Ahsante JF kwa kunipatia mke wa pili….! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ahsante JF kwa kunipatia mke wa pili….!

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by Mtambuzi, Oct 1, 2012.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Oct 1, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Yeah, waungwana wanasema like father like son….

  Mimi nimetokea katika familia ya ndoa za mitala, baba yangu alikuwa na wake watatu, duh! Huyu alijipunja, kwani baba yake ambaye ni babu yangu yeye alikuwa na wake sita wenye maumbo makubwa kama cacico au charminglady….

  Kwa kifupi ni kwamba kwa mila a desturi za kwetu kuoa wake wengi ni jambo lisilokwepeka…
  Nimetanguliza maelezo hayo ili msije nitia vidole vya macho… (Nawajua sana wanawake wa humu JF, hasa huyu snowhite, BADILI TABIA, nyumba kubwa gfsonwin, Preta, na vidosho wengine, nasema mnikome…

  Ni hivi, kuna binti mmoja ambaye ni mjane tumejuana humu humu JF, yeye ana umri wa miaka 26 na amefiwa na mumewe mwaka jana (Msiniulize amekufa kwa ugonjwa gani, mie sio ZIRAELI mtoa roho za watuna hiyio hainihusu) na kuachiwa mabinti wawili ambao ni mapacha wenye umri wa miaka 3… sasa kutokana na kwamba anakabiliwa na hali ngumu ya kutunza hiyo familia yake, nimeona ni vyema nimuoe, ili asije akaadhirika hapa mjini. Si mnajua ukioa mjane unapata Baraka kwaMungu..!

  Kwani kuna ubaya gani kwa akina Ngina, king'asti na Cantalisia kupata wadogo zao mapacha, na pengine nitaongeza wengine hapo wa kwangu…..Vuteni subira nitawaalika kwenye sherehe ndogo ya ndoa itkayofanyika mwezi huu mwishoni huko Vikindu….

  Ngoja nimepata mgeni kidogo, nitarudi muda mfupi ujao kuwapa taarifa zaidi…
   
 2. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #2
  Oct 1, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,507
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  Hivi wapi wanauza sime mpya mpya?
   
 3. SnowBall

  SnowBall JF-Expert Member

  #3
  Oct 1, 2012
  Joined: Sep 13, 2011
  Messages: 3,067
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Mtambuzi mradi hautaagiza viagra ..i support you buddy..kidume lazima uwe na uwezo wa kucommand nyumba zaidi ya moja..lol
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 4. snowhite

  snowhite JF-Expert Member

  #4
  Oct 1, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 14,174
  Likes Received: 2,136
  Trophy Points: 280
  kwa mtaji huu utatukoma humu,tena ngoja nimwite madameb ,halafu na akija mwaJ atamaliza kesi huwezi kumuolea mke mwingine mama ngina tunashuhudia halafu unasema eti kuoa mjane ni thawabu!akh!eti Kaunga umesikia maneno ya huyu mzee wa ununio?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 5. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #5
  Oct 1, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,507
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  Mie kwanza namngojea huyo mjane ni nani? Manake asitafute mjane mwenzie akajitwalia, atuletee eda nyumbani kwetu?
  Umemuambia una mabinti rijali? Manake hapa ni kama wake wenza, tunagawana pocket money. Yaani leo patachimbika wallah!
   
 6. snowhite

  snowhite JF-Expert Member

  #6
  Oct 1, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 14,174
  Likes Received: 2,136
  Trophy Points: 280
  ahhhahhah we pacha humtakiii mema babu wa watu!sasa zile mingle zote za ujanani af sa hizi aoe mke wa pili tena binti mbichi wa miaka 26 si anataftia watu murder huyu!
   
 7. snowhite

  snowhite JF-Expert Member

  #7
  Oct 1, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 14,174
  Likes Received: 2,136
  Trophy Points: 280
  hhahhahahhahah sijui kama alilizingatia hili la mabinti rijali!
   
