Ahadi Zetu Kabla Ya Kuoa/Kuolewa huwa ni tamu ila sasa baada

zagarinojo

JF-Expert Member
Jul 26, 2020
2,622
2,835
Mara nyingi kabla hatujaoa huwa tunafikiria kuhusu maisha ya ndoa yatakavyokua baada ya kuoa/kuolewa.

Huwa tunajinadi kama wagombea ubunge katika majimbo yao.

Ahadi kama vile "Mi nikishaoa siwezi mpiga mke wangu sipendi kupiga wanawake ntamkanya tu"

"Hata iweje siwezi kumsaliti (kuchepuka) mke wangu kipenzi"

"Ntakuwa namsaidia kazi za nyumbani asjione kama vile mfanyakazi tutapika wote na tutakula wote"

"Ntahakikisha namtimizia kila anachohitaji sitaki ateseke"


Baada ya ndoa nadhani huwa mchezo unabadilika ahadi kama vile zinafifia!

Kwa wanawake sijui ni ahadi gani huwa wanazifikiria kabla ya kuingia kwenye ndoa..

Au ndo Zile
"Ntahakikisha namtunza mume wangu"

"Ntampikia chakula kizuri siku zote"

"Ntampenda kuliko mwanaume yeyoye na sitomsaliti"

Vipi Ahadi Zako Kabla ya Ndoa umetimiza
Au ni zipi ahadi zako Kabla Ya Ndoa?
 
Inategemeana na mke/mume utakaye mpata, Kama akienda vile ulivyokua unamuwazia kichwan unaweza kutimiza ahadi hizo ila akienda kinyume unajikuta na ww unaenda kinyume tu!
 
Back
Top Bottom