Ahmad Rashad Ally ofisini kwa Jomo Kenyatta, Nairobi, 1963

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,896
30,234
AHMAD RASHAD ALLY OFISINI KWA JOMO KENYATTA NAIROBI 1963

Nimeeleza kuwa Ahmad Rashad alikuwapo siku Abdul Sykes alipokutana na Jomo Kenyatta Nairobi 1950.

Mzee Ahmad Rashad ana historia ndefu na ya kusisimua lakini hii tungoje siku nyingine In Shaa Allah.

Ahmad Rashad alikimbia Zanzibar baada ya kutokea matatizo yaliyosababisha yeye na mwenzake Ahmed Said Abdullah, maarufu kwa jina la Bamanga washitakiwe mahakamani kwa kesi ya siasa.

Vijana hawa wadogo wawili wote walikuwa wanatoka katika koo maarufu Zanzibar, Bakashmar na Kharusi.

Ushahidi ulikuwa hafifu dhidi yao wakaachiwa.

Rashad akaenda Bombay kisha Cairo kwa mipango maalum na Gamal Abdul Nasser wa Misri mwaka wa 1952.

Rais Nasser akampa Rashad kazi ya utangazaji katika Radio Free Africa, radio aliyoianzisha makhsusi kwa ajili ya ukombozi wa Afrika.

Pumu ilikuwa imepata mkohozi.

Ingekuwa msomaji wangu umebahatika kumjua Mzee Rashad ungenielewa kwa nini nimesema upele umepata kucha za mkunaji.

Ahmed Rashad katika miaka ile ya 1950 sauti yake kupitia Radio Free Africa ilikuwa maarufu Afrika ya Mashariki hasa Zanzibar ikihamasisha mapambano ya kuwatoa wakoloni wote Afrika.

Kabla ya kukimbia Zanzibar Ahmad Rashad Ali alikuwa mtangazaji maarufu Sauti ya Zanzibar.

Wapigania uhuru walikuwa wakipita Cairo Ahmad Rashad alikuwa akiwapa fursa za kuzungumza na dunia nzima.

Hii ndiyo sababu Jomo Kenyatta akamwalika katika sherehe za uhuru wa Kenya mwaka wa 1963 na akamwalika ofisini kwake.

Mzee Rashad kanieleza niko na yeye hadhir uso kwa macho.

Kenyatta alimkumbuka Rashad kuwa walionana mwaka akiwa na Abdul Sykes mwaka wa 1950.

Kenyatta alimshukuru Rashad kwa kazi yake aliyofanya kuisadia Kenya wakati yeye yuko kifungoni Kapenguria.

Katika zawadi ambazo Kenyatta alimpa Rashad ni tai yenye rangi za bendera ya Kenya.

Rashad akachukua fursa ile kumuombea msamaha rafiki yake mtangazaji mwenzake aliyekuwa kafukuzwa kazi Kenya Broadcasting Corporation (KBC).

Mzee Rashad anasema Kenyatta alimwambia kuwa amemsamehe kwa heshima yake Rashad anamrudisha kazini lakini yeye Rashad aende akamwambie aache upuuzi wake.

Screenshot_20211009-121838_Facebook.jpg

Picha ya kwanza kushoto ni Ahmad Rashad, Dr. Harith Ghassany na Mwandishi na picha ya pili wa pili kulia waliosimama ni Ahmed Said Abdullah.
 
AHMAD RASHAD ALLY OFISINI KWA JOMO KENYATTA NAIROBI 1963

Nimeeleza kuwa Ahmad Rashad alikuwapo siku Abdul Sykes alipokutana na Jomo Kenyatta Nairobi 1950.

Mzee Ahmad Rashad ana historia ndefu na ya kusisimua lakini hii tungoje siku nyingine In Shaa Allah.

Ahmad Rashad alikimbia Zanzibar baada ya kutokea matatizo yaliyosababisha yeye na mwenzake Ahmed Said Abdullah, maarufu kwa jina la Bamanga washitakiwe mahakamani kwa kesi ya siasa.

Vijana hawa wadogo wawili wote walikuwa wanatoka katika koo maarufu Zanzibar, Bakashmar na Kharusi.

Ushahidi ulikuwa hafifu dhidi yao wakaachiwa.

Rashad akaenda Bombay kisha Cairo kwa mipango maalum na Gamal Abdul Nasser wa Misri mwaka wa 1952.

Rais Nasser akampa Rashad kazi ya utangazaji katika Radio Free Africa, radio aliyoianzisha makhsusi kwa ajili ya ukombozi wa Afrika.

Pumu ilikuwa imepata mkohozi.

Ingekuwa msomaji wangu umebahatika kumjua Mzee Rashad ungenielewa kwa nini nimesema upele umepata kucha za mkunaji.

Ahmed Rashad katika miaka ile ya 1950 sauti yake kupitia Radio Free Africa ilikuwa maarufu Afrika ya Mashariki hasa Zanzibar ikihamasisha mapambano ya kuwatoa wakoloni wote Afrika.

Kabla ya kukimbia Zanzibar Ahmad Rashad Ali alikuwa mtangazaji maarufu Sauti ya Zanzibar.

Wapigania uhuru walikuwa wakipita Cairo Ahmad Rashad alikuwa akiwapa fursa za kuzungumza na dunia nzima.

Hii ndiyo sababu Jomo Kenyatta akamwalika katika sherehe za uhuru wa Kenya mwaka wa 1963 na akamwalika ofisini kwake.

Mzee Rashad kanieleza niko na yeye hadhir uso kwa macho.

Kenyatta alimkumbuka Rashad kuwa walionana akiwa na Abdul Sykes mwaka wa 1950.

Kenyatta alimshukuru Rashad kwa kazi yake aliyofanya kuisadia Kenya wakati yeye yuko kifungoni Kapenguria.

Katika zawadi ambazo Kenyatta alimpa Rashad ni tai yenye rangi za bendera ya Kenya.

Rashad akachukua fursa ile kumuombea msamaha rafiki yake mtangazaji mwenzake aliyekuwa kafukuzwa kazi Kenya Broadcasting Corporation (KBC).

Mzee Rashad anasema Kenyatta alimwambia kuwa amemsamehe kwa heshima yake Rashad anamrudisha kazini lakini yeye Rashad aende akamwambie aache upuuzi wake.

Screenshot_20211009-121838_Facebook.jpg
 
Ahsante kwa historia...
Smart...
Ikitokea fursa nitakuwekeeni hapa jinsi Ahmed Rashad alivyokuwa na ushawishi kwa Gamal Abdul Nasser kupitia kwa mshauri wake wa mambo ya Afrika Mohamed Faik na vipi aliweza kuisaidia Zanzibar.

Nilijifunza mengi kutoka kwa Mzee Rashad.
 
Itapendeza sana...
 
Back
Top Bottom