 8. charminglady

  charminglady JF-Expert Member

  #8
  Oct 1, 2012
  Joined: Apr 16, 2012
  Messages: 17,856
  Likes Received: 1,131
  Trophy Points: 280
  mh,mzee Mtambuzi nani kakwambia mie nina umbo kubwa? my huz C6 hebu njoo umwambie huyu mzee ka mie ni mnene au lah!!!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 9. cacico

  cacico JF-Expert Member

  #9
  Oct 1, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 8,392
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  babu mbona kuutangaza wasifu wangu hadharani???? ila hongera babu Mtambuzi kwa kufanya yale yaliyo mema! nitakuja vikindu!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 10. Madame B

  Madame B JF-Expert Member

  #10
  Oct 1, 2012
  Joined: Apr 9, 2012
  Messages: 24,128
  Likes Received: 4,994
  Trophy Points: 280
  [MENTION=96061]snowhite, mwaJ[/MENTION],
  hebu njooni tujitayarishe,
  Lile Pensi langu la Mauamaua umenionea wapi?

  Haiwezekani amuongezee majukumu Mama Ngina.
  Lazima tukafanye Tifu Vikindu watujue sie watoto wa Mikanjuni.
  Pigapiga mateke majungu yote ya Ubwabwa na Maharage.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 11. cacico

  cacico JF-Expert Member

  #11
  Oct 1, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 8,392
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  mmmhhhh! upo?? mi mithd u, lol
   
 12. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #12
  Oct 1, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,507
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  mi sijaelewa kabisa. Hii kampuni ya kusitiri wajane kaianzisha lini? Manake kuna mbaba mjane nataka kumuanzishia maza.
  :banghead:
   
 13. cacico

  cacico JF-Expert Member

  #13
  Oct 1, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 8,392
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  madameB upo mwali?? umenionea Asprin huko fyatanga?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 14. SnowBall

  SnowBall JF-Expert Member

  #14
  Oct 1, 2012
  Joined: Sep 13, 2011
  Messages: 3,067
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Ila Madame Bmusimuamini sana mzee wa ununio a.k.a Mtambuzi hachelewi kusepa huyu.......
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 15. Madame B

  Madame B JF-Expert Member

  #15
  Oct 1, 2012
  Joined: Apr 9, 2012
  Messages: 24,128
  Likes Received: 4,994
  Trophy Points: 280
  Nipo Mrembo cacico,
  Asprin mara ya mwisho nilimuona Kwenye Karandinga la Polisi.
  Nasikia kakamatwa ugoni na mke wa baba mwenye nyumba wake,
  Muda huu atakuwa anachezea vitasa Wazo Polisi.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 16. snowhite

  snowhite JF-Expert Member

  #16
  Oct 1, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 14,174
  Likes Received: 2,136
  Trophy Points: 280
  mpka asepe tushampa kibano cha haja ,haiwezekeni amchake mama ngina wa watu halafu aoe kigoli tena kilicho kijane halafu wala hataki kujua mume mwenzie marehemu yalimsibu yapi!atachezea kichapo huyu mpka asahau aliye mkewe ni nani!ahahahahhaahha King'asti na Madame B pamoja sana!kwanza tukaanzzie pale kwenye pub yake inawezekana ndo kale kalikuwa kanasave kwa bidii ile juzi kwenye birthday yake,maana mi baba yenu unafikiri namuamini?ah
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 17. Michael Scofield

  Michael Scofield JF-Expert Member

  #17
  Oct 1, 2012
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 1,218
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Ngoja ukachezeshwe viduku na huyo binti! mpaka naniliu zikukauke, alafu mwenzio ndio anakwambia bado nataka, we ndio kwanza umempa mgongo!! shauri zako! ndoa ndoano.
   
 18. Madame B

  Madame B JF-Expert Member

  #18
  Oct 1, 2012
  Joined: Apr 9, 2012
  Messages: 24,128
  Likes Received: 4,994
  Trophy Points: 280
  Akisepa tunamtimbia Maguu hadi kwake.
  Chezeiya.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 19. Nicas Mtei

  Nicas Mtei JF-Expert Member

  #19
  Oct 1, 2012
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 11,569
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Mkuu Mtambuzi kwa sasa nipo Ununio. Nimemwona kijana flani hvi mmfanana sana. Nadhan ni yule ulyenambia. Fanya mpango uje umgomboe. Anaish kwa bibi yake.
   
 20. snowhite

  snowhite JF-Expert Member

  #20
  Oct 1, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 14,174
  Likes Received: 2,136
  Trophy Points: 280
  au ni zile zawadi alizoletewa na kina Kaizer ndo kazibalisha kuwa za madafu af akaenda brela kusajili kampuni Kaizer unaona hasara ya kumtuza Mtambuzi kwa deutche mark?anaanza kuleta mbofu mbofu za kuleta frau mtambuzi the second!ah wapi!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Loading...