Bwana Ahmed Rajab, kwanini usipendekezee tu kuvunjwa muungano? mkataba wa nini tena, tusije koseana kwenye vipengere vya huo mkataba then tukaanza kupelekana mahakani tena, mi nafikiri kama unayo hoja juu ya muungano, washawishi tu wazanzibar wenzio muuvunje tu huu muungano na kila moja awe na chake, simple as that, kumsingizia JK Nyerere kwamba hata katika vyama vingi alikataa muungano usijadiriwe hiyo ni uongo, kwa muislam kama wewe kuongea uongo ni jambo baya sana, nadhani utakapo kwenda kupiga Rakaa leo kumbuka kumwomba msamaha muumba wako kwamba umemsingizia mtu, nakumbuka vizuri sana tena hata hotuba za mwalim bado ninazo, alilikemea kundi lile la G 55 juu ya hoja yao ya muungano, point yake ilikuwa hivi, "nyie ni wabunge wa CCM, mnaitumikia katiba ya CCM pia, kama mngekuwa wabunge wa vyama vya upinzani sina tatizo na hilo lakini sio nyie watu wa CCM ambao hata chama chenu kinaamini hivyo juu ya muundo wa muungano" sasa mkuu unaposema hata katika mfumo wa vyma vingi eti Nyerere alikataa watu wasijadiri muungano hiyo sio kweli, huo ni uongo na kama unaweza kutetea kitu hata kudanganya ndipo ninapodhani kuwa huenda una ajenda nyingine ya siri, halafu eti nasikia wewe huishi Zanzibar wala huku Tanganyika, hivi ni kweli?
katika hadidu rejea za tume ya mabadiliko ya katiba haziruhusu kutoa maoni ya kuvunja muungano that's y tunatoa maoni ya muungano wa mkataba ambao unakaribia kuwa sawa na kuvunja.