Ahmed Adam – Mnubi aliyemkirimu na kumlaza Mwalimu Julius Nyerere nyumbani kwake Mikindani 1955

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,788
30,084
AHMED ADAM – MNUBI ALIYEMKIRIMU NA KUMLAZA MWALIMU JULIUS NYERERE NYUMBANI KWAKE MIKINDANI 1955

1571243041746.png

Tukio dogo la kiburi cha askari mpumbavu wa mkoloni ndiko kulisababisha watu wa Mikindani wafungue tawi la TANU.

Askari mmoja mpita njia aliingia katika ubishi na kijana mmoja wa pale mjini, akiitwa Hassan Masudi Vuni.

Akitumia mamlaka yake ya kukamata mhalifu, askari huyo alimpiga Vuni kwa kumuonea.

Miongoni mwa watazamaji wa tukio hilo alikuwa Rashid Ali. Rashid Ali alikwenda kusimulia tukio hili kwa Mohamed Ali Abdallah.

Alipokuwa akisimulia mkasa ule, pamoja naye alikuwa Suleiman Hassan Msepele.

Walipokuwa wakijadiliana Msepele alitamka kwamba tukio kama hilo kamwe lisingeweza kutokea Dar es Salaam kwa sababu Mwafrika mmoja jina lake Julius Nyerere alikuwa ameanzisha chama cha siasa kupigania uhuru wa Tanganyika.

Rashid Ali na Mohamed Ali Abdallah walitamani kujua mengi zaidi kuhusu Mwafrika huyu aliyekuwa akijulikana kwa jina la Nyerere na chama chake cha siasa, lakini Msepele hakuwa na mengi ya kueleza kuhusu Nyerere na hicho chama chake. Kwa hiyo basi, hawa watu watatu waliamua kumtuma mtu Dar es Salaam kupata habari zaidi kuhusu chama hicho.

Mohamed Ali aliandika barua na kumpa Msham Awadh na Ali Muhidin kumpelekea Nyerere Dar es Salaam.

Ndani ya barua hiyo Mohamed Ali alimweleza Nyerere kwamba ukoloni ulikuwa bughudha kubwa katika Jimbo la Kusini, na wangependa kufungua tawi la TANU mjini Mikindani ili kupigania uhuru.

Mwaka 1955 Mohamed Ali alikuwa na umri wa miaka 45.

Alikuwa hana elimu kama elimu inavyojulikana kwa kuwa hakusoma shule yoyote. Alipokuwa kijana mdogo baba yake alimpeleka Zanzibar kusoma elimu ya dini.

Wakati huo Zanzibar ilikuwa ndiyo kitovu cha elimu ya Kiislamu Afrika ya Mashariki na nchi jirani.

Huko Zanzibar kijana Mohamed Ali alisoma kwa Sheikh Mohamed L’Khamus. Kisha aliendelea na masomo yake mjini Dar es Salaam kwa Sheikh Wazir bin Said, mwanafunzi wa Sheikh maarufu sana na aliyekuwa Khalifa wa Tariqa ya Askariyya, Sheikh Idrissa bin Saad. Baada ya kumaliza masomo yake mjini Dar es Salaam alisafiri hadi Belgian Congo na halafu alirudi Ujiji nchini Tanganyika kufanya biashara ndogo ndogo.

Mwaka 1947 Mohamed Ali alirudi Lindi na kutoka hapo alikwenda Mikindani na kuwa fundi cherahani.

Msham Awadh alikuwa akijulikana Lindi nzima na Mikindani kwa sababu ya biashara yake. Mshama Awadh alikuwa alikuwa muuza uzuri, yaani vitu vya urembo kama vile uturi, dalia, marashi, rangi na manukato mengine kwa wanawake wa hii miji miwili.

Alikuwa akiuza bidhaa zake kikapuni akipita nyumba hadi nyumba. Hawa walikuwa ndiyo aina ya watu walioanzisha na kuongoza harakati za kumaliza utawala wa kikoloni.

Hawakuwa wajuzi wa lugha ya Kiingereza wala hawakuwa na ujuzi wa maisha ya ulimwengu wa Kimagharibi kama walivyokuwa baadhi ya Waafrika wengine waliyopata elimu ya Kimagharibi.

Msham Awadh na Ali Muhidin walikwenda hadi Dar es Salaam kukutana na Mwalimu Nyerere, John Rupia, Said Chamwenye, Oscar Kambona na Dossa Aziz katika makao makuu ya TANU, New Street.

Msham Awadh na Ali Muhidin walipewa kadi za TANU na wakaambiwa wafungue tawi Mikindani.

Wakati Msham Awadh na Ali Muhidin wakiwa njiani kwenda Dar es Salaam kukutana na Nyerere, Mohamed Ali alisafiri kwenda Lindi kukutana na Suleiman Masudi Mnonji mmoja wa viongozi wa TANU hapo mjini na kumweleza kuwa Mikindani walikuwa wamekusudia kufungua tawi la TANU.

Mnonji alimpa kadi Mohamed Ali na akawa mwanachama na akamwambia arudi Mikindani na kuanza kufanya kampeni kwa nguvu kwa ajili ya TANU na awafahamishe watu kuwa Nyerere yupo njiani kuja Jimbo la Kusini.

TANU Lindi walikuwa wamemualika Julius Nyerere kuja Lindi na katika ratiba yake alipangiwa kufika Mikindani. Nyerere, Ali Mwinyi Tambwe na Rajabu Diwani waliwasili Mikindani kutoka Lindi siku ya Jumamosi. Kabla ya kuwasili ujumbe huo, kazi kubwa kuliko zote waliyokuwanayo uongozi wa TANU Mikindani ilikuwa kutafuta mahali pa kumlaza Nyerere.

Walimwendea Ahmed Adam, Mnubi mmoja tajiri na mtu wa makamo, aliyemiliki nyumba moja ya fahari.

Nyumba hii ilikuwa ya ghorofa moja na ilijengwa kwa mawe na chokaa.

Ahmed Adam aliombwa awe mwenyeji wa Nyerere na ujumbe wake.

Nyumba hii tayari lilikuwa na kisa chake. Ilijengwa na hayati kaka yake Ahmed Adam baada ya Vita Kuu ya Kwanza.

Kaka yake alikuwa askari wa Kinubi aliyekuwa katika jeshi la Wajerumani.

Huenda alichukuliwa Misri mwishoni mwa mwa karne ya kumi na tisa na Wajerumani kuja Tanganyika kama mamluki katika jeshi la Wajerumani chini ya Kamanda Herman von Wissman.

Baada ya vita alilipwa kiinua mgongo na serikali ya Ujerumani na kwa kutumia fedha hizo alijenga nyumba hiyo.

Katika Vita Kuu ya Kwanza yeye alipigana katika jeshi la Wajerumani dhidi ya Waingereza chini ya Paul von Lettow Vorbeck.

Baada ya vita Wajerumani wakiwa wameshindwa vita, Waingereza waliitikadi nyumba hiyo kama mali ya adui wa himaya ya Kiingereza na kwa hiyo ilibidi itaifishwe.

Hii ilikuwa ndiyo nyumba pekee iliyokuwa nzuri yenye kumilikiwa na Mwafrika na kwa ajili hii haikuweza kukosa kuhusudika.

Utawala wa Waingereza ulikuwa katika taratibu ya kuitaifisha nyumba hiyo wakati ilipofahamika kwamba serikali isingeweza kufanya hivyo kwa sababu ya kifungu cha sheria ambacho kilisema kuwa mali ya Waafrika waliokuwa wakitumika katika majeshi ya watawala wao haiwezi kutaifishwa.

Hii ilinusuru nyumba hiyo na hivyo ilibakia mikononi mwa mwenyewe mpaka alipofariki na nyumba hiyo ikaja kuwa katika miliki ya mdogo wake, Ahmed Adam. Ahmed Adam alikubali kumpokea Nyerere na ugeni wake nyumbani kwake.

Nyumba hiyo ilikuja kuwa tawi la kwanza la TANU Mikindani.

Siku hiyo hiyo ya Jumamosi, usiku Nyerere aliitisha mkutano wa ndani wa wanachama wa TANU na wanachama kama 30 hivi walihudhuria.

Nyerere aliwaeleza kwa ufupi juu ya ile safari yake ya Umoja wa Mataifa na hali ya siasa kwa ujumla kama ilivyo mjini Dar es Salaam.

Nyerere aliwahakikishia wasikilizaji wake kuwa kulikuwa na uwezekano mkubwa sana kuwa Tanganyika itakuwa huru katika uhai wao.

