AHMED RAJAB: Je, Sheikh Abeid Karume naye akitaka kurejesha usultani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

AHMED RAJAB: Je, Sheikh Abeid Karume naye akitaka kurejesha usultani?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Sep 6, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Sep 6, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145

  BARAZANI KWA AHMED RAJAB

  Toleo la 257 5 Sep 2012

  MOJA ya mambo yenye kushangaza katika mjadala unaoendelea Zanzibar kuhusu Muungano wa Tanzania ni ile dhana ya kwamba upinzani dhidi ya muundo wa sasa wa Muungano ulianza jana au kwamba umekuwa ukichochewa na mtu fulani au kikundi fulani chenye ‘ajenda ya siri.'

  Ukweli wa mambo ni kwamba Muungano uliasisiwa katika mazingira ya kutatanisha na hivyo tangu siku ya mwanzo ya kuzaliwa kwake ni wachache Zanzibar waliousherehekea kwa moyo mkunjufu. Wengi walikuwa na dukuduku na waliingiwa na wahasha lakini hawakuwa na la kufanya.


  Wajumbe kadhaa wa Baraza la Mapinduzi la awali wameniambia kwamba lau suala hilo lingejadiliwa kwa uwazi katika Baraza hilo na lau wajumbe wa Baraza wangepewa fursa ya kuamua basi wangeliupinga muundo huo wa Muungano.

  Hawasemi kwamba wangelipinga kuwapo kwa aina ya umoja au shirikisho baina ya Tanganyika na Zanzibar, lakini wangepinga muundo ulioibuka wa Muungano wa nchi hizo mbili. Tukumbuke kwamba wakati huo Baraza la Mapinduzi ndilo lililokuwa na majukumu ya utungaji wa sheria za Jamhuri ya Watu wa Zanzibar.

  Wenye kuhoji (bila ya kutoa hoja madhubuti) kwamba wenye kuupinga muundo wa Muungano wana ajenda ya siri ya kurejesha usultani wanajikanganya na kujisuta wenyewe.

  Sijui Sheikh Abeid Karume, mmoja wa waasisi wa Muungano huu, alikuwa na ajenda gani ya siri alipokuwa akiupiga vijembe Muungano katika siku za mwisho za uhai wake. Wakati huo alikuwa amekwishatanabahi kwamba muundo wa Muungano kama ulivyo haukuwa na manufaa kwa nchi yake. Ndiyo maana akatamka kwamba ‘Muungano ni kama koti likikubana unalivua'.

  Wakati mwingine siku moja tu kabla hajaiaga dunia alimwambia Bwana Salim Rashid, katibu mkuu wa kwanza wa Baraza la Mapinduzi, kwamba Muungano ni kama matoto ya treni na Zanzibar inashikilia shoka ambalo karibu italitumia kuukata mnyororo unaoyaunganisha hayo matoto na ukikatika kila toto litakwenda upande wake. Kwa hayo alikuwa na maana kwamba Tanganyika ingekwenda upande wake na Zanzibar ingekwenda upande wake.


  Wala sijui kina Kanali Seif Bakari na wenzake na tepu zao za ‘Kiroboto' zilizokuwa zikitangazwa Redio Zanzibar walikuwa na ajenda gani na ya kumrejesha sultani gani Zanzibar.

  Ninachojaribu kukumbusha ni kwamba upinzani dhidi ya muundo wa Muungano haukuanza jana wala leo. Lililo muhimu zaidi ni kutambua kwa kujikumbusha kwamba upinzani huo ulijikita pia ndani ya duru za waliokuwa wakihodhi madaraka Visiwani Zanzibar baada ya Mapinduzi ya mwaka 1964.

  Viongozi hao wa Mapinduzi walikuwa na imani thabiti na ile sera ya kutaka kuleta umoja barani Afrika lakini kwa namna mambo yalivyokuwa yakienda baada ya kuundwa Muungano walianza kuukosoa muundo wa Muungano huo.

  Mara kadha wa kadha katika uhai wake wa miaka 48 Muungano wetu umekuwa ukikabiliwa na mikwaruzano ya aina kwa aina.
  Kwa mfano, kuna kile kisa kilichosababisha Sheikh Aboud Jumbe kupokonywa wadhifa wake wa kuwa Rais wa Zanzibar mnamo mwaka 1984 alipojaribu kuirejeshea Zanzibar mamlaka yake kamili ya utawala. Aling'olewa madarakani kwa nazaa na Chama cha Mapinduzi (CCM) na wala si na Baraza la Mapinduzi kama ilivyotakiwa na Katiba ya Zanzibar.

  Ni muhimu tuwe tunakumbuka kuwa Wazanzibari hawakuanza kudai mabadiliko ya muundo wa Muungano baada ya kuanza mchakato wa sasa wa kulitafutia taifa Katiba mpya lakini walianza kunung'unika tangu miaka ya 1960 walipogutuka na kuona kwamba muundo wa Muungano hauwapi fursa waitakayo ya kujiamulia mambo yao na kuyatetea maslahi yao.

  Ndiyo maana kila walipopata fursa ya kutoa maoni yao juu ya Muungano, kama kwa mfano, wakati wa Tume za Nyalali na Kisanga Wazanzibari wengi walipendelea pawepo na mfumo wa serikali tatu katika Muungano.Waliamini kwamba mfumo huo ungeirejeshea Zanzibar mamlaka yake yaliohamishiwa Bara.
  Tusisahau pia kwamba si zamani sana ilikuwa ni kosa, tena la uhaini, kwa Mtanzania ‘kuujadili' Muungano kadamnasi, seuze kupendekeza mageuzi katika muundo wake au kupendekeza kwamba uvunjwe kabisa.

  Juu ya kuwako vipingamizi hivyo Wazanzibari wameendelea kuwa wavumilivu lakini hawakusita kuyakosoa yale mambo yenye kuyadhuru maslahi yao ya kitaifa.

  Wale wenye kufikiri kwamba msimamo wa Wazanzibari juu ya Muungano ni wa karibuni pamoja na kampeni inayopigwa Visiwani ya kutaka mageuzi ya kimsingi kuhusu Muungano hawaiangalii historia ipasavyo.
  Wangeitalii historia ipasavyo wangeona kwamba hata katika vikao mbalimbali vya Baraza la Wawakilishi tokea miaka ya 1980 suala la Muungano lilikuwa likiibuka mara kwa mara na kwamba Baraza hilo kila lilipopata fursa lilikata maamuzi yenye kutetea maslahi ya Zanzibar. Mifano ya hivi karibuni ni pamoja na yale maamuzi yanayohusika na masuala ya mafuta na gesi asilia.

  Tumeshuhudia pia kwamba kila siku zikisonga mbele Baraza la Wawakilishi limekuwa likizidi kupaza sauti yake kuhusu msimamo wake juu ya Muungano. Limekuwa likifanya hivyo hata kabla ya mchakato wa sasa wa Katiba kuanza.

  Hivyo ni kosa na upotoshaji wa hali ilivyo kudai kwamba ni jumuiya, chama au mtu fulani mwenye kuwachochea au kuwahamasisha Wazanzibari wawe na msimamo fulani juu ya Muungano.
  Tuseme tu kuwa mazingira ya sasa yanawawezesha Wazanzibari kutoa maoni yao kwa uwazi zaidi bila ya kuingiwa na hofu. Hii leo sheria haitomtia nguvuni mtu anayetoa maoni ya kutaka muundo wa Muungano ubadilishwe au hata anayetaka Muungano wenyewe uvunjwe.
  Hofu hiyo ilikuwapo zamani hata pale uliporejeshwa tena mfumo wa vyama vingi vya kisiasa kwani Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alisema kwamba vyama vipya vya kisiasa vinaweza kujadili masuala yote lakini visiuguse Muungano.

  Hivyo, wengi walitishika kuukosoa Muungano wakiamini kwamba ilikuwa ni uhaini kufanya hivyo kutokana na maneno ya Mwalimu.

  Si ajabu kuwaona Wazanzibari wakiwa na hofu hiyo kwani kwa jumla Watanzania wote waliteseka chini ya mfumo wa chama kimoja cha kisiasa kuanzia mwaka 1964 hadi 1992.
  Kadhalika, kwa muda wa miaka 28 kati ya 48 ya Muungano, CCM ikiwa na makao yake makuu mjini Dodoma, ndiyo iliyokuwa ikishika mpini kuhusu masuala ya Muungano kama vile kwa mfano wakati wa kutungwa Katiba ya Muungano mwaka 1977.
  Sasa hali ya mambo imebadilika na ndiyo maana wakati wa kutoa maoni yao mbele ya Tume ya Warioba kuna Wazanzibari wanaosema kuwa wanataka pawepo Muungano wa Tanganyika na Zanzibar utaojengeka juu ya msingi wa Mkataba na si Katiba.

  Katika Muungano wa aina hiyo kila nchi itakuwa na mamlaka kamili ya utawala wa mambo ya ndani ya nchi yake pamoja na shughuli za kigeni au za kimataifa. Mfumo huo ni bora zaidi kushinda ule wa serikali tatu ambao wengi wanauona kuwa umepitwa na wakati na uliokwishakataliwa na Serikali za Jamhuri ya Muungano ya Tanzania.

  Kadhalika, kuna uwezekano mkubwa kwamba muundo wa aina hiyo utaweza kuzivutia nchi nyingine katika kanda ya Afrika ya Mashariki na ya Kati kujiunga na Muungano wetu na hivyo kuimarisha kidhati Umoja wa Kiafrika.

  Hapana shaka yoyote kwamba Muungano wa aina hiyo utakuwa imara na wa maana zaidi kinyume na huu wa sasa ulioselelea kuwa wa nchi mbili tu takriban nusu karne baada ya kuasisiwa na usiokwisha kukumbwa na mikwaruzano na kero za kila aina.

  Kwa hakika historia ya Muungano itapoandikwa kwa dhati na bila ya upendeleo itaonyesha kwamba Zanzibar daima imekuwa na dukukudu kuhusu nafasi yake ndani ya huu Muungano baina yake na Tanganyika. Historia hiyo itaonyesha pia kwamba kuna Wazanzibari wenye kuamini kwamba wameonewa katika mahusiano kati ya nchi yao na Tanganyika.

  Ili kuondosha chokochoko zilizopo na kuondosha ukinzani uliopo kati ya pande mbili za Muungano kuna haja ya kuwa na muundo wa Muungano utaoziridhisha pande zote mbili na utaoweza kuzifuta kabisa na kwa njia za amani na udugu tofauti zilizopo kati yao kwa manufaa ya Watanganyika na ya Wazanzibari.

  Kama kweli tunataka bara la Afrika liungane kiuchumi, kisiasa na kijamii basi kuna ulazima kwamba misingi ya umoja huo iwe madhubuti na iziwezeshe nchi zinazoungana ziungane kila moja ikiwa na mamlaka kamili ya kujiamulia mambo yenye kuhusika na maslahi yake.
  Muungano aina hiyo utafana endapo tu utakuwa ni wa hiyari na si wa kulazimishwa na ikiwa utaipa kila nchi iliyomo ndani yake haki ya kuwa na kauli sawa na uhuru wa kujiamulia yaliyo yake bila ya kuyadhuru maslahi ya nchi nyingine zilizo ndani ya Muungano huo.   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Sep 6, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Wewe Mwandishi Unaonaje? Ungependa USULTANI URUDI ZANZIBAR?
   
 3. J

  JokaKuu Platinum Member

  #3
  Sep 6, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,747
  Likes Received: 4,967
  Trophy Points: 280
  ..sasa Ahmed Rajab alikuwa akimcheka nini Prof.Issa Shivji?

  ..hivi kweli makala zake[ahmed rajab] za karibuni haziendi kinyume na maandiko yake ya muda mrefu??

  ..sisi wengine tumezoea makala za Ahmed Rajab zilizojaa uzushi, chuki, na ubaguzi, dhidi ya wa-Tanganyika.

  ..Ahmed Rajab anapoandika makala kama hii, tena kwa lugha ya uungwana, huku akichombeza kuhusu muungano wa mkataba, inabidi tujiulize kulikoni?!

  ..kama Mtanganyika nasema, LET ZANZIBAR GO. wa-ZNZ hawajui wanataka nini. watu wa namna hiyo haiwezekani wakaridhika na muungano wa aina yoyote ile.
   
 4. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #4
  Sep 6, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Kwa kweli nimeshachoshwa na makala kama hizi ambazo hazina tija. Let them go.
   
 5. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #5
  Sep 7, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,355
  Trophy Points: 280
  wasomi wengi sana zanzibar wamekuwa hopeless kabisa.Watu wamewaamini na kuwapenda .Wanajua pangilia maneno ila hawajui pangilia theme, na wala hawajui umuhimu wa kuwa consistent katika ideas.Kwani ndipo zinampta mtu utambulisho na misimamo yake.

  Halafu huwa kinga yao kwa watu wao ni kujiweka kuwa ni waliobobea, halafu wanajifanya dangaanya wenzao kuhusu bara, wanadanganya watu wao kuwa bara hawana Ilm ya Zanzibar.Baada ya hapo ndi[o wanaanza ndika mambo ajambo yao,bila kujikumbusha misimamo yao, na ujumbe waupelekao.

  Nilikuwa nikicheka kila nimsikiapo prof Haroub Othman akiongea BBC masuala yahusuyo mashariki ya kati na nchi za Kimagharibi.Muda wote walikuwa kama vibaraka wa ukomunisty, na siasa za akina Ghaddafi,unajiuliza hawa ndiow aliosomea hela za walipa kodi?Hawa ndio waliopewa vipaumbela katik kuendelea na alimu ya juu na kuwaacha wenzao mitaani?Hawa ndio sasa hivi wanakuwa vibarua na wadhaifu kuliko wale waliowaacha mitaani?Nakosa majibu kabisa.

  Hawa waandishi wana vitabu kama vijarida vya udaku.Kuna machanganyiko wa dini, siasa , philosophy, na ujinga walioweka mizizi, historia ya uhuru na muungano, pamoja na MOU, na mijadala ya kuhsu sultani kurudi au lah.Hap ndipo akili zaozlipoishia na mwandishi wahizo habari akipindisha historia na kunadika chochote cha uahsama ndipo anazidi onekana na wenzie kuwa ni mwandishi mashuhuri.
   
 6. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #6
  Sep 7, 2012
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,221
  Likes Received: 7,342
  Trophy Points: 280
  Mkuu, huyu jamaa ni member JF. Ukisoma makala hii anajaribu kujibu tuhuma zilizotolewa zikihoji ushiriki wake katika kuwadanganya wazanzibar akishirikiana na maalimu Seif.

  Mara ya pili amekana serikali 3 baada ya kupashwa kuwa Tanganyika ikirudi kila mtu na lake.
  Sasa ameshupalia mkataba.

  Ni mwandishi wa kiwango cha chini sana. Kawatia wenzake mkenge wa nyimbo ya tatu,tatu halafu kawarudi.
  Anawaimbisha tena mkataba, mkataba.

  Mambo magumu hawana pa kushika, kuondoka hawataki wanataka kubaki mguu nje mguu ndani.
  Subiri tume ziingie Mijini na kwenye majiji wataambiwa wazi

  LET ZNZ GO!
   
 7. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #7
  Sep 7, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,361
  Likes Received: 6,380
  Trophy Points: 280
  This is just silly! Kama Muungano wa Kimkataba unatoa mamlaka kamili kwa nchi (iliyomo kwenye muungano huo) kujiamulia mambo yake ya ndani na ya nje - MUUNGANO WANAUTAKA WA NINI SASA? AU WATAUNGANA KATIKA VITU GANI AMBAVYO HAVIWEZI KUWA VYA NDANI AU NJE YA NCHI HUSIKA? Njia rahisi ni kwa Zanzibar kujiondoa tu kwenye Muungano haiitaji kuungana na Tanganyika.
   
 8. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #8
  Sep 7, 2012
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,221
  Likes Received: 7,342
  Trophy Points: 280
  Mwanakijiji, Ukisoma habari nzima utashangaa sana. Wanataka kila nchi iwe na maamuzi yake na iwe huru, wakti huo huo wanataka mkataba! jamani hawa wenzetu ?!!!!!

  Ukisoma anasema muungano ni kama koti lilkikubana unalivua, sasa badala ya kulivua wanataka walivue lakini wampe Mtanganyika kazi ya kulibeba. Vua koti weka chini nenda zako.

  Ahmed ameshtuka baada ya kusikia kuwa Tanganyika ikirudi sheria za Tanganyika zitatumika na hakuna uchochoro wa muungano. Ameshtuka baada ya watu kuhoji, hivi serikali 3 alizokuwa anapigia debe ziweje? na ZNZ itachangia nini?

  In fact makala yake ililenga kujibu zile makala za washirazi na wamatumbi tulizokuwa tunazijadili.
  Kujibu kati ya mapinduzi daima na sultani oyee
  Kujibu kuwa Ahmed Rajab, Jusa, Maalimu Seif, Raza na wenye asili hiyo wanamtaka sultani.

  Ukweli niujuao mimi Waunguja wengi wameshtukia janja hii na wao wanahoji kuhusu ushirazi na hasa waarabu kulivalia njuga jambo hili.

  Tanganyika tunasema mkataba wa nini? Si kila mtu aamue hatima yake.
  Ahmed hana jibu mkataba uhusu nini, anadhani atatuimbisha nyimbo za mkataba kama Wazanzibar.
  Member huyu wa JF tunamwambia wazi, mkataba wa nini kama huwezi kuutetea rudi unguja ukawafundishe kuimba nyimbo wasizojua maana yake sisi tunasema LET ZNZ GO!

  Ahmed Rajabu kaimbishe nyimbo za mchakamchaka Zanzibar, ukija Tanganyika uje na majibu mktaba wa mambo gani?
   
 9. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #9
  Sep 7, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,361
  Likes Received: 6,380
  Trophy Points: 280
  Halafu hivi haya maneno ya Karume ambayo yananukuliwa sana yalisemwa wapi na alikuwa anazungumzia nini? Maana huwa yanarudiwa kuwa Karume alisema alisema na watu tunakubali ni kweli alisema... maana mara zote yanatolewa hayo tu sijui kilichosemwa kabla ilikuwa nini na kilichosemwa baada kilikuwa nini
   
 10. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #10
  Sep 7, 2012
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Nicholas, Mwanakijiji, Nguruvi3 , jokakuu na Jasusi.

  Siku zote kwa mtu makini na msomi mwenye kuelimika anajibu hoja kwa kutoa hoja. Kwa maana kuwa kunakuwa na ushindanishaji wa hoja kwa hoja na sio dharau wala kejeli.

  Msomi yoyote aliyeelimika anapoanza kutoa lugha za mkato na kejeli pasi na kujikita kutoa hoja basi huyo anaitwa MUF'LIS kwa maana amefirisika sio tu kiakili bali hata kimawazo.

  Sasa ushauri wangu kwenu wote jaribuni kwa kadri ya uwezo wenu kujibu hoja zake ambazo kwangu mimi naziona ni madh'buti sana na amezipangilia kwa mpangirio na mtiririko mzuri sana na hazina hata chembe ya shaka ndanimwe.

  Alichobainisha Ahmed Rajab ni uhalisia na ukweli mtupu. Na kama kwa waandishi mahiri na waliobobea kama Ahali yangu Ahmed (nimezoea kumuita Tuyuri wa kingazija) ametoa suluhisho lake ambalo nyie wote ndio mnapingana nalo kwa maneno ya kejeli.

  Sasa kwa kuwadarsisha kidogo. Mtu makini anatakiwa kusoma hoja zote za mwandishi nutufa kwa nutufa na kuelewa na kujua ametumia mtindo gani katika kujenga hoja zake. Hapo kwenye suluhisho ni sehemu ya mwisho sana katika kufikia tamati.

  Kumbukeni kuwa kila mwenye kupinga Muungano wenu basi anasababu zake za msingi zinazomfikisha hapo na vile vile kila mwenye kuutetea muungano basi ana sababu zake za kumfikisha katika maamuzi hayo. lakin ikumbukwe kuna wale wasio na hoja ambao siku zote ni bandera kufuata upepo na wamekuwa washabiki pasi na kuwa na hoja kama mlivyo nyie.

  Nawashauri kwa mara nyingine jikiteni katika kujenga hoja ili kuungana/ kupingana na hoja za mwandishi. Kwani muungano wenu ni wa nchi mbili huru na kila upande una fursa sawa ya kuujenga/ kuuvunja. sasa msiwe mwanyonge kiasi cha kusema basi wao wajitoe kwani nasi tumewachoka. Kumbukeni hata nyie mnayo nafasi ya kuwafurusha kama mumewachoka.na sio kubakia kusema LET THEM GO

  Fungukeni kiakili na acheni woga. Kwani siku zote ukweli udumu daima
   
 11. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #11
  Sep 7, 2012
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,221
  Likes Received: 7,342
  Trophy Points: 280
  Aaa MM bwana, amesema hayo bwana huamini nini? Tena mengine Ahmed Rajab amenukuu dakika chache kabla ya kuuawa, soma hapo juu kwenye makala.

  Karume kauawa 1972 juzi juzi tu tunashindwaje kusikia maneno yake na tulikuwa na redio na TV ya rangi ya kwanza Afrika!

  Acha mchezo bwana, ZNZ ilikuwa nzuri sana wakati wa sultani, watu walikuwa na minyororo shingoni na walikuwa wanapata kila kitu na raha tupu seuse maneno ya juzi juzi. Kasema Karume tumemsikia maskani kizimkazi na doledumbwi !
  Hebu tuache tuimbe nyimbo zetu za mkataaaba,unakuja! mkataaba unakuja!
   
 12. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #12
  Sep 7, 2012
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,221
  Likes Received: 7,342
  Trophy Points: 280
  Ahali yangu Baru baru,
  Nakuhakikishia kuwa makala ya Ahmed ina udhaifu wa hali ya juu sana. Nitainukuu kifungu kimoja baada ya kingine kama alivyoileta na mwisho utagundua kuwa hakuna usomi ni kuhangaika na kutapa tapa.
  Nitarejea
   
 13. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #13
  Sep 7, 2012
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Nitashukuru sana na nakushauri kama utaweza ipeleke kwenye gazeti husika ili nayo itoke kuwapa fursa wengi wasio nafasika kupitia forum hii waisome gazetini.

  Kila la kheir na L'jumaa kareem
   
 14. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #14
  Sep 7, 2012
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 9,002
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  hii ni sawa na mke mwenye kiburi anayeomba talaka ili hali hajui ataishi vp.
  hivi hawa jamaa zetu wamehesabiwa sensa kweli?
   
 15. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #15
  Sep 7, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145

  Jaribu kuniambia ni nchi zipi zenye Muungano wa kimkataba?
   
 16. m

  mliberali JF-Expert Member

  #16
  Sep 7, 2012
  Joined: Jul 13, 2012
  Messages: 2,879
  Likes Received: 1,514
  Trophy Points: 280
  huyu jamaa anajiita mwandishi mahiri . mbona hamna kitu ni hewa tu. anachoongea hapo juu hakijui. kuna vitu muhimu vinavyo fanya muungano wa nchi au (states)kama USA, UK. kuwa SOVEREIGN STATE.bila kujali muundo wa serikali, ukiviondoa vitu hivyo kama vitu. huyu mwandishi **** anavyodai, hakuna sovereign state. logically kama hakuna sovereignity hakuna muungano wowote hiyo itakuwa ni kama regional intergrations, international communities, SADCC,ECOWAS nk

  hapa tunazungumzia muungano wa kujenga nchi a "SOVEREIGN STATE". tunawezaje kujenga nchi moja kubwa na imara lakini yenye serikali ndani yake kwa ku overcome internal political differences hiyo ndo point

  contrary to that ni kuvunja nchi tu. na tujadili vilevile consequences za kuvunja nchi. twaweza kudhani ni kitu kidogo sana ila tutakuja kujuta baadaye

  suluhisho ni either selikali tatu au moja na

  kwa serikali tatu twaweza kuwa na mabunge matatu. bunge dogo la zanzibar, bunge dogo la bara na bunge kuu la muungano(senete)

  tujadili kwa nia ya kupata suluhisho la muungano siyo kuvunja kama huyu mwandishi **** anavyotaka eti "muungano wa mkataba" kwani huu uliopo ni wa nini???,sasa kama tukivunja muungano huu itakuwa haina maana ya kuingia kwenye miungano mingine
   
 17. takashi

  takashi JF-Expert Member

  #17
  Sep 7, 2012
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 909
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Sasa unakereka kutumia (kunukuu) maneno ya Karume? Hivi si wewe na kundi lako ,kila siku mnaimba nyimbo hapa za kumuabudu yule aliyekuwa dikteta wa kwanza tz?
   
 18. takashi

  takashi JF-Expert Member

  #18
  Sep 7, 2012
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 909
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Sasa kama huyu jamaa atakua sio mwandishi mahiri, huyu MM kijiji atakua nani? Kila siku hapa anatuletea porojo Baba wa taifa , blah blah nyingi. Hamna lolote brain washed people.
   
 19. J

  JokaKuu Platinum Member

  #19
  Sep 7, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,747
  Likes Received: 4,967
  Trophy Points: 280
  Barubaru,

  ..nakumbuka ktk moja ya post zako hapa JF uliandika kwamba Tanganyika na Zanzibar zimeungana "kimkataba" na siyo "kikatiba."

  ..sasa anapoibuka Mzanzibari mwenzako na kupendekeza "muungano wa mkataba" huoni kwamba analeta ubabaishaji??

  ..mimi nadhani wakati umefika kwa wa-Zanzibari wawe wazi ktk kile wanachokitaka, na pia kile wasichokitaka.

  ..ingependeza kama mngeweza kutueleza ktk huo mkataba mpya kati ya Tanganyika na Zanzibar mnataka mambo gani yawepo humo.
   
 20. M

  Mazindu Msambule JF-Expert Member

  #20
  Sep 7, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 4,320
  Likes Received: 1,496
  Trophy Points: 280
  Bwana Ahmed Rajab, kwanini usipendekezee tu kuvunjwa muungano? mkataba wa nini tena, tusije koseana kwenye vipengere vya huo mkataba then tukaanza kupelekana mahakani tena, mi nafikiri kama unayo hoja juu ya muungano, washawishi tu wazanzibar wenzio muuvunje tu huu muungano na kila moja awe na chake, simple as that, kumsingizia JK Nyerere kwamba hata katika vyama vingi alikataa muungano usijadiriwe hiyo ni uongo, kwa muislam kama wewe kuongea uongo ni jambo baya sana, nadhani utakapo kwenda kupiga Rakaa leo kumbuka kumwomba msamaha muumba wako kwamba umemsingizia mtu, nakumbuka vizuri sana tena hata hotuba za mwalim bado ninazo, alilikemea kundi lile la G 55 juu ya hoja yao ya muungano, point yake ilikuwa hivi, "nyie ni wabunge wa CCM, mnaitumikia katiba ya CCM pia, kama mngekuwa wabunge wa vyama vya upinzani sina tatizo na hilo lakini sio nyie watu wa CCM ambao hata chama chenu kinaamini hivyo juu ya muundo wa muungano" sasa mkuu unaposema hata katika mfumo wa vyma vingi eti Nyerere alikataa watu wasijadiri muungano hiyo sio kweli, huo ni uongo na kama unaweza kutetea kitu hata kudanganya ndipo ninapodhani kuwa huenda una ajenda nyingine ya siri, halafu eti nasikia wewe huishi Zanzibar wala huku Tanganyika, hivi ni kweli?
   
Loading...