Ahsante Halotel kurejesha mabaki ya dk, internet na sms

Amoxlin

JF-Expert Member
May 30, 2016
3,784
4,089
Amani kwetu wana Jf.

Leo natumia nafasi hii kuupongeza uongozi mzima wa kampuni ya mawasiliano ya halotel kwa ubunifu wao mkubwa.

Kwa sasa kila unapojiunga na kifurushi chochote cha halotel na muda ukaisha bila kukimaliza basi utakapojiunga tena utajumlishiwa na kile ulichobakiza bila kumaliza ktk kifurushi kilichopita.

Pia gharama ya vifurushi vyao ni nzuri mfano. Tsh.1500 dk 100 mitandao yote wiki. Tsh.1000 dk 50 mitandao yote wiki. Tsh.1000 sms 5000 mwezi nk...

Kwa hili nitaendelea kuwa mteja wenu.
 
Halotel wako poa sana...kwa wanaolalamika data kwenda fasta mi nahisi inasababishwa na mtandao kuwa freshi (speedy) na simu kuwa na mambo mengi yanayohitaji updates...kama hutumii internet bora uzime data
 
Hivi unabakizaje mb mpaka wazile kabla ya muda..?
Mkuu mimi huwa natumia data kabla hazijaisha vizuri wananitumia sms ya ati zimebaki 20!. Ili niamini na hizo 20 kuwa zimeisha mpaka simu inionyeshe kimnara kwa pembeni ndo najua zimeisha.. unaposikia tunakula mpaka ukoko ndo sisi Sasa😜
 
Hahahah kwa matumizi hayo kwa siku 12 huwezi kuwa na tatizo mkuu. Endelea kuinjoy!
Kuna line za Royal /au vifurushi vya Royal???? ndzo unapata vifurushi hivyo! Alini convince mtu aliyetumia miezi mitatu bil shida. Lakini kama kawaida ya makampuni haya, ni wezi wanavuta watu, then mkiwa wengi wanabadilika! Let me try anyway!
 
Kuna line za Royal /au vifurushi vya Royal???? ndzo unapata vifurushi hivyo! Alini convince mtu aliyetumia miezi mitatu bil shida. Lakini kama kawaida ya makampuni haya, ni wezi wanavuta watu, then mkiwa wengi wanabadilika! Let me try anyway!
Mie nina Line ya Royal 4G! Hicho kifurushi nimejiunga 3 times in a row.

3.5GB za kasi ya 4G utazitumia within a week kama ni mtumiaji mzuri wa data. Instagram,Facebook,Youtube combined!

Baada ya hapo speed ya kobe mpaka mwezi uishe!
 
Halotel wako vizuri, nikijiunga bando langu hua linaisha kihalali kabisa na kwa sasa mtandao uko vizuri haunisumbui hata.
 
Sijawahi ibiwa na hawa watu toka 2015. Kifurushi kinapoisha hiwa napitia app inayotunza kumbukumbu za matumizi ya mb nakuta sawa kabisa.
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom