Ahmed Rajab: Nyerere na fitna za Upemba na Uunguja

Wazanzibari kwa sasa wanaonekana wako pamoja kwa kuwa wana-fight against a common enemy aitwaye muungano au Tanganyika lakini "wakishashinda vita hii" na kuipata "nchi yao" hawataishia hapo.

Watagundua kuwa Zanzibar siyo moja. Watatokea tena "wana uamsho" wengine wa kuidai pemba au Unguja. Kwa kuwa asilimia kama 99% ya wazanzibar ni waislamu hakutakuwa na hoja ya udini isipokuwa hoja kuu itakuwa ni ya u-pemba na u-unguja. Watataka kuwe na equal representation kila sehemu kati ya wapemba na waunguja (jambo ambalo si rahisi). This is too obvious. Watu wa pemba (CUF) wataona heri wajitenge na wa-Unguja (CCM).

Kuna mambo ambayo kwa sasa hayasemwi na watu wanaoitaka Zanzibar huru lakini wataanza kuyasema muungano ukivunja. Tusubiri muungano uuvunjike tuone
Labda nikuulize kidogo, kilichowaunganisha wapemba na waunguja ni kitu gani? Mkataba wa muungano au? Pemba ilikuwa na kiongozi tofauti na wa unguja? Wapemba au waunguja waliambiwa waungane?

Labda ukijibu hayo ndo utakuwa ushaindoaha wasiwasi ulokuwa nao kuhusu upemba na unguja, because itabidi CCM ibadilike na cuf ibadilike na viee vyama vya wazanzibari tu na sio vua muungano tena!
 
Labda nikuulize kidogo, kilichowaunganisha wapemba na waunguja ni kitu gani? Mkataba wa muungano au? Pemba ilikuwa na kiongozi tofauti na wa unguja? Wapemba au waunguja waliambiwa waungane?

Labda ukijibu hayo ndo utakuwa ushaindoaha wasiwasi ulokuwa nao kuhusu upemba na unguja, because itabidi CCM ibadilike na cuf ibadilike na viee vyama vya wazanzibari tu na sio vua muungano tena!

Kuna wale wazee ambao waliandika waraka umoja wa mataifa wakitaka msaada wa Pemba kujitenga na kuwa nchi. Nadhani hawa wazee walikuwa wanawakilisha kundi fulani ambalo bado lipo. Ni rahisi pemba kujitenga Zanzibar ikiwa nchi kamili kuliko kujitenga muungano ukiwepo.
 
Vipi yeye Ahmed Rajab, anaangukia upande gani kwenye maandishi yake mengi? Asije akafikiri mao aliyemsema Stalin alikuwa ana afadhali. Wote walikuwa great leaders who made great mistakes. Historia inathibitisha hivyo.
 
Mwalimu Julius Nyerere amekuwa akisifiwa kwa kila kitu, hata mimi namsifia kwa yale mazuri hasa kunisomesha bure. Lakini ni mara chache sana kusikia mtu akizungumzia udhaifu wake. Kwa maoni yangu Mwalimu alikuwa na:-

  • Udhaifu wa kuwapendelea wachache. Kuunganisha nchi mbili zenye idadi tofauti ya wananchi kuwa na uwakilishi na sauti sawa bila kujali wengi wape. Suala hili limefanya Zanzibar kuwa na sauti kubwa bila sababu yoyote. Nchi kama Marekani "electoral votes" zinaendana na idadi ya wananchi wa jimbo husika. Hata Tanzania Bara (Tanganyika) ingawa wabunge wanachaguliwa kutoka majimboni lakini idadi ya wabunge kwa kila mkoa inatofautiana kulingana na idadi ya watu. Ikumbukwe kwamba aliendelea na udhaifu huo mpaka wakati wa usuluhishi wa vita vya Burundi alipong'ang'ania kuwa pamoja na kuwa Wahutu ni wengi lakini Watusi walio wachache wawe na sauti mpaka suala hilo likaja kutatuliwa na Mandela alipoingia kuwa msuluhishi. Mandela aliwambia Watusi waziwazi kuwa wasiiyumbishe nchi kwa uchache wao. Matokeo yake ndio ukawepo mkataba wa Arusha.
  • Udhaifu wa kujipendela yeye mwenyewe, (sio kwa mali bali kwa madaraka). Aliamua kuwa wizara zote za Tanzania Bara ziwe ndani ya Muungano. Hii hakuifanyika kwa bahati mbaya. Alijua kuwa yeye ndie angekuwa Rais wa Muungano, kwa hiyo hakutaka kuachia Wizara zisizokuwa za Muungano kwa bara ziongozwe na mtu mwingine, akaziweka zote kwenye Muungano. Akasahau (maana yeye kama sehemu ya viongozi wale wa zamani hakujua kwamba iko siku ataondoka madarakani) kwamba iko siku Mzanzibar angeweza kuongoza Serikali ya Muungano. Angeweza kabisa kuweka ndani ya masharti ya Muungano kuwa ikiwa Rais wa Muungano atatoka Zanzibar basi serikali yote ya Muungano ijumuishe wizara zote za Zanzibar na Mtanganyika aongoze wizara zisizo za Muungano upande wa Tanzania Bara. Matokeo yake ndio tunayoyaona kuwa Mzanzibar anaongoza wizara inayohudumuia Bara tu kwa kuwa wizara zote za bara ziko ndani ya Muungano. Kwa mantiki hiyo Mzanzibar anaruhusiwa kuajiriwa ndani ya Serikali upande wa Bara kwa kuwa hiyo ni serikali ya Muungano lakini Mbara (Mtanganyika) hawezi kuajiriwa ndani ya serikali ya Zanzibar kwa kuwa sio serikali ya Muungano na yeye sio Mzanzibar. Kisa hofu ya kumezwa na wengi.

Mambo haya naamini kama yangeliamliwa vinginevyo basi tusingekuwa na mtafaruku kuhusu muungano kama tulionao sasa.
 
Nasema ivi, tangu nizaliwe zanzibar mpaka apa nlivokuwa hai sijawahi kusikia wazanzibari wenye asili ya kizanzibari wakibaguana, muungano na uvunjike kisha tuone wapi watu watabaguana. Ustaarabu wenyewe wabara wamefundishwa na hai wazanzibari, kujenga hawajui wamefumbuliwa mach. Kuna makabila 120, kuna wakiristo na waislam na mayahudi, kuna weupe na kuna weusi wenye asili ya kitanganyika, hebu twambieni kwanini pasiwe na machafuko ya kiubaguzi bara?

FYI zanzibar kabla ya mapinduzi ilikua na umoja wa watu wake, waingereza wakataka kuweka differences kwa makusudi ya kuweka chuki, wakawa wanawapanga waarabu katika vyeo vya juu, wahindi na washirazi kati na weusi mwisho, hiyo ni mipango ya mwingereza kama hamjui, Mfalme alikuwa just pambo tu la kuwatuliza watu wasije wakawageukia wazungu, wakataarisha mipango yao ya ubaguzi kisha nchi wakaipa uhuru wakijua kuwa tayari ubaguzi upo, na kukawa na chama hasa ambacho kimejibaguwa afro shirazi party, huku chama za Zpp kikiwa cha kila mtu bila ya kupiga kampeni za uasili. Ubaguzi huo ililetwa na mwingereza na kibaraka chao Nyenyere Maharage! Lakini muda umefika, zanzibar huru itapatikana na hatibaguliwa mtu! Propaganda zenu ni old model, ata CIA hawatumii izo siku izi! :D


Unauwezo mdogo sana wa kupambanua mambo, keep on dreaming!! Kwahiyo hivi ndovyo mkikusanywa kwenye mihadhara ya UAMSHO ndivyo mnavyokaririshwa!
 
Labda nikuulize kidogo, kilichowaunganisha wapemba na waunguja ni kitu gani? Mkataba wa muungano au? Pemba ilikuwa na kiongozi tofauti na wa unguja? Wapemba au waunguja waliambiwa waungane? Labda ukijibu hayo ndo utakuwa ushaindoaha wasiwasi ulokuwa nao kuhusu upemba na unguja, because itabidi CCM ibadilike na cuf ibadilike na viee vyama vya wazanzibari tu na sio vua muungano tena! :D

Kama utajua ni kwann si rahisi CCM kupata landslide victory pemba katka chaguzi yoyote ile basi utakuwa umepata jibu.
 
Sasa kwanini Halmashauri kuu Upande wa Zanzibar walimkataa Salim Ahmed Salim pendekezo la kuwa Rais wa Jamhuri ya

Muungano wa Tanzania? Mbona walimpachika Majina Mengi yasiyostahili?


Siyo hiyo tu, Salim Ahmed Salim alikuwa chaguo la Mwalimu Nyerere. Na kama alikuwa amewapiga gazi watu wasiweze kufikiri, ilikuwaje chaguo lake la kumrithi halikupita, badala yake akapitishwa Mzee ruksa? Tunapokuwa tunachambua tujaribu kuwa wakweli badala ya kupotosha hasa kwa vijana ambao hawakuwepo kwenye uongozi wa mwalimu - alistaafu mwaka 1985.
 
Wazanzibari kwa sasa wanaonekana wako pamoja kwa kuwa wana-fight against a common enemy aitwaye muungano au Tanganyika lakini "wakishashinda vita hii. Watagundua kuwa Zanzibar siyo moja. Watatokea tena "wana uamsho" wengine wa kuidai pemba au Unguja. Kwa kuwa asilimia kama 99% ya wazanzibar ni waislamu hakutakuwa na hoja ya udini isipokuwa hoja kuu itakuwa ni ya u-pemba na u-unguja. Watataka kuwe na equal representation kila sehemu kati ya wapemba na waunguja (jambo ambalo si rahisi). This is too obvious. Watu wa pemba (CUF) wataona heri wajitenge na wa-Unguja (CCM). Kuna mambo ambayo kwa sasa hayasemwi na watu wanaoitaka Zanzibar huru lakini wataanza kuyasema muungano ukivunja. Tusubiri muungano uuvunjike tuone

tuyaone kweli,mana 2tayaona meng kweli,
kwani nyinyi midanganyika mnaogopa nin wazanzibar wakibaguana waunguja na pemba,nyiny nd mlolileta lisubirini lije,bt mujue LIKIPULIZWA ZANZIBR LITACHEZWA BARA NA MAZIWA MAKUU
 
Sio kweli kwamba Nyerere alisema Muungano ukivunjika basi Unguja na Pemba zitabaguana lakini Bara watabaki shwari, uongo mkubwa! Na ukweli anaujua. Mwandishi unatia doa na aibu ukurasa wa makala za RAIA MWEMA. Kwa hiyo chochote anachoandika kuanzia hapo inabidi mtu uki dauti kwa sababu unajua una dili na mwandishi mwongo!


ulizaliwa baada ya kuanzishwa vyama vingi au baada kufa Nyerere??
 
Siyo hiyo tu, Salim Ahmed Salim alikuwa chaguo la Mwalimu Nyerere. Na kama alikuwa amewapiga gazi watu wasiweze kufikiri, ilikuwaje chaguo lake la kumrithi halikupita, badala yake akapitishwa Mzee ruksa? Tunapokuwa tunachambua tujaribu kuwa wakweli badala ya kupotosha hasa kwa vijana ambao hawakuwepo kwenye uongozi wa mwalimu - alistaafu mwaka 1985.

ndivyo alikuambia hivyo Nyerere kule Msasani
 
Kama utajua ni kwann si rahisi CCM kupata landslide victory pemba katka chaguzi yoyote ile basi utakuwa umepata jibu.

wewe umo kwenye ile Mafia ya REDET ya Mkandala???? au wewe ndiye mkandala mwenyewe ??
 
moja ya makosa makubwa aliyoyafanya nyerere kwa kusudi au kwa sadfa, ni hilo la kuwafanya wananchi wenzake waache kufikiri na wawe wanayafuata tu aliyokuwa akiyasema bila ya kuyazingatia au kuyapima.

ingekuwa bora kama mwandishi angeweza kufafanua zaidi nguvu aliyokuwa nayo nyerere ya kuwafanya wananchi wenzake waache kufikiri. Hivi kweli nyerere alitawala hata bongo zetu kiasi kwamba hatukuweza kufikiri wenyewe? Mbona tunampa hata sifa asizostahili?

kosa sio la nyerere ila babu na baba zetu waliokuwa wanafuta ili kuchumia tumbo, itakaje mtu akuambie ufanye mambo yasiyofaa nawe ufanye kisha umlaumu- upuuzi mkubwa

 
Siyo hiyo tu, Salim Ahmed Salim alikuwa chaguo la Mwalimu Nyerere. Na kama alikuwa amewapiga gazi watu wasiweze kufikiri, ilikuwaje chaguo lake la kumrithi halikupita, badala yake akapitishwa Mzee ruksa? Tunapokuwa tunachambua tujaribu kuwa wakweli badala ya kupotosha hasa kwa vijana ambao hawakuwepo kwenye uongozi wa mwalimu - alistaafu mwaka 1985.

Salim, Alijaribu tena wakati wa Kikwete hapo ndio walimsengenya Vibaya Sio wakati wa JK; Wakati wa JK Nyerere alisha Mprepare ALI HASSAN MWINYI kuwa Rais wa Muungano
 
Moja ya makosa makubwa aliyoyafanya Nyerere kwa kusudi au kwa sadfa, ni hilo la kuwafanya wananchi wenzake waache kufikiri na wawe wanayafuata tu aliyokuwa akiyasema bila ya kuyazingatia au kuyapima.

Ingekuwa bora kama mwandishi angeweza kufafanua zaidi nguvu aliyokuwa nayo Nyerere ya kuwafanya wananchi wenzake waache kufikiri. Hivi kweli Nyerere alitawala hata bongo zetu kiasi kwamba hatukuweza kufikiri wenyewe? Mbona tunampa hata sifa asizostahili?

Hadi loe watanganyika akili zao wamekatiwa na hayati nyerere, na bahati mbaya kesha kufa kwa hiyo kafa nazo, ndio maana unakuta watanganyika wanaendelea kunukuu kauli mbalimbali za nyerere hata zile zisizo na maana, wapo wanaomuona ni mtakatifu na kupigania jamii nzima ikubali hivyo.
 
Pamoja na kwamba nimekuwa Msomaji mzuri wa gazeti la Raia Mwema kuna baadhi ya mambo yamekuwa yananikera kuna mwandishi anaitwa Mwakyembe yeye siku zote makala zake huwa zinazungumzia Mbeya hana habari nyingine, yuko Karugendo yeye makala zake nyingi anazumgumzia Kagera ingawa mara chache anazungumzia maswala ya kitaifa mwingine ni huyu Ahmed Rajab amekuwa akizungumzia zaidi Zanzibar na hasa upande wa Pemba; ukisoma makala zake nyingi amekuwa anaegemea upande mmoja.

Nakubaliana naye Nyerere alikuwaa na makosa kama binaadamu wengine wowote na yako mengi lakini vile vile alikuwa na mazuri yake kikubwa alikuwa na uwezo wa kujenga hoja, hivyo tunatakiwa tuyaache mabaya yake na kufata mazuri yake.

Kuhusu Zanzibar hakukosea kuna tatizo kubwa la Unguja na Pemba na ndio maana Salim amekwamishaa mara mbili kuwa Rais wa Muungano mwanzo Nyerere alipostaafu na mara ya pili baada ya Mkapa kumaliza kipindi chake na wengi waliompinga ni watu wa unguja hivyo haiingii akilini kuwa leo hii wakitoka nje ya muungano watakuwaa kitu kimoja. Baada ya Mwinyi kuchaguliwa kuwa Rais wa muungano weengi walitegemea ambaye angemrithi kwa Zanzibar angekuwa Seif Shaarif Hamad lakin baada akachaaguliwa Idrisa Abdul Wakil ambaye alitawala kipindi kimoja wanae walimshauri asigombee tena kutokana na hali halisi ya kisiasa tofauti kubwa kati ya unguja na pemba ni kuwa pemba wanahisi wanatengwa ndio maana walienda Un kuomba kujitenga lakini watu wa Pemba wako salama zaidi kwenye huu muungano kuliko baadhi ya viongozi wao wanavyowaaminisha.

Swala la uamsho kuonana na mabalozi au viongozi wa magharibi walikutana kwa maslahi ya nani kwa sababu Marekani hii yenye nguvu ili kuungana walipigana vita kulazimisha muungano lakini Marekani hao hao ndio wanaongoza kuvunja muungano wa mataifa mengine.

Tatizo kubwa tulilo nalo watanzania ni kuamini watu wa mataifa ya nje ndio wanaweza kuleta suluhu ya matatizo yetu. Tunajua kuna tetesi Pemba kuna mafuta unategemea mataifa kama Marekani yasitafute ushawishi kwa gharama yoyote lakini kuna watu ambao wengi wao ambao walikimbilia nchi km Oman baada ya mapinduzi wanataka kurudi huku kwa mlango wa nyuma.

Mwisho namuomba mwandishi asipotoshe ukweli kwani ukweli unajulikana tukishatengana itafatia unguja na Pemba au mauaji zaidi ya yaliyotokea Rwanda
 
Swadakta. Makala imetulia tuli.

Haya wanaharakati za kuchonganisha watu njooni tuwasikie.

Tunaomba link ya ilikokotolewa hii makala.

Kwa kweli mwandishi huyo ameandika makala ndefu lakini pia ni nzuri.
Alichokiandika ni jinsi anavyofikiri yeye, na naamini hajatumwa na mtu. Ni mawazo yake, ambayo wenye kutaka kuyaamini na kuyafuata ruksa na wasiotaka nao pia ruksa.

Kwa staili yiyo hiyo aliyoyasema Hayati Nyerere ni mawazo yake na utabiri wake. Si lazima kuyaamini na kuyafuata, ila anayeona yana ukweli atayaamini na kinyume chake pia ruksa.

Sasa Bwana mkubwa Ahmed Rajab (mwandishi maarufu na wa kuheshimika) asilazimishe kwamba Hayati Nyerere alikosea na kwamba yeye pekee ndiye yuko sahihi, hapana ni makosa.

Zanzibar siyo koloni, ni nchi huru ndani ya jamhuri ya Tanzania. Wana baraza lao la kutunga sheria (Baraza la Wawakilishi). Kinachowaogopesha leo hii kupitisha sheria ya kutoutambua Muungano na kuwa nchi yenye mamlaka kamili ni nini?

Waamue leo hii na tuone baada ya hapo nani alikuwa sahihi kuhusu matokeo ya Zanzibar kujitenga, ni Mkuu Ahmed Rajab au Hayati Mwl. Nyerere?
 
Marehem Mwalim Mwenye Heri.

Ujinga ni kushabikia hata ambacho Ahmed ankipinga ambacho ni CCM!

Punguza ujinga utaelewa kwamba we are fighting the same fight na acha kushabikia ujinga wa CCM!
 
Sio kweli kwamba Nyerere alisema Muungano ukivunjika basi Unguja na Pemba zitabaguana lakini Bara watabaki shwari, uongo mkubwa! Na ukweli anaujua. Mwandishi unatia doa na aibu ukurasa wa makala za RAIA MWEMA. Kwa hiyo chochote anachoandika kuanzia hapo inabidi mtu uki dauti kwa sababu unajua una dili na mwandishi mwongo!

Simlaumu mwandishi huyo, maana amandika kwa kadri ya muono wake akitokea visiwani.Pekua zaidi na utagundua itikadi na muelekeo wake katika jamii.
 
Ujinga ni kushabikia hata ambacho Ahmed ankipinga ambacho ni CCM!

Punguza ujinga utaelewa kwamba we are fighting the same fight na acha kushabikia ujinga wa CCM!


Kama anapinga CCM mimi nashangilia ukweli au kuna tatizo hapo?

Au hizo ni hasira za kuongezewa kodi ya mvinyo?
 
Asante sana Ahmed Rajab.

Naona umemchambua vilivyo "Mwenye Heri"

Uchambuzi gani wenye uongo dhahiri? Mfano, mfarakano utawabagua --------------------, huo ni upotofu dhahiri ambao unafanya uchambuzi wote kunuka mavi. Kumbuka uongo huzaa chuki, chuki huzaa mfarakano na vita. Mwandishi na wanaomuunga mkono wana kasoro itakayowatafuna hadi kaburini.
 
Back
Top Bottom