Siku iliyofuatia mkutano wa hadhara ulifanyika mjini Mikindani mahali palipojulikana kama Jangwani, karibu na ufuko wa Bahari ya Hindi.

Mkutano huu uliohudhuriwa na watu wengi na uliendelea bila mushkeli wowote ukitoa kitendo kidogo kilichofanywa na mwalimu mmoja wa shule, Abdulrahman Muhibu aliyekuwa amelewa.

Muhibu alikuwa ametoka kunywa pombe na alipita karibu na uwanja wa mkutano ambapo Nyerere alikuwa akihutubia. Katika hali yake ya ulevi alimpigia kelele Nyerere akamwita muongo.

Huenda Muhibu alikuwa akifahamu vyema ujumbe wa Nyerere, na akiwa vile alivyokuwa, mtumishi wa serikali na mlevi, aliona wazo la mwalimu wa shule Mwafrika kama yeye kuwaongoza watu hadi uhuru upatikane ni jambo lisilowezekana.

Kwa haraka Muhibu alikamatwa na watu na ilikuwa karibu wamtie adabu ndipo Nyerere alipoingilia na hivyo kumnusuru.

Jioni hiyo baada ya mkutano Nyerere na ujumbe wake waliondoka kwenda Newala, kwenye ngome ya Yustino Mponda. Mponda alikuwa mmoja wa wajumbe wa Baraza la Kutunga Sheria waliosafirishwa na Gavana Edward Twining hadi Umoja wa Mataifa, New York, kumpinga Nyerere.

Sasa TANU ilikuwa ikichukua mkokoto wake wa kampeni hadi ndani ya ardhi ya Mponda ambayo yeye alikuwa liwali na mjumbe wa Baraza la Kutunga Sheria.

Nyerere alipomaliza ziara yake ya Jimbo la Kusini, fikra za watu wengi zilibadilika.

Tatizo kubwa kusini mwa Tanganyika kuhusu TANU ilikuwa Kanisa likiwaonya waumini wake kuchukua tahadhari na TANU kwani kanisa likiona harakati zile za kudai uhuru zilikuwa sawa na harakati zilizosababisha Vita Vya Maji Maji na kusababisha majemedari 62 wa vita vile kama Abdulrauf Songea Mbano kunyongwa na kuzikwa katika kaburi la halaiki Songea.

Kuja kwa Nyerere Wakristo waliokuwa wakitishwa na Kanisa hawakuamini tena kuwa TANU ilikuwa harakati za Waislam sawasawa na Vita Vya Maji Maji.

Nyerere, Tambwe na Diwani walipokuwa wanashika njia kurudi Dar es Salaam, matawi ya TANU yalikuwa tayari yamefunguliwa Masasi, Ndanda na Newala ambazo zilikuwa sehemu za Ukristo na ngome kuu ya Kanisa Katoliki katika Tanganyika.
 
Attachments

  • KARUME AND ALI MWINYI TAMBWE.jpg
    KARUME AND ALI MWINYI TAMBWE.jpg
    4.4 KB · Views: 3

Shukran sana Mzee wangu Mohammed Said
 
Hilo ndio jengo picha (2) lililotolewa maelezo na muandishi Mr. Mohamed Said na hicho chumba cha juu ndicho alicholala Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Picha nyingine (3) zinaonesha Mji wa Kihistoria wa Mikindani ulioko kandokando kabisa ya Bahari ya Hindi. Picha hizi nilizipiga mwaka 2016 mwezi Desemba..
WhatsApp Image 2019-10-14 at 09.56.39.jpeg
WhatsApp Image 2019-10-14 at 09.57.04.jpeg
WhatsApp Image 2019-10-14 at 10.09.23.jpeg
WhatsApp Image 2019-10-14 at 10.10.06.jpeg
WhatsApp Image 2019-10-14 at 10.14.42.jpeg
 
Hilo ndio jengo picha (2) lililotolewa maelezo na muandishi Mr. Mohamed Said na hicho chumba cha juu ndicho alicholala Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Picha nyingine (3) zinaonesha Mji wa Kihistoria wa Mikindani ulioko kandokando kabisa ya Bahari ya Hindi. Picha hizi nilizipiga mwaka 2016 mwezi Desemba..View attachment 1233321View attachment 1233322View attachment 1233326View attachment 1233327View attachment 1233328
Ahmed,
Huwezi kuamini lakini jicho langu lilipoona picha ya kwanza nimepata mshtuko na neno lililotoka kwangu ni, ''Subhanallah,'' ametukuka Mwenyezi Mungu!

Ahsante sana kwa kunisadikisha kwa picha hizi kuwa nimesema kweli.
Alhamdulilah, sifa zote zinamstahiki Allah.

Nakushukuru sana ndugu yangu.
Picha nzuri sana.

Sasa naona majina haya yamefanana.
Naona hapo pana udugu wa nasaba.

Tafadhali tufahamishe sote tunaokusoma.
 
Ni kweli Mzee Ahmed Adam Ahmed ni babu yangu mzaa Baba yangu mzazi Adam Ahmed Adam (Mwenyezi Mungu awarehemu). Kuna mengi yamejificha hapa. Ilikuaje mpaka kufikia kusahaulika kwenye historia ya nchi hii?
 
Ndugu yangu Ahmed,
Katika maisha yangu ya utafiti wa historia hii nimepata mshtuko mkubwa mara mbili.
Mara ya kwanza siku nililetewa ''confidential report,'' kutoka Uingereza ikionyesha taarifa za mkutano wa Abdul Sykes na Kenyatta uliofanyika Nairobi mwaka wa 1950.

Abdul alikuwa Secretary wa TAA na alikuwa kijana wa miaka 26.

Mkutano huu nilikuwa nimeaundika katika kitabu cha Abdul Sykes lakini sikuwa na uthibitisho ila kauli ya Ahmed Rashad Ali aliyekuwapo siku Abdul Sykes alipokutana na Jomo Kenyatta.

Zaidi ya miaka 30 ilikuwa imepita ndipo nikapata huu uthibitisho.
Mara ya pili ni leo kutoka kwako.

Nitashukuru kama utanipatia picha ya babu yetu.
 
AHMED ADAM – MNUBI ALIYEMKIRIMU NA KUMLAZA MWALIMU JULIUS NYERERE NYUMBANI KWAKE MIKINDANI 1955

Tukio dogo la kiburi cha askari mpumbavu wa mkoloni ndiko kulisababisha watu wa Mikindani wafungue tawi la TANU.

Askari mmoja mpita njia aliingia katika ubishi na kijana mmoja wa pale mjini, akiitwa Hassan Masudi Vuni.

Akitumia mamlaka yake ya kukamata mhalifu, askari huyo alimpiga Vuni kwa kumuonea.

Miongoni mwa watazamaji wa tukio hilo alikuwa Rashid Ali. Rashid Ali alikwenda kusimulia tukio hili kwa Mohamed Ali Abdallah.

Alipokuwa akisimulia mkasa ule, pamoja naye alikuwa Suleiman Hassan Msepele.

Walipokuwa wakijadiliana Msepele alitamka kwamba tukio kama hilo kamwe lisingeweza kutokea Dar es Salaam kwa sababu Mwafrika mmoja jina lake Julius Nyerere alikuwa ameanzisha chama cha siasa kupigania uhuru wa Tanganyika.

Rashid Ali na Mohamed Ali Abdallah walitamani kujua mengi zaidi kuhusu Mwafrika huyu aliyekuwa akijulikana kwa jina la Nyerere na chama chake cha siasa, lakini Msepele hakuwa na mengi ya kueleza kuhusu Nyerere na hicho chama chake. Kwa hiyo basi, hawa watu watatu waliamua kumtuma mtu Dar es Salaam kupata habari zaidi kuhusu chama hicho.

Mohamed Ali aliandika barua na kumpa Msham Awadh na Ali Muhidin kumpelekea Nyerere Dar es Salaam.

Ndani ya barua hiyo Mohamed Ali alimweleza Nyerere kwamba ukoloni ulikuwa bughudha kubwa katika Jimbo la Kusini, na wangependa kufungua tawi la TANU mjini Mikindani ili kupigania uhuru.

Mwaka 1955 Mohamed Ali alikuwa na umri wa miaka 45.

Alikuwa hana elimu kama elimu inavyojulikana kwa kuwa hakusoma shule yoyote. Alipokuwa kijana mdogo baba yake alimpeleka Zanzibar kusoma elimu ya dini.

Wakati huo Zanzibar ilikuwa ndiyo kitovu cha elimu ya Kiislamu Afrika ya Mashariki na nchi jirani.

Huko Zanzibar kijana Mohamed Ali alisoma kwa Sheikh Mohamed L’Khamus. Kisha aliendelea na masomo yake mjini Dar es Salaam kwa Sheikh Wazir bin Said, mwanafunzi wa Sheikh maarufu sana na aliyekuwa Khalifa wa Tariqa ya Askariyya, Sheikh Idrissa bin Saad. Baada ya kumaliza masomo yake mjini Dar es Salaam alisafiri hadi Belgian Congo na halafu alirudi Ujiji nchini Tanganyika kufanya biashara ndogo ndogo.

Mwaka 1947 Mohamed Ali alirudi Lindi na kutoka hapo alikwenda Mikindani na kuwa fundi cherahani.

Msham Awadh alikuwa akijulikana Lindi nzima na Mikindani kwa sababu ya biashara yake. Mshama Awadh alikuwa alikuwa muuza uzuri, yaani vitu vya urembo kama vile uturi, dalia, marashi, rangi na manukato mengine kwa wanawake wa hii miji miwili.

Alikuwa akiuza bidhaa zake kikapuni akipita nyumba hadi nyumba. Hawa walikuwa ndiyo aina ya watu walioanzisha na kuongoza harakati za kumaliza utawala wa kikoloni.

Hawakuwa wajuzi wa lugha ya Kiingereza wala hawakuwa na ujuzi wa maisha ya ulimwengu wa Kimagharibi kama walivyokuwa baadhi ya Waafrika wengine waliyopata elimu ya Kimagharibi.

Msham Awadh na Ali Muhidin walikwenda hadi Dar es Salaam kukutana na Mwalimu Nyerere, John Rupia, Said Chamwenye, Oscar Kambona na Dossa Aziz katika makao makuu ya TANU, New Street.

Msham Awadh na Ali Muhidin walipewa kadi za TANU na wakaambiwa wafungue tawi Mikindani.

Wakati Msham Awadh na Ali Muhidin wakiwa njiani kwenda Dar es Salaam kukutana na Nyerere, Mohamed Ali alisafiri kwenda Lindi kukutana na Suleiman Masudi Mnonji mmoja wa viongozi wa TANU hapo mjini na kumweleza kuwa Mikindani walikuwa wamekusudia kufungua tawi la TANU.

Mnonji alimpa kadi Mohamed Ali na akawa mwanachama na akamwambia arudi Mikindani na kuanza kufanya kampeni kwa nguvu kwa ajili ya TANU na awafahamishe watu kuwa Nyerere yupo njiani kuja Jimbo la Kusini.

TANU Lindi walikuwa wamemualika Julius Nyerere kuja Lindi na katika ratiba yake alipangiwa kufika Mikindani. Nyerere, Ali Mwinyi Tambwe na Rajabu Diwani waliwasili Mikindani kutoka Lindi siku ya Jumamosi. Kabla ya kuwasili ujumbe huo, kazi kubwa kuliko zote waliyokuwanayo uongozi wa TANU Mikindani ilikuwa kutafuta mahali pa kumlaza Nyerere.

Walimwendea Ahmed Adam, Mnubi mmoja tajiri na mtu wa makamo, aliyemiliki nyumba moja ya fahari.

Nyumba hii ilikuwa ya ghorofa moja na ilijengwa kwa mawe na chokaa.

Ahmed Adam aliombwa awe mwenyeji wa Nyerere na ujumbe wake.

Nyumba hii tayari lilikuwa na kisa chake. Ilijengwa na hayati kaka yake Ahmed Adam baada ya Vita Kuu ya Kwanza.

Kaka yake alikuwa askari wa Kinubi aliyekuwa katika jeshi la Wajerumani.

Huenda alichukuliwa Misri mwishoni mwa mwa karne ya kumi na tisa na Wajerumani kuja Tanganyika kama mamluki katika jeshi la Wajerumani chini ya Kamanda Herman von Wissman.

Baada ya vita alilipwa kiinua mgongo na serikali ya Ujerumani na kwa kutumia fedha hizo alijenga nyumba hiyo.

Katika Vita Kuu ya Kwanza yeye alipigana katika jeshi la Wajerumani dhidi ya Waingereza chini ya Paul von Lettow Vorbeck.

Baada ya vita Wajerumani wakiwa wameshindwa vita, Waingereza waliitikadi nyumba hiyo kama mali ya adui wa himaya ya Kiingereza na kwa hiyo ilibidi itaifishwe.

Hii ilikuwa ndiyo nyumba pekee iliyokuwa nzuri yenye kumilikiwa na Mwafrika na kwa ajili hii haikuweza kukosa kuhusudika.

Utawala wa Waingereza ulikuwa katika taratibu ya kuitaifisha nyumba hiyo wakati ilipofahamika kwamba serikali isingeweza kufanya hivyo kwa sababu ya kifungu cha sheria ambacho kilisema kuwa mali ya Waafrika waliokuwa wakitumika katika majeshi ya watawala wao haiwezi kutaifishwa.

Hii ilinusuru nyumba hiyo na hivyo ilibakia mikononi mwa mwenyewe mpaka alipofariki na nyumba hiyo ikaja kuwa katika miliki ya mdogo wake, Ahmed Adam. Ahmed Adam alikubali kumpokea Nyerere na ugeni wake nyumbani kwake.

Nyumba hiyo ilikuja kuwa tawi la kwanza la TANU Mikindani.

Siku hiyo hiyo ya Jumamosi, usiku Nyerere aliitisha mkutano wa ndani wa wanachama wa TANU na wanachama kama 30 hivi walihudhuria.

Nyerere aliwaeleza kwa ufupi juu ya ile safari yake ya Umoja wa Mataifa na hali ya siasa kwa ujumla kama ilivyo mjini Dar es Salaam.

Nyerere aliwahakikishia wasikilizaji wake kuwa kulikuwa na uwezekano mkubwa sana kuwa Tanganyika itakuwa huru katika uhai wao.

Siku iliyofuatia mkutano wa hadhara ulifanyika mjini Mikindani mahali palipojulikana kama Jangwani, karibu na ufuko wa Bahari ya Hindi.

Mkutano huu uliohudhuriwa na watu wengi na uliendelea bila mushkeli wowote ukitoa kitendo kidogo kilichofanywa na mwalimu mmoja wa shule, Abdulrahman Muhibu aliyekuwa amelewa.

Muhibu alikuwa ametoka kunywa pombe na alipita karibu na uwanja wa mkutano ambapo Nyerere alikuwa akihutubia. Katika hali yake ya ulevi alimpigia kelele Nyerere akamwita muongo.

Huenda Muhibu alikuwa akifahamu vyema ujumbe wa Nyerere, na akiwa vile alivyokuwa, mtumishi wa serikali na mlevi, aliona wazo la mwalimu wa shule Mwafrika kama yeye kuwaongoza watu hadi uhuru upatikane ni jambo lisilowezekana.

Kwa haraka Muhibu alikamatwa na watu na ilikuwa karibu wamtie adabu ndipo Nyerere alipoingilia na hivyo kumnusuru.

Jioni hiyo baada ya mkutano Nyerere na ujumbe wake waliondoka kwenda Newala, kwenye ngome ya Yustino Mponda. Mponda alikuwa mmoja wa wajumbe wa Baraza la Kutunga Sheria waliosafirishwa na Gavana Edward Twining hadi Umoja wa Mataifa, New York, kumpinga Nyerere.

Sasa TANU ilikuwa ikichukua mkokoto wake wa kampeni hadi ndani ya ardhi ya Mponda ambayo yeye alikuwa liwali na mjumbe wa Baraza la Kutunga Sheria.

Nyerere alipomaliza ziara yake ya Jimbo la Kusini, fikra za watu wengi zilibadilika.

Tatizo kubwa kusini mwa Tanganyika kuhusu TANU ilikuwa Kanisa likiwaonya waumini wake kuchukua tahadhari na TANU kwani kanisa likiona harakati zile za kudai uhuru zilikuwa sawa na harakati zilizosababisha Vita Vya Maji Maji na kusababisha majemedari 62 wa vita vile kama Abdulrauf Songea Mbano kunyongwa na kuzikwa katika kaburi la halaiki Songea.

Kuja kwa Nyerere Wakristo waliokuwa wakitishwa na Kanisa hawakuamini tena kuwa TANU ilikuwa harakati za Waislam sawasawa na Vita Vya Maji Maji.

Nyerere, Tambwe na Diwani walipokuwa wanashika njia kurudi Dar es Salaam, matawi ya TANU yalikuwa tayari yamefunguliwa Masasi, Ndanda na Newala ambazo zilikuwa sehemu za Ukristo na ngome kuu ya Kanisa Katoliki katika Tanganyika.
Mzee una vitu adimu na muhimu sana kwenye historia ya nchi yetu
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom