Ahsante JK kwa Uungwana | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ahsante JK kwa Uungwana

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by QUALITY, Mar 16, 2011.

 1. QUALITY

  QUALITY JF-Expert Member

  #1
  Mar 16, 2011
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Leo kidogo nimeanza kufarijika ingawaje bado nina wasiwasi kama maelekezo ya Jk yatatekelezwa.

  Leo saa 12 asubuhu, kupitia BBC, nimemsikia Kikwete akisema wataalamu wakae pamoja ili kuona namna ya kukabiliana na mfumuko wa bei nchini ili kupunguza ugumu wa maisha kwa watanzania.

  Taarifa hii imenifariji kidogo kwa vile imekuja siku chache tangu chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania kufanya maandamano kanda ya ziwa na kuitaka serikali kutoa tamko kuhusu ugumu wa maisha, mfumuko wa bei (hasa bei ya sukari) na ufisadi. JK ameisha ongelea bei ya sukari na kuagiza (ingawaje hakuna aliyetekeleza) sukari kuzwa sh 1,700. Leo ameongelea mfumuko wa bei unaosababisha ugumu wa maisha (mafisadi hajaongelea na bila shaka hatakuwa na jipya). Lakini kama anawasikiliza wapinzani na anatolea kauli itakuwa vyema. Ngoja tuone utekelezaji!
   
 2. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #2
  Mar 16, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Tumesikia wachumi wake Ikulu wametunukiwa nishani ya utendaji bora wa kimataifa, vipi tena washindwe kumshauri jambo la kufanya kunyanyua uchumi wa taifa.
   
 3. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #3
  Mar 16, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,107
  Likes Received: 22,154
  Trophy Points: 280
  Wangekuwa wameshindwa wangepataje hizo "nishani za kimataifa"?
   
 4. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #4
  Mar 16, 2011
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,795
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  ...usiwe na haraka ya kupongeza maneno. subiri matendo ndio utoe pongezi.
   
 5. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #5
  Mar 16, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,707
  Trophy Points: 280
  One premise does not lead to a valid conclusion. Hizo ahadi zimeanza lini na utekelezaji wake lini umeanza? Danganya toto tu hiyo! Ni ngumu kumuamini huyo mzee wa porojo!
   
 6. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #6
  Mar 16, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  lazima tukishukuru chadema angalau sasa kinaiendesha ikulu na kuweka katika mawazo ya watawala agenda za maisha ya wananchi wa kawaida. tuombe atende sasa hayo anayoyasema na ashughulikie ufisadi. imagine sukari inapanda kwa zaidi ya 30% eti wafanyabiashara wameificha na serikali haijamkamata yoyote kwa uhujumu uchumi, badala yake tunasikia wanabembelezwa waisambaze sukari iliyofichwa!

  kwa kweli inakatisha tamaa sana
   
 7. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #7
  Mar 16, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,785
  Likes Received: 2,397
  Trophy Points: 280
  Juzi niliona ilovo-kilombero sugar wanauza sasa sukari kwa sh 1500 kilo pale kamata dar wana ofisi!Ama kweli nchi hii bila mgomo ama maandamano mambo hayaendi
   
 8. Kurunzi

  Kurunzi JF-Expert Member

  #8
  Mar 16, 2011
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 4,006
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180
  JK, JK ..JK RAIS WANGU, Hivi mpaka leo hao wanauchumi hawajakaa na kuangalia tatizo hilo? My God! Nilifikiri walishafanya hivyo muda sasa umekuja na habiri mpya ya hatua za kuchukuwa kumbe ndo story imeanza sasa kunafaida gani ya kuwa na wanauchumi ambao mpaka uwashitue ndiyo wafanye kazi pana tatizo hapo muheshimiwa. Ok hata ilo agizo ulilotoa umelitoa kimzaa mzaa hivi nilitegemea ungesema nawaagiza wanauchumi wote mkutane ndani ya siku 14 mtuletee ripoti na nini cha kufanya .

  Ni hayo tu wana Jf.
   
 9. B

  Bobby JF-Expert Member

  #9
  Mar 16, 2011
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,682
  Likes Received: 197
  Trophy Points: 160
  Quality umenichanganya kidogo hapo kwenye bold, la sukari umesema katoa tamko na hakuna aliyetekeleza na of course kama kawaida yake yuko so relaxed as if hakutoa agizo lolote ambalo halijafanyiwa kazi. Sasa unatoa vipi pongezi wakati huyu aliyetoa agizo hili la mfumuko wa bei ndio huyo huyo alitoa agizo la bei ya sukari ambalo halijafanyiwa kazi? Halafu kituko kingine hao waliomkumbusha kuhusu bei ya sukari, mfumuko wa bei na mengineyo aliwaita wavunjifu wa amani kwa kitendo chao cha kuiamsha serikali toka usingizini na ameyakubali waliyoyapigia kelele, sasa sijuwi na yeye ni mvunjifu wa amani pia kama alivyo pm wake mtaalamu wa kulalamika pasipokuchukua hatua?
   
 10. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #10
  Mar 16, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,276
  Trophy Points: 280
  Mkwere ametoa ahadi 68 wakati wa kampeni na mpaka sasa alichofanya ni kwenda kuomba msaada wa robo ya bajaj alizoahidi, kama kuna binadamu mwenye akili timamu na sio akili mgando anategea lolote jipya kutoka kwa mtu huyu, basi nampa pole. nadhani anaota ndoto za mchana.
   
 11. A

  Awo JF-Expert Member

  #11
  Mar 16, 2011
  Joined: Apr 12, 2010
  Messages: 790
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 45
  Hili la kupunguza kodi ili kupunguza bei ya vitu amedesa kwa Gerald Hando aliyesema kwenye power breakfast jana asubuhi. Ni upuuzi Rais kutoa agizo kwa wataalam kukaa na kuja na suluhu. Alitakiwa akae yeye na washauri wake wa uchumi wapate suluhisho halafu ndio aje kwenye vyombo vya habari na kusema nini kifanyike. Aache kutoa maagizo, anamwagiza nani na kazi alioomba mwenyewe? Tuliompigia kura hatukuwachagua hao anaowaagiza, tulimchagua yeye hivyo afanye kazi yake.
   
 12. QUALITY

  QUALITY JF-Expert Member

  #12
  Mar 16, 2011
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Bobby, usishangae sana. Maana Kikwete ahadi alizotoa ahtekelezi ila anatekeleza zile zilizotolewa na CHADEMA. Mimi ninachompongeza ni usikivu kutoka kwa wenzetu waanaowasikilizaa wananchi CHADEMA. Hapo tu

  Sasa lawama haziishi kwa sababu yeye ni lazy fair leader, yaani kiongozi mshikaji. hana uwezo wa kukemea wala kufuatilia kama agizo lake alilotoa linafuatwa au la. hata pale anapogundua kuwa halikufuatwa, hachukui hatua. Anakaa kimya!!!

  Mchana mwema
   
 13. QUALITY

  QUALITY JF-Expert Member

  #13
  Mar 16, 2011
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  (Kwenye bold tafadhali) Inawezekana alisikia huko lakini hilo liko katika Ilani ya uchaguzi ya CHADEMA na walisema wazi wazi kuwa wataondoa kodi kwenye baadhi ya bidhaa kurahisha maisha ya watz. Wakati huo wa kampeni, JK alisema kuondoa kodi kwenye bidhaa haiwezekani, Leo imewezekanaje????????????
  :focus:
   
 14. m

  msosholisti Member

  #14
  Mar 16, 2011
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 60
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hata hao CDM wamekopi ilani ya uchaguzi kwa CUF. wale wachaga wakanywe mbege tu
   
 15. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #15
  Mar 16, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Zile siku 9 zimeisha tayari.....too late to meet the deadline
   
 16. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #16
  Mar 16, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Kazi ipo...kumbe Zitto nae anakunywa Mbege?
   
 17. K

  Kikambala Senior Member

  #17
  Mar 16, 2011
  Joined: Jun 28, 2008
  Messages: 163
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  hana mpya jana kaenda kuchekacheka hazina.Tra na bandarini baada ya miaka sita baada ya ziara ya kwanza mambo shaghala baghala
   
 18. MESTOD

  MESTOD JF-Expert Member

  #18
  Mar 16, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 4,641
  Likes Received: 142
  Trophy Points: 160
  Tatizo la kwetu hapa kuajiriwa kwa kujuana kwingi sana! Huwezi kumshurutisha mtoto wa shangazi, ukienda kumsalimu aunt itakuwaje wakati mwanae kakusemelea ulimfokea kazini? Iliyopo hata kwenye expense ya wengine lazima umbembeleze tuu. Au mpaka tukodi management ya kuendesha ikulu ndo nchi iende? Hapana hatujafika huko! Rais Mh sana toa matamko ukiwa serious, maana you have all signs of power. Ndo maana mzee unapoenda airport hata kabla hujatoka bafuni barabara zimeshafungwa. Katiba imekupa kila aina ya nguvu, itumie please kwa ajili yetu.
   
 19. MESTOD

  MESTOD JF-Expert Member

  #19
  Mar 16, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 4,641
  Likes Received: 142
  Trophy Points: 160
  Asimsahau Arfi Saidi, na Mchungaji Msigwa na Sugu aaaa, list kubwa. Nyie watu ukabila hadi wapi? Lakini huko nako tutawatoa tuu.
   
 20. M

  MZAWATA JF-Expert Member

  #20
  Mar 16, 2011
  Joined: Feb 10, 2011
  Messages: 555
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  huyu anatupiga changa la macho tu,hakuna jipya
   
Loading...