,imani, Matumaini na Mapendo kwa Mungu na unyenyekevu uliotukuka kwa Watanzania aliowahudumia kwa Miaka yote ya uhai wake,

Watanzania tunahuzunika kuondokewa na mpendwa wetu Benjamin William Mkapa lakini pia tunasherehekea maisha yake hapa duniani, hasa shabaha yake ya msingi ya kuchangia kutanabahisha kiongozi huyu mwafrika na Mtanzania kweli kweli aliyejibidiisha kusarifu kwamba siasa ni ''tunu faradhi ya upendo kwa sababu lengo lake ni kukuza faida na maendeleo ya Waafrika na Watanzania wote,

Kumtafakari Benjamin William Mkapa, fikra na mchango wake kwa maendeleo endelevu Tanzania, Afrika na uliwenguni kote ni kukumbuka fikra ya kukuza maendeleo fungamani ya Watanzania, waafrika na ulimwengu mzima.

Benjamin William Mkapa hakutoa nafasi wala kuendekeza upendeleo binafsi kwake wala kwa familia yake, bali alihimiza "kufyekelea" mbali matabaka ya kiuchumi, kikabila au kikanda. Alitilia mkazo watu wote kueshimiana licha ya tofauti zao kidini, kinasaba au kikabila,

Benjamin William Mkapa alikuwa na busara kujiepusha na hila za mataifa ya kigeni mintarafu amani, umoja na maendeleo fungamani ya Tanzania na Afrika katika ujumla wake. Kama kiongozi makini Benjamin Mkapa alisimama kidete kuunda umoja miongoni mwa waafrika kama ilivyokuwa adhma na bidii ya Mwalimu Julius Nyerere.

-Ahsante kwa kutuletea Rais John Pombe Magufuli.

Mwaka 1995 ulituibulia "chuma" mbeba maono na mtenda kazi Rais John Pombe Magufuli,ulikuwa mtu mwenye roho kama ya Yohana Mbatizaji,katika mwili wa Nabii Elia,ukamuinua John Pombe Joseph Magufuli na kumtawaza kuwa Askari wako shupavu kati ya Askari wako wa miamvuli katika baraza lako la Mawaziri,

John Pombe Magufuli sasa ni Rais wa Tanzania wa awamu ya Tano,2015-2025,Amefufua ndoto za Mwalimu Julius Nyerere za kupambana na maradhi,umaskini na elimu,kwa sasa elimu ni bure,uchumi tumeingia wa kati,

Huduma za afya zimeboreshwa,viongozi hawatibiwi nje,Sekta yetu ya afya imepewa uweza,imejiamini na sasa tuna Madaktari bingwa na wanatibu Watanzania hapa hapa Tanzania.

Rais John Pombe Magufuli anachukia rushwa na anapambana nayo kwa gharama zote,na wala rushwa si viongozi wa umma tena,wamebaki wachache kama wajumbe wa mkutano mkuu wa tawi,kata na Wilaya.

Ukifika mwambie Mwalimu Julius Nyerere,tunamuenzi ila yupo Mwanafunzi wake anatembea katika njia yake,nae ni John Pombe Magufulia,tukiangalia chini tunaona barabara nzuri, tukiangalia juu tunaona ndege za atcl,

John Pombe Magufuli amelifufua shirika lako ttcl,John Pombe Magufuli amelijenga bwawa la Rufiji na amelipa jina Bwawa la Umeme la Julius Nyerere,Mwanafunzi wako John Pombe Magufuli amehamishia makao Makuu ya Nchi kuwa Dodoma,sawa sawa na mapenzi yako na ndoto yako ilivyokuwa.

Tunasikitika mmeondoka lakini mmetuachia mwanafunzi wanu John Pombe Joseph Ahsanteni sana,John Joseph Pombe Magufuli amechukua dhana ya jumuiko la mawazo mazuri ya watangulizi wake wote na kuyaweka katika vitendo na sasa hivi Tanzania inang'ara.

Ukikutana tu na Mwalimu Nyerere mwambie aichungulie Dodoma, aangalie Rufiji mambo yanavyokwenda, aangalie madini aliyotuonya subirini watanzania wasome waje wachimbe kwa faida na sasa tunachimba kwa faida na Saniniu Laizer ni bilionea wa kwanza aliyetokana na rasilimali yetu ya madini,

Mkumbushe kutuombea bado donda ndugu la rushwa katika uchaguzi linatutesa atusaidie kumwambia Mungu ampe nguvu John Pombe Magufuli ya kulishinda hili nalo hata ikimlazimu kuteua aliyepata zero kwa haki,tunaamini Mungu atatusaidia,tutalishinda na hili pia.

Nimalizie kwa nukuu ya Mwalimu Julius Nyerere wakati wa kura za maoni za urais ndani ya CCM mwaka 1995,zilizobakisha wagombea watatu Jakaya Kikwete, Benjamin Mkapa na Cleopa Msuya wakisubiri Mkutano Mkuu wa kuteua Mgombea mmoja ataepeperusha bendera ya CCM,

Watanzania walikuwa wanasubiri na kudadisi kujua Mwalimu Julius Nyerere alikuwa anamtaka nani,katika maongezi na wageni wake Mwalimu alisimulia jinsi ambavyo wagombea, katika mkutano wao wa NEC, Halmashauri Kuu ya CCM, walikuwa wamechuana vikali,

Mwalimu Nyerere alisema “Pale Dodoma tumeshinda pesa za bangi,Sisi tumo ndani tunajadiliana namna ya kupata mgombea bora, kule nje ya ukumbi kuna watu walikuwa na pesa za bangi wanatafuta raisi,Nafurahi kwamba tumewashinda…”

Katika kuwaenzi Hayati Mwalimu Julius Nyerere na Mzee Benjamin William Mkapa,Mungu atuongoze tukawashinde wote walioshinda,wanaoshinda na watakaoshinda kwa rushwa na pesa za bangi,Daima tutawakumbuka na kuwaenzi Viongozi wetu,Pumzika kwa amani Mzee wetu Benjamin William Mkapa.

Nikiishia hapa,Mimi ni,
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854.

-Bachelor of Business Administration in International Business.
-Master's in Leadership and Management.

-Research; Assessing Effects of Micro-Financing on Poverty Reduction.
 
Mr Clean aliyejigawia mgodi wa Kiwira??? Mr clean aliyewaua wazanzibar mwaka 2001??? Mr clean aliyejigawia mashamba kilombero???

Mr clean aliyejipa zawadi za madini kila alipotembelea migodi??? Mr clean aliyeuza nyumba za serikali saivi viongozi hawana pa kukaa??? Mr clean aliyebinafsisha mashirika ya umma kwa bei ya kutupa???!

Najua unatafuta uteuzi. Kwanza matokeo yako sijui ubungo/ Kibamba kura za maoni yalikuwaje ???
 
"Mwaka 1995 ulituibulia "chuma" mbeba maono na mtenda kazi Rais John Pombe Magufuli"

Rekebisha mwaka ,ni 2015
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom