Ahsante JF kwa kunipatia mke wa pili….!

Haki yake kutokana na tamaduni zao, ila nafikiri bwana Mtambuzi hapo ange msaidia kama kawaida na kwa binadamu yoyote, sio mpaka amuoe yani amu weke ndani, Brother snowBall command si suruhisho wala kipimo cha mwanaume wa shoka.....
kwa mtaji huu utatukoma humu,tena ngoja nimwite madameb ,halafu na akija mwaJ atamaliza kesi huwezi kumuolea mke mwingine mama ngina tunashuhudia halafu unasema eti kuoa mjane ni thawabu!akh!eti Kaunga umesikia maneno ya huyu mzee wa ununio?
 
Yeah, waungwana wanasema like father like son….

Mimi nimetokea katika familia ya ndoa za mitala, baba yangu alikuwa na wake watatu, duh! Huyu alijipunja, kwani baba yake ambaye ni babu yangu yeye alikuwa na wake sita wenye maumbo makubwa kama cacico au charminglady….

Kwa kifupi ni kwamba kwa mila a desturi za kwetu kuoa wake wengi ni jambo lisilokwepeka…
Nimetanguliza maelezo hayo ili msije nitia vidole vya macho… (Nawajua sana wanawake wa humu JF, hasa huyu snowhite, BADILI TABIA, nyumba kubwa gfsonwin, Preta, na vidosho wengine, nasema mnikome…

Ni hivi, kuna binti mmoja ambaye ni mjane tumejuana humu humu JF, yeye ana umri wa miaka 26 na amefiwa na mumewe mwaka jana (Msiniulize amekufa kwa ugonjwa gani, mie sio ZIRAELI mtoa roho za watuna hiyio hainihusu) na kuachiwa mabinti wawili ambao ni mapacha wenye umri wa miaka 3… sasa kutokana na kwamba anakabiliwa na hali ngumu ya kutunza hiyo familia yake, nimeona ni vyema nimuoe, ili asije akaadhirika hapa mjini. Si mnajua ukioa mjane unapata Baraka kwaMungu..!

Kwani kuna ubaya gani kwa akina Ngina, king’asti na Cantalisia kupata wadogo zao mapacha, na pengine nitaongeza wengine hapo wa kwangu…..Vuteni subira nitawaalika kwenye sherehe ndogo ya ndoa itkayofanyika mwezi huu mwishoni huko Vikindu….

Ngoja nimepata mgeni kidogo, nitarudi muda mfupi ujao kuwapa taarifa zaidi…

Hivi hii ndoa ilishafungwa au ndio uliogopa vitisho?
 
ha ha haaaa Mtambuzi huo uzee wako uko wapi,
au ndo mbinu za kuwakimbia hao wakupendao?
jikongoje hivyo hivyo nasikia kuna majiko ya mkaa humo ndani.
Nawalia timing kama namchinja kobe vile...
Si unajua sisi wazee wakati mwingine mpaka kwa Hendeli kama nawasha yale magari ya kizamani ya kijerumani
 
Last edited by a moderator:
ha ha haaaa Mtambuzi huo uzee wako uko wapi,
au ndo mbinu za kuwakimbia hao wakupendao?
jikongoje hivyo hivyo nasikia kuna majiko ya mkaa humo ndani.

Natamani niwe na nguvu hizo, lakini na huu uzee jamani Mamndenyi nitaweza kweli sarakasi za hawa mabinti wa siku hizi wanaojua kujiviringisha kama chatu anaponasa windo lake, si nitakufa kwa mihemko...
Heri nijitafutie mzee mwenzangu tulishane ugoro maana huyo tutawezana, akitema mate huku na mie natema mate kule ngoma droo

depressed-black-man-getty590.jpg
 
ha ha haaa
pole weee Mamndenyi anauliza, muda umekwenda wapi Mtambuzi?
Natamani niwe na nguvu hizo, lakini na huu uzee jamani Mamndenyi nitaweza kweli sarakasi za hawa mabinti wa siku hizi wanaojua kujiviringisha kama chatu anaponasa windo lake, si nitakufa kwa mihemko...
Heri nijitafutie mzee mwenzangu tulishane ugoro maana huyo tutawezana, akitema mate huku na mie natema mate kule ngoma droo

depressed-black-man-getty590.jpg
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom