Ahmed Rajab: Nyerere na fitna za Upemba na Uunguja

akili za wazanzibari zimetawaiwa na uislam na kudai haki zao , mwarabu gani anayeitaka nchi iliyovurugwa ????

tanganyika yote na zanzibari yake zote hazikaliki angalia wengine wamekimbilia uingereza na kuingia kwenye
biashara hizi 38 Degrees | Save Eddy Cosmas

Hapo Unanishangaza kidogo, Tanganyika ipi haikaliki? ni maeneo gani ya Tanganyika hayakaliki? Ni Watanganyika au Wazanzibari ndio Wamekimbilia Uingereza kama Wakimbizi?

Na Hueleweki Wao wengi Wanaupenda U-Middle Eastern hawajioni kama Waafrika wenye Tamaduni za kiafrika na Ukaribu na Tanganyika...

Hatuongelei Udini, hapa tunaongelea Fitna kati ya Nyerere za Upemba na Uunguja.
 
Tatizo kuubwa lililopo katika nchi za Afrika na hasa Tanzania (Zanzibar), ni kutukuza asili za baadhi ya watu na asili za mawazo ya dini. Hili ni tatizo kubwa linaloendelea kusumbuwa. Kwa nini hatuwezi tukawa na mawazo huru ya kujithamini sisi na kujitukuza kama bin-Adam na nchi? Mimi huwa natizama tatizo hilo kwa ujumla wake katika misingi ifuatayo...

(1) Tanzania ni nchi ya Mungu kama nchi zingine.
Tanzania ina watu walioumbwa na Mungu kama ilivyo kwa mataifa mengine ya dunia. Je kwa nini sisi tusimwoneshe huyo Mungu wetu uwezo wetu wa ibada ya kweli na watu wa Oman wakashangaa na kuiga kutoka kwetu? Kwa nini sisi tusiombe duwaa zetu na ibada zetu zinazoweza kupokelewa na Mwenyezi Mungu hadi tukabarikiwa? Kwa nini bado tunaendelea kutukuza Oman tu? Vatican tu? Israel tu? Kwani wao sio watu kama sisi? Huu ni ujinga na upumbavu uliosheheni upunguwani kwenye vichwa vya watu wajinga wasio na ufahamu bali kutukuza ujinga na giza ....

(2) Kama sisi tunaamini watu wote ni bin-Adam kwa 100%, kwanini tunashindwa kujithamini kama bin-Adam wengine? Kwa nini lazima tuone fahari kujitambuliswa kuwa mimi ni Mwarabu hata kama ngozi yako ni kama ya Maganga Onyango bin Matonya? Kwani Mwarabu ndiyo nani basi? Kama tukijithamini na tukijiamini tunaweza kufanya maajabu mapya ambayo yaliwashinda waarabu wa zamani na wa sasa. Americans rose to become a powerful nation kwa sababu ya kujiamini. Na wala hutakuta wakihangaika kutafuta wametoka wapi..kule kuna watu wenye asili ya Africa, Europe, Asia na Middle East...lakini mara zote wanajitambulisha kama Americans. Obama ni mtu ya Kenya, lakini huoni akihangaika na Kenya zaidi ya Amerika. Mtizamo wa namna hiyo ungeweza kusaidia nchi ya Tanzania kupona...lakini sasa haitawezekana kwa sababu wengine..ni wa-Arab na wanataka arabic culture iwe na more influence katika nchi, wengine ni wa-Islam na wanataka nchi iwe ya ki-Islam zaidi... kwasababu jambo hilo halitawezekana matokeo yake ni kuwa nchi hii itaingia kwenye vurugu hapo baadae.

(3) Kama Tanzania ni nchi ya Mungu, na kama wa-Tanzania ni bin-Adam 100% sasa kwa nini tusiwe na mashujaa wetu kama Mwenyeheri Nyerere? Hayati Karume? Chief Mirambo, Chief Mareale, nk. Kuwatambua mashujaa wetu ni kujitambua kuwa sisi pia ni watu 100% tuliojaaliwa uwezo wa kuwaza na kutenda mambo makubwa na ya kushangaza.

Kukosekana kwa mambo hayo, kama Ahmed Rajab alivyoonesha, ni dalili ya kubakiwa na mawazo ya utumwa na uduni wa kuwaza na kupambanua mambo katika mazingira yanayotuzunguka. Haya ni makovu ya utumwa. Huu ni ugonjwa kama ukoma ambao ni sumu ya maendeleo kwa Ahmed na wenzake
 
Hapo Unanishangaza kidogo, Tanganyika ipi haikaliki? ni maeneo gani ya Tanganyika hayakaliki? Ni Watanganyika au Wazanzibari ndio Wamekimbilia Uingereza kama Wakimbizi?

Na Hueleweki Wao wengi Wanaupenda U-Middle Eastern hawajioni kama Waafrika wenye Tamaduni za kiafrika na Ukaribu na Tanganyika...

Hatuongelei Udini, hapa tunaongelea Fitna kati ya Nyerere za Upemba na Uunguja.

Labda unaishi dunia nyengine huko UK , na ulaya kwa jumla kumejaa watu wa Tanganyika waliokimbia na kuchukua ukimbizi ukienda Marekani ndio hakusemeki kila kona wapo .

Tuje na hiyo mada ya uunguja na upemba , wewe unaona huo ubaguzi haukulenga dini lakini msikilize Peter Smith katika kitabu chake anasema kitu gani kuhusu Nyerere

Imani Petro Mbinu za makafiri 5 13 - YouTube
 
Nithibitishie kama Marekani na Uingereza inachukua Wakimbizi wa kisiasa

kutoka Tanganyika; Walichukuwa Wa Zanzibar/Pemba wakati ule

wa Utawala wa Mkapa lakini hawakuchukua wa Tanganyika Hata kidogo na

Walichukukua Ukimbizi kwa Sababu Gani tena? Amerika Ukisema wewe ni

Mtanganyika Unataka Ukimbizi Unapewa Ndege na Ticket Kurudi Bongo; Wapo

wanaosema ni Warundi, Wanyarwanda hapo wabongo wako wa hivyo...
 
Nithibitishie kama Marekani na Uingereza inachukua Wakimbizi wa kisiasa

kutoka Tanganyika; Walichukuwa Wa Zanzibar/Pemba wakati ule

wa Utawala wa Mkapa lakini hawakuchukua wa Tanganyika Hata kidogo na

Walichukukua Ukimbizi kwa Sababu Gani tena? Amerika Ukisema wewe ni

Mtanganyika Unataka Ukimbizi Unapewa Ndege na Ticket Kurudi Bongo;
Wapo

wanaosema ni Warundi, Wanyarwanda hapo wabongo wako wa hivyo...

kumbe unataka ubishi wakati jibu umeshalitoa mwenyewe huko mwisho !!!!
 
Hizi fitna za ‘Upemba’ na ‘Uunguja’, za ‘ubwana’ na ‘utwana’ na za ‘ugaidi’ wa Uamsho ni fitna zinazotiwa na watu walio maluuni. Lengo lao kubwa ni kuwapotosha Wazanzibari wauzime mjadala wa Muungano. Hawajali iwapo watalitimiza lengo hilo kwa kuyakiuka maadili ya uongozi au ya uandishi.

Ahmed Rajab, kwa nukuu hiyo ya juu itokayo katika makala yako inakuweka na wewe mwenyewe katika kundi lile la MALUUNI anaepotosha Watu nje ya UKWELI hasa Wapemba na Wazanzibari. Makala yako imeelemea upande mmoja, hivyo badala ya kujaribu kusaidia inaongeza Fitina pande zote husika na swala la Muungano.
Unachojaribu kusema ni kuwa Makanisa hayakuchomwa.
Uamsho ni watakatifu (Ati kwa sababu USAID) wanawafadhili (Bila shaka ni baba yao CIA aliyemfadhili BIN LADEN).
Kuwa Amiri Faridi wa Uamsho si Mwarabu.
Kuwa vurugu za 26/05/2012. Uamsho hawana hoja kabisa na vurugu hizo.(Hivi unaandika ukiwa London, Zanzibar au Dar?)

Yaani umeonyesha wazi Unafik na UDHAIFU wako, na kwa bahati Daraja lako umejipa mwenyewe 'MALUUNI'.

LOL... Nimekutega na umekubali ni Canada ndiko wanakokwenda... kweli haujui chochote

akili yako iko timamu ??? unajua unachokiandika ??? kwani hapa kuna samaki , au ndege wa kutega???

tizama umeandika mwenyewe huko juu kuwa hakuna pahala watanganyika wanakoomba hifadhi , mwisho ukamalizia nakunukuu Wapo wanaosema ni Warundi, Wanyarwanda hapo wabongo wako wa hivyo...

NI KITU GANI KINACHOWAFANYA WAIKIMBIE NCHI YAO NZURI WAKAJIBANDIKE URAIA WA NCHI NYENGINE ????

HAYO NDIYO MATUNDA YA NYERERE NA MUUNGANO WAKE , HUO UTANZANIA HAWAUTAKI HUWA UNALAZIMISHWA TU

MWISHO HAWAKO HUKU WALA KULE
 
Unaona Sasa haujui sababu ngoja nikusaidie tuache kuzungushana kuzunguka

mti nipate kizunguzungu bila sababu Lakini wakati Mwingine Jaribu

kuongelea issue ukiwa na uelewa na pia sababu; Sio kudakia bila sababu

inaondoa Umaarufu wa JAMII FORUMS...

HAYA SABABU YA WATANGANYIKA KUWA WARUNDI AU WANYARWANDA SIO KUWA

WANAIKIMBIA TANGANYIKA NI KWA SABABU WAKIFIKA AMERICA AU CANADA NI SHIDA

KUPATA VIBALI VYA KUFANYA KAZI AU RUHUSA YA KURUDI NYUMBANI KUTEMBELEA

MARA NYINGI KUOA LOCALS KUNA MATATIZO YAKE MARA NYINGI WARUNDI NA

WANYARWANDA WANAOCHUKULIWA WALIISHI KWENYE MAKAMBI BONGO WENGI WAO

WANAONGEA KISWAHILI NA WANAIPENDA TANZANIA, HAWAONI SHIDA KUWASAIDIA

WATANZANIA NA WAO KUPATA HUO MSAADA WA KUPATA HAYO MAKARATASI NA SIO

KAMA WAKIMBIZI KWAHIYO WANAZURI TANZANIA KAMA KAWAIDA NI JINSI YA KUISHI

NCHI ZA WATU NA NI KUTAFUTA MAISHA NDUGU YANGU; HAKUNA WA KUKATAZWA;

THERE IS ALWAYS SILVER LINING IN THE SKY FOR ANYONE WHO TRY TO SURVIVE...
 
Mkuu Ahmed Rajab utakuwa inaikana historia ya Zanzibar kwa sababu ya visingizio vya Nyerere. Ebu nikuulize ni Nyerere au mkoloni aliyeanzisha chama cha Hizbu? kisha chama kinachoitwa Afroshiraz kwa maana chama cha watu weusi na Washiraz? na Ni Nyerere aliyewaambia kina Babu kuondoka Hizbu kuunda Umma Party - chama ambacho kitatetea maslahi ya maskini wakulima wa Zanzibar ambao walikuwa wakinyanyaswa?. Kwa nini yalikuwepo makundi haya awali hata kabla ya Uhuru au Nyerere ndiye sababu?..

Bila shaka kabisa kwamba alotuweka ktk hali hii alikuwa mkoloni mwenyewe nasi tukaitikia Hewallah bwana na kuunda vyama hivyo haikuwa Nyerere. Hata bara kulikuwa na vyama vya makabila mbali kabisa na TAA au TANU na mgawanyioko huu ulitokana na imani zetu wenyewe kuwa dhaifu. Halafu ajabu ni kwamba unatuletea habari za kiongozi wa UAMSHO iwe mwarabu au mweusi lakini unasahau jambo moja tu kwamba ni wewe umeanza kwa kusema "Kheri ya mja ni ulimi wake na shari ya mja ni huo huo.." Lakini maajabu umeshindwa kupima maneno yako mwenyewe na yale ya UAMSHO yanavyopokelewa na wengine kwa sababu yanakugusa wewe kwa manufaa yako kama yalivyokuwa yakiwagusa watu wengine walokuwa upande wa Nyerere.

Pili, umedai pia Nyerere aliwahi kusema hakuna WATU waswahili sijui wewe unafikiria vipi maana kweli hakuna watu waswahili isipokuwa ipo lugha ya kiswahili iloongewa na watu wenye asili tofauti. Wapo weusi na waarabu waloongea kiswahili (lugha) na hawajui lugha nyingine zaidi ya kiswahili huitwa waswahili kwa sababu ya lugha yao lakini hakuna kabila la waswahili as a genetic name kwa asili ya watu hao na lugha yao. Wapo watu weusi Sudan wasioongea lugha nyingine isipokuwa kiarabu. Hawa watu sii waarabu (genetically) isipokuwa wanazungumza kiarabu - lugha ya mawasiliano.

Tatu, swala la serikali ya Umoja wa kimataifa ni seriikali ya Zanzibar ambayo kama kuna upinzani utatoka Zanzibar kwa nini iwe swala la bara?. Kama Karume na Maalim Seif ndio walokubaliana mkapiga kura bila kuvihusisha vyama vingine vya Upinzani huko huko Zanzibar wala viongozi wao, inakuwaje swala hili liwe la bara. Na je sii kweli Makamba alihusika pia na utaweza vipi kuigawa CCM bara na visiwani? maswali haya mmewahi kujiuliza kwanza kabla ya kutuvamia bara kama ndio sababu ya kutovunjika kwa muungano.

Halafu pengine unasahau kwamba sii mara ya kwanza kutokea ushirikiano wa vyama Zanzibar au serikali ya umoja wa kimataifa. Kabla ya Uhuru wa mwaka 1963 vyama viwili vilishirikiana vile vile kwa sababu ya kumwonda mkoloni na vikaunda serikali ya kimataifa lakini maajabu lengo kuu likuwa kumrudisha Sultan ambaye alikuwa mtawala chini ya hifadhi ya Muingereza. Na walifanya makusudi kuwanyima ushindi AfroShiraz ambao walijipanga vizuri kupata ushindi.
Haya leo hii yale yale kama Dejavuu yametokea tena baina ya CCM na CUF Zanzibar kuunda mseto mwingine ambao ni kuhakikisha CCM inaendelea kutawala Zanzibar, lakini kwa wasiojua wanafikiri ni kutafuta utetezi wa Wazanzibar ktk serikali yao na maajabu hasira za Wazanzibar zinakwenda bara wakati walojipanga wao wenyewe kufikia maamuzi hayo ikiwa suluhisho la kero za muungano.

Mkuu wangu labda nikwambie tu ya kwamba ktk SIASA kama kweli UAMSHO ni watetezi wa dini na siasa basi waelewe tu ya kwamba huwezi kutetea haki za wananchi kwa kutaka kuuvunja Muungano isipokuwa mkubali bila unafiki kwamba hamkubali pia MAPINDUZI maana muungano ndilo chimbuko la Mapinduzi ya mwaka 1964. Tumesema sana na tutarudia kusema kama kweli mnataka kujitenga basi la kwanza kabisa ni kuvunja baraza la Mapinduzi ambalo ndilo lilotuingiza ktk yamin tulokula.

Na maadam madai yenu ni kwamba hakuna hatari zozote za kuhofia ama kuyalinda Mapinfdduzi sasa baraza lile la nini hadi leo ktk nchi ambayo ina vyama vingi? livunjeni na muunde Mfumo mpya wa Zanzibar inayolindwa na kutetewa na vyombo vyake vya serikali iwe ya mseto au mihimili yake. Na kinachowashinda kipi haswa kufanya zoezi la kura za maoni ikiwa hili ni swala lenu wenyewe lakini UAMSHO na viongozi wengine kazi kubwa wanayoifanya ni kutangaza uadui wao na bara.

Huku bara hata siku moja hutawasikia wakinyoosha kidole na kusema wana uadui na Visiwani japokuwa viongozi wengi wa visiwani wameshika madaraka makubwa bara. Na mwisho, pengine nimalizie kwa kusema ya kwamba dini hata siku moja sio suluhisho la maisha ya binadamu bali ni mwongozo sahihi ambao unampa binadamu alotihaniwa njia bora za ibada zake na anatakiwa kuamini na kufuata au kutoufuata iwe hata kula chakula ama kusali na kufunga. Nitarudia kusema hivi Uislaam ni dini ya Mwenyezi Mungu sii ya Sheikh Rajab wala Fareed, hata Mtume Muhammad (SAW) alikuwa muislaam aliyewajibika kufanya Ibada tofauti kabisa na maneno ya kuwa Waislaam ni WATU wafuasi wa Muhammad kama walivyo Wayahudi wafuasi wa Juda na wakristu wafuasi wa Yesu. Sisi sote ni Ummat Muhammad na tunaombeana dua kila siku ya Mwenyezi Mungu atunusu atusitir sote na dunai hii, pengine nimalizie tu kwa kusema Tofauti baina yako wewe na Kafir ni ibada maana hata Kafir anaweza kufanya mema yote na pengine mazuri zaidi yako isipokuwa asichoweza ni Sala tu.

You ain't any better than anyone isipokuwa kwa mwenye Mwenyezi Mungu ndiye mjuzi wa wajuzi wote. Fanya ibada zako itangazeni dini kwa wale wasioamini na sio kuanzisha uhasama na kuupotosha Uislaam ambao lengo lake ni kuwaokoa hata wale wasioamini. Hakuna aya hata moja inayosisitiza kuvunja Muungano wa WATU kwa sababu za kisiasa na madai ya NCHI huru. Uislaam unatazama uhuru wa watu wake ktk kufanya ibada na sio kuendesha utawala unaofanya haramu zote..
 
salim ahmed salim ni fitna za watanganyika wenyewe sio wazanzibar kwa nini zanzibar kuna wahindi warabu mawaziri lakini ni mkapa na watanganyika wenzenu ndio walitumia fitna hiyoo
 
Mkandara,

Ahali yangu skuli ni muhimu sana kwa mja kusoma. Na msomi yoyote kwanza anaanza kutafiti jambo kabla kulitolea kauli, hii ni kujiepusha na propaganda na ushabiki. Sasa kabla ya kutaka kukusaidia kidogo kuhusu UAMSHO, labda ningependa kukuuliza yafuatayo.
1. nilipo blue. Je unaweza kutubainishi nini malengo ya UAMSHO na nini madai ya dhidi ya muungano wenu?
nafikiri ukilijua hili basi usingeandika yote uliyoeleza.

Lakin la pili mimi nilitaka niendelee na hiyyo hiyyo hotba ya JK Nyerere ambayo mimi nimeipa jina la "Dhambi ya Ubaguzi" ambapo alisema kuna wazanzibar na wazanzibara.

Kama uliisikiliza yote kuna sehemu alisema alipoalikwa chakula na Getrude Mongela pale Washington na kukutana na mama wa kiganda ... Nilichotaka kubainisha hapa pale aliposema yeye aliwashawishi rais wa Uganda na Kenya waungane ili kupunguza ukabila uliomo ndani yya nchi zao.

lakin Nyerere huyo huyo aliyeweza kutambua nchi za kenya na Uganda kulikuwa kuna ukabila alishindwa kubainisha kuwa nchini kwake Tanganyika kulikuwa na UDINI mkubwa sana. Na kwa kutaka kulificha hilo aliamua kuunganisha na Znz ili kuuwa nguvu za watanganyika waislam ndani nchi yao.

Kumbuka kuwa Nyerere huyo huyo alitumia nguvu zake zote kuuwa taasisi ya waislam wa Afr mashariki na kuunda Bakwata. Kisha huyo huyo tena akakazania kuunwa kwa EAC. kweli kuna mambo. Labda bila kukuficha agenda ya udini ilifichika sana ndani ya watanganyika hususan waislam kwa sababu tu ya Muungano ambao waislam wengi viongozi ndani ya muungano wenu na uongozi wa juu walitokea Znz.

Nakuhakikishi ukivunjika Muungano tu basi Tanganyika lazima mtapambana kuhusu udini kwani hata hao mnaosema kuwa walikuwa hawasoma sasa wamesha elevika na wamesoma wanataka kila kitu pasu kwa pasu. Na Dalili zote zipo wazi. Mfano kauli ya mtei kuhusu tume ya kukusanya maoni ya katiba, madudu yaliyofanywa na baraza la mitihani kwa watahiniwa wa kiislam na sasa kuhusu Sensa

Mficha maradhi kifo ndio hicho. tunawapa pole. Znz hata siku moja haijawahi kuwa na vurugu za Kidini. sasa leo zinaokea wapi? Iweje aslimia 99.8% wagombane na less than 1% tena wengi toka Tanganyika.

Tafuta ukweli badala ya kunasa kwenye propaganda.
 
Je unaweza kutubainishi nini malengo ya UAMSHO na nini madai ya dhidi ya muungano wenu?

Ahlan Baru baru. Ukweli unabaki kuwa hakuna anayeweza kusimama na kueleza kwa kina malengo halisi ya UAMSHO. Hiyo ni siri yao na kwa mbahati mbaya au nzuri inajidhihiri bila kutaraji.

Kwa kufuatilia mijadala na hoja zao tu juu juu, lengo la UAMSHO ni kutaka Zanzibar ijitenge na bara kwa vile kuvia kwa maendeleo ya visiwani ni matokeo ya unyonyaji wa Tanganyika. Ingawa hawajaweza kutetea unyonyaji huo kwa mantiki na akili hilo ni moja ya mambo wanayoyapigia kelele.

Lengo la pili ni kurudisha utamaduni wa Zanzibar wa kiisalam ulioharibiwa na muungano. Zanzibar ikijitenga basi ujambazi, umalaya, ushoga na ubazazi wote unaopelekwa na wabara na si raia mwingine utafutika.
Hapo dola ya kiislam itatawala hasa kwa kuzingatia kuwa upo uhusiano wa kindugu na kidamu kati ya Zanzibar na Uarabuni.

Ili kufanikiwa katika malengo hayo, UAMSHO wanaamini kuwa kuondoa Watanganyika kwa jina la machogo ni sehemu muhimu. Ili kuungwa mkono ni lazima wawashambulie wakristo kwanza. Sababu za kumshambulia wakristo hazipo isipokuwa kwa kumuunganisha Nyerere na imani yake. Nyerere ni conduit tu lakini lengo ni Mtanganyika.

Ninachoweza kusema hapa nikuwa lengo la UAMSHO ni kubwa sana kuliko unavyosikia au unavyoelewa.
Hata Wazanzibar hawajui isipokuwa kikundi kinachopata ufadhili kutoka Oman.

Kuna jambo linanisikitisha sana na sijui kwanini Wazanzibar hawalielewi au wana unafiki kiasi hicho.
Ungeelewa madhara yaliyotokana na kuvunjika kwa EAC sijui kama kuna mtu angesimama kusema Nyerere alivunja EAC
Huu ni ujinga wala si uongo. Inaweza kuwa sipo sahihi na hapa ndipo nakuuliza Baru baru swali lifuatalo

Nyerere alisimamiaje kuua EAC kama ulivyosema. Hebu tuhabarishe
 
Mkandara,

Ahali yangu skuli ni muhimu sana kwa mja kusoma. Na msomi yoyote kwanza anaanza kutafiti jambo kabla kulitolea kauli, hii ni kujiepusha na propaganda na ushabiki. Sasa kabla ya kutaka kukusaidia kidogo kuhusu UAMSHO, labda ningependa kukuuliza yafuatayo.
1. nilipo blue. Je unaweza kutubainishi nini malengo ya UAMSHO na nini madai ya dhidi ya muungano wenu?
nafikiri ukilijua hili basi usingeandika yote uliyoeleza.

Lakin la pili mimi nilitaka niendelee na hiyyo hiyyo hotba ya JK Nyerere ambayo mimi nimeipa jina la "Dhambi ya Ubaguzi" ambapo alisema kuna wazanzibar na wazanzibara.

Kama uliisikiliza yote kuna sehemu alisema alipoalikwa chakula na Getrude Mongela pale Washington na kukutana na mama wa kiganda ... Nilichotaka kubainisha hapa pale aliposema yeye aliwashawishi rais wa Uganda na Kenya waungane ili kupunguza ukabila uliomo ndani yya nchi zao.

lakin Nyerere huyo huyo aliyeweza kutambua nchi za kenya na Uganda kulikuwa kuna ukabila alishindwa kubainisha kuwa nchini kwake Tanganyika kulikuwa na UDINI mkubwa sana. Na kwa kutaka kulificha hilo aliamua kuunganisha na Znz ili kuuwa nguvu za watanganyika waislam ndani nchi yao.

Kumbuka kuwa Nyerere huyo huyo alitumia nguvu zake zote kuuwa taasisi ya waislam wa Afr mashariki na kuunda Bakwata. Kisha huyo huyo tena akakazania kuunwa kwa EAC. kweli kuna mambo. Labda bila kukuficha agenda ya udini ilifichika sana ndani ya watanganyika hususan waislam kwa sababu tu ya Muungano ambao waislam wengi viongozi ndani ya muungano wenu na uongozi wa juu walitokea Znz.

Nakuhakikishi ukivunjika Muungano tu basi Tanganyika lazima mtapambana kuhusu udini kwani hata hao mnaosema kuwa walikuwa hawasoma sasa wamesha elevika na wamesoma wanataka kila kitu pasu kwa pasu. Na Dalili zote zipo wazi. Mfano kauli ya mtei kuhusu tume ya kukusanya maoni ya katiba, madudu yaliyofanywa na baraza la mitihani kwa watahiniwa wa kiislam na sasa kuhusu Sensa

Mficha maradhi kifo ndio hicho. tunawapa pole. Znz hata siku moja haijawahi kuwa na vurugu za Kidini. sasa leo zinaokea wapi? Iweje aslimia 99.8% wagombane na less than 1% tena wengi toka Tanganyika.

Tafuta ukweli badala ya kunasa kwenye propaganda.
Umeanza na kuniuliza swali ambalo sielewi unataka nikujibu malengo yapi?.. UAMSHO ni jumuiya ya Kiislaam. Hapa tayari unawajumuisha hata wananchi walioko bara, Kenya, Uganda na dunia nzima na malengo yake ni kuitangaza dini ya Mwenyezi Mungu haswa kwa wale wasioamini..

Sasa Jumuiya hii inapoacha kazi hii na kuzungumzia kuuvunja Muungano ambao unajumuisha waislaam wa bara na visiwani, unaondoa wajibu na malengo ya chombo hiki na kukifanya chama cha siasa cha Waislaam ambao hakuna kitu hicho isipokuwa kuna Islaam dini na ndio unatakiwa kuitetea. Badala ya kuiwezesha Jumuiya hii kuingia hadi nyumba ya Mkristu na Mpagani wakampa darsa kuhusu Uislaam na sio Waislaam ni watu gani ni dalili ya kupoteza malengo, kuwa na uongozi mbaya ambao unakiuka dini na hivyo kupoteza dira.

Kama chama cha dini ambacho kinatetea Watu wake ni jukumu la UAMSHO kuzungumza ama kupeleka malamishi yao kwa viongozi wa umoja wa serikali ya kimataifa ambao ni kazi yao kuchukua malalamishi haya na kuyafikisha inapotakiwa lakini haiwezekani UAMSHO kuchukua jukumu la serikali ya kimataifa na kuifanya yao KINAFIKI wakishindwa kuwakemea viongozi wao bali kuwapamba kwa sifa ati kwa sababu ni Waislaam.

Mkuu wangu unapoitangaza dini huendi kwa Waislaam bali kwa wale wasiokuwa waislaam. na hapa ndipo inapotakiwa hekima na unyenyekevu mkubwa sana ili upate kusikilizwa na hata kumvuta asiyeamini ktk Uislaam. Nimesema sana na nitazidi kusema Uislaam ni dini ya Mwenyezi Mungu sii yako wewe ulotoa shahada kama sehemu ya mwili wako. Sasa ebu nambie hao UAMSHO wataweza vipi kuingfia nyumba ya mkristu na kuitangaza dini?..Hii kazi haikuwa yao na kama kuna malalamishi yoyote tunasema Dr.Shein yupo, Bilal, Maalim Seif, Vuai, Nahodha hawa wote wameshika nafasi muhimu sana za utawala nchini na tayari wameisha sikia vilio vyenu waacheni waifanye kazi yao na kama wasipoleta majibu yanayoridhisha waulizeni wao na sii kueneza siasa za kibaguzi kisha mseme mchawi ni Nyerere kwa sababu tunaosema ni sisi Wabara basi kuna mahusiano na Nyerere.

Mkuu wangu kuna tofauti kubwa saa kati ya kuitafsiri hotuba ya mtu na kumtazama yeye anafanya nini. Kwa mfano Sheikh anayekemea Ubaguzi wakati yeye mwenyewe kaoa mke wa kabila au asili yake sii Ubaguzi. Ni muhimu wewe ulosoma ukaelewa kwamba nafsi zetu zina uchaguzi ambao hauwezi kuwa sababu ya kutokanya maovu. Muhimu ni ujumbe wenyewe unamlenga nani tofauti na UAMSHO wanavyodai haki ya Wazanzibar wakati wanaelewa vizuri kwamba kunyauka kwa embe kunatokana na mdudu aliyeko ndani ya kokwa.

Wazanzibar na Wazanzibara hawatengwi bara, hakuna historia ya hata mtu mmoja Mzanzibar wala Mzanzibara kutengwa bara, isipokuwa kwao ambako tumeyaona zamani na leo bado tunayaona mkililia Uhuru wenu pasipo kumshirikisha Mzanzibara. Hiyo serikali ya umoja wa kimataifa mliwashirikisha hata Wazanzibara? au ndio wametupwa hawahesabiki tena. Leo tupo ktk nchi moja yenye umoja wa Jamhuri na hamuwatambui Je mkijitenga itakuwaje?. bila shaka yatatungwa mengine maana ni rahisi sana kumlalamikia Nyerere kwa ukristu wake.

Wakati Nyerere akizungumzia swala la Ubaguzi ambalo lilikuwa raised na mama wa Kiganda ilikuwa kwanza kwa kusifiwa UMOJA wetu ndani ya nchi lakini mwalimu akamwambia sii kweli hatujawa na UMOJA huo kama anavyofikiria nasi tuna matatizo yetu. Kusema kuna Wazanzibar na Wazanzibara sio ubaguzi bali ni ukweli wa historia ya visiwa vile maana walikuwepo Wazanzibar waliohamia Bara na hubeba passport za bara japokuwa asili yao ni visiwani. Na mbona huko Zanzibar kwenyewe kuna watu hujiita Wangazija, Wayemen na WaOman hawa nao ni wabaguzi kwa sababu hutaja asili zao?.

Kuhusu Jumuiya ya Waislaam wa East Afrika, hii jumuiya siku zote waislaam wanapenda sana kumlalamikia Nyerere lakini pia wanashindwa kuelewa ya kwamba Waislaam wenyewe baada ya Uhuru waligawanyika makundi mawili, kuna wale (Hassan Bin Amir) waliojitenga na kina AbdulWahid na Mwapachu kwa sababu tu walikaribishwa wakristu kina Nyerere na iliwakwaza kuona Mkiristu anachukua leading role ktk struggle against Colonial rule. Wakajikata na wakaunda chama chao wenyewe kikiitwa - All Muslim National Union of Tanganyika (AMNUT). Na wala haikuwa Tanganyika tu hata Kenya kulikuwa na vyama vya kisiasa vya kiislaam tu wakati hakuna chama hata kimoja Tanganyika, Kenya, Zanzibar wala Uganda kilichokuwa cha Wakristu tu. Walokuwa wabaguzi kina nani?..

Halafu maajabu ya Mussa. hawa hawa walitaka kuipindua serikali ya TANU baada ya Uhuru bila kujali ya kwamba ndani ya TANU pia kulikuwepo waislaam isipokuwa wao ndio walijiona wabora zaidi kuliko waislaam woote nchini walopiga kura kuichagua TANU kuongoza nchi yao. Tofauti na Mapinduzi ya Zanzibar, Waislaam walitaka kuuondoa utawala wa TANU kwa sababu tu walitaka nchi iongozwe na waislaam na iwe ya Kiislaam..Halafu hata siku moja sijawasikia mnaodai kuwa Waislaam mkilaani kitendo hicho wala kuzungumzia coup iloshindikana kuwa ni uasi.

Sasa baada ya Mapinduzi kushindikana mlitaka Nyerere afanye nini? kama sii kutazama vyombo vyote vilivyokuwa affiliated na AMNUT kupigwa marufuku na waliokuwa mstari wa mbele kuvunja EAMWS walikuwa waislaam wenyewe kina Adam Nassib kwa sababu za kisiasa ambazo hata leo zinatumika. Ikiwa chombo chochote cha kijumuiya kinajihiusisha na ku sponsor Ugaidi ama kimejihusisha na mpango wa kuipindua serikali ulitaka serikali afanye nini?..

The only option ni kukipiga marufuku na kuunda chama ambacho kitakuwa controlled na serikali maana ni sisi wenyewe tulokwenda way over board kama leo navyowaona UAMSHO wakijaribu sana ku stage Mapinduzi kwa kuitumia dini. Tunawakanya kwa nia nzuri tu ya kwamba mnayoyafanya sii mazuri jamani itangazeni dini na sii kuingilia siasa za WATU maana dini sii watu bali Imani ya Uungu. This happened then na ina happen sasa kwa hiyo kuna uwezekanao mkubwa hata UAMSHO kikapigwa marufuku na msimlalamikie Nyerere wala Mungu.
 
Mkuu Mkandara,
Tuliwahi kumuuliza Mohamed Said,kama waislam ndio waliokuwa wengi na ndio walioleta uhuru peke yao, ilikuwaje basi hawakupigia kura chama cha AMNUT! MS hakuwa na jibu na sidhani Baru baru analo!
Endelea kutoa dozi mkuu
 
BWANA YESU ANAOKOA, KWA NINI MNAUMIZA AKILI HIVI?KWA NINI MNASONONEKA?KWA NINI MNAHANGAIKA NA HII DUNIA? MPE BWANA YESU MAISHA YAKO NA KUHAKIKISHIA HUTA JUTA,roho ya hasira,chuki na mambo mabaya yataondoka nawe utakuwa mwenye furaha muda wote.KARIBU KANISA LOLOTE LILILOKARIBU NAWE LINALOAMINI WOKOVU.
AU TUWASILIANE KWA EMAIL :johnhella2007@yahoo.com hiyo email naitumia hata facebook ukisearch kwa email hiyo utanipata
 
Back
Top Bottom