Ahadi za wabunge nyakati za Uchaguzi na utekelezaji wake

Katibu Tarafa

JF-Expert Member
Feb 16, 2007
989
51
Nimekuwa nikipata wakati mgumu kujua hizi ahadi za wabunge wakati wa uchaguzi huwa zinatekelezwa vipi?
1.Kwa kutumia pesa zao wenyewe (mkono na shule jimboni kwake)
2.Ruzuku kutoka ktk chama anachotoka mgombea
3.kutokana na bajeti ya serikali

Kwa mwenye ufahamu anaweza kutupa mwangaza juu ya hii mada,ilituweze kujua kwa nini majimbo mengi yapo duni sana hata kama yanautajiri wa kutosha.
 
Kazi ya Mbunge uwakilishi wa wananchi, kuwakilisha Matatizo ya kimaendeleo ya wananchi serikalini ili yaweze kupatiwa ufumbuzi, mbunge kama mtu binafsi hana uwezo wa kuwaletea wananchi maendeleo endelevu hata Mkono mwenyewe hawezi, anaweza kujenga shule moja watoto wa jimbo lake wakasoma lakini hawezi kuinua uchumi wa kila mwananchi kwa juhudi zake binafsi. Kwahiyo ni serikali ndo inatakiwa kutekeleza ahdi za mbunge kwa wananchi. Ndo maana kuna wabunge masikini pia ambao hawawezi kujenga shule kama mkono wanachofanya ni kuwakilisha wananchi.

Swali lako ni la msingi sana, hata wananchi wa kwaida wanapaswa kufahamu, ili waondoe fikra kwamba maendeleo yanaletwa na mbunge binafsi na si serikali kupitia mbunge.
 
ahadi wanazotoa wakati mwingine ni kwa ajili ya kuupata tuu ubunge wenyewe kwa most of them

yaani inakuwa kuwa mbunge anatoa ahadi kibao kuwa atafanya hili atafanya lile ili mradi apate tuu ubunge ila hali halisi hakuna atakaloweza kufanya kutokana na mfuko wake zaidi ya kuomba serikali kuu imfikirie kwenye budget yake.
kama serikali haitakuwa na fungu la ahadi ilizotolewa na mbunge hapo ina maana kuwa inawezekana hata hiyo miaka mitano pamja na jimbo kuwa na rassilimali kibao likakosa maendeleo ya maana

kinachohitajika sio ahadi ila ile creativeness ya mbunge kwenye kubuni miradi ambayo rasilimali zake zinapatikana kwenye jimbo husika na sio kusubiri fungu kutoka serikalini ambalo halina uhakika
 
CS,
Kama wabunge hawana uwezo wa kutekeleza ahadi wanazotoa kwa wananchi,basi hilo ni kosa na ni udanganyifu ambao ni sawa na kugushi hati au taarifa ili kujipatia ajira.

Ni vipi serikali itaweza kutekeleza ahadi za wabunge wake ?au wabunge hutoa ahadi baada ya kupokea maelezo kutoka ktk chama anachokiwakilisha.
 
MR Rocky,
Hiyo miradi ambayo ataibuni ktk jimbo lake itagharamiwa na bajeti ipi,ya halimashauri usika au bajeti kuu ya serikali.

Kwa mtazamo wangu,bajeti ya serikali ingepangwa kutokana na mikoa na sio wizara kama ilivyo sasa ilikupunguza urasimu na kuongeza kasi ya maendeleao ktk mikoa husika.
Kwa maana hiyo wabunge wangeweza kusimamia vizuri pesa zinazotolewa ktk mikoa yao,tofauti na sasa ambapo bajeti inapangwa na wizara.kuna mikoa mingi sana ambayo haina maji salama ya bomba lakini inavianzo vingi vya maji.ni rahisi kutatua matatizo ya mkoa kuliko wizara
 
MR Rocky,
Hiyo miradi ambayo ataibuni ktk jimbo lake itagharamiwa na bajeti ipi,ya halimashauri usika au bajeti kuu ya serikali.

Kwa mtazamo wangu,bajeti ya serikali ingepangwa kutokana na mikoa na sio wizara kama ilivyo sasa ilikupunguza urasimu na kuongeza kasi ya maendeleao ktk mikoa husika.
Kwa maana hiyo wabunge wangeweza kusimamia vizuri pesa zinazotolewa ktk mikoa yao,tofauti na sasa ambapo bajeti inapangwa na wizara.kuna mikoa mingi sana ambayo haina maji salama ya bomba lakini inavianzo vingi vya maji.ni rahisi kutatua matatizo ya mkoa kuliko wizara


Katibu tarafa;

kuna mikoa ambayo ina rasilimali nyingi sana ambazo zinazalisha pato ambalo kama kungekuwa na utaratibu unaoeleweka lingekuwa ni mtaji mzuri sana kuinua pato la mtu mmoja mmoja kwa kila mkoa

hii ya kupangiwa budget na wizara hadi fungu lije litoke kwa kweli hapo hakuna kitu ni kuwadanganya wananchi
tufike mahali tuwaulize hao wabunge wanaoahidi hiki na kile kuwa hilo fungu watalipata wapi na sio wao waahidi na then wategemee serikali ifanye.

Vle vile Katibu Tarafa kuna vyanzo vingi sana vya mapato kwa baadhi ya mikoa ambavyo havifall under central government ambavyo kila mkoa ungevitumia kujiongezea kipato na kuanzisha miradi ambayo ni kwa faida ya mkoa na wananchi wanaoishi kwenye mkoa husika
 
Kwa mwenye ufahamu anaweza kutupa mwangaza juu ya hii mada,ilituweze kujua kwa nini majimbo mengi yapo duni sana hata kama yanautajiri wa kutosha

kinachohitajika sio ahadi ila ile creativeness ya mbunge kwenye kubuni miradi ambayo rasilimali zake zinapatikana kwenye jimbo husika na sio kusubiri fungu kutoka serikalini ambalo halina uhakika

Swali lako ni la msingi sana, hata wananchi wa kwaida wanapaswa kufahamu, ili waondoe fikra kwamba maendeleo yanaletwa na mbunge binafsi na si serikali kupitia mbunge.

Nakubaliana na watoa hoja kuwa tatizo kubwa kwa wabunge wetu wakati wa kampeni ni kutoa ahadi ambazo nyingi hazitekelezeki katika mazingira ya kawaida. Katibu Tarafa, wakati wa kampeni wabunge wengi wanaahidi kuwa watajenga shule, watajenga zahanati, watajenga barabara, wataleta maji na kadhalika, bila kufafanua kwa wananchi kuwa ni kwa namna gani watatekeleza hivyo vitu. Kimsingi inatakiwa wawaambie wananchi kuwa, kwa kushirikiana nao, watasababisha hayo maendeleo tajwa yatokee, kwa sababu bajeti ya nchi kama yetu haiwezi kuhudumia kila sekta kati ya hizo tajwa bila nguvu za wananchi. Kwamba bila ushiriki wa wananchi hayo maendeleo ni ndoto. Wabunge wanaogopa suala la kuwaambia wananchi kuwa watawashirikisha kwa sababu wanajua wananchi watahisi wanataka kuchangishwa hivyo hawatawapa kura zao, kwani kila mtu anajua adha ya michango.
Mrocky, nakubaliana na wewe kwa asilimia zote kuhusu ubunifu wa mbunge husika. Ni kazi ya mbunge kubuni miradi mbali mbali katika jimbo lake na kutumia fursa na rasilimali zilizopo kuwaletea maendeleo wanajimbo wake, wala sio suala la kuiachia serikali tu. Wabunge wengi wanaangalia namna watakavyofaidi mema ya nchi kwa faida zao, na si kwa faida ya wapiga kura wao. Shida inarudi pale pale kuwa wabunge wengi sio wawazi kwa sisi wapiga kura. Nimehudhuria mikutano mingi sana ya kampeni, sijasikia mara nyingi wabunge wakiongelea suala hili, zaidi ya kusifia sera za vyama vyao, ambazo aghalabu hazileti maendeleo yanayoonekana. Ili kutumia rasilimali zetu kwa maendeleo ya majimbo yetu tunahitaji "Enabling Environment" kutoka serikalini. Kwa jina lingine tunahitaji fursa tu! Fursa hizi ni zipi basi? Hizi ni miundombinu bora, sheria bora, ulinzi na usalama wa raia na mali zao na motisha za namna nyingine. Vitu hivi vikipatikana, inawezekana kabisa raia wakatumia fursa walizonazo katika maeneo yao kujiletea maendeleo, kwani watakuwa na uhakika wa kufanya kazi za uzalishaji mali pasipo bughudha. Na katika misingi ya utandawazi, serikali inabidi itoe fursa tu kwa wananchi.
Ikumbukwe kuwa wengi wa wapiga kura tunaowaongelea hapa ni wale asilimia 80 ambao wanaishi vijijini, ambao hata mlo mmoja kwa wengi wao ni shida kuupata. Sasa hawa ndio wanalishwa propaganda na wabunge kuwa maendeleo yataletwa na wabunge. Ukiwaambia wachangie jengo la shule wanasema hawawezi kufanya ivyo kwa kuwa mbunge aliahidi kutekeleza! Hii ndio sura halisi ya wabunge wetu walio wengi.
 
Mtu Pori kuwa mbunge sio sera wala kumwaga blah blah pale jukwaani ila ni kutoa kile ambacho utawafanyia wananchi wako ukishapata kurta za wananchi wako. Sio kuwadanganya kuwa nitawajengea barabara, shule, hospitali, sijui nini na nini wakati huna mpango hujacreate something new ambacho kinazalisha au kinaweza kuwa mradi au hilo fungu linatoka wapi

mbinu moja nzuri ni kwa wananchi kuwauliza hawa majenerali wetu wanapotoa ahadi hizo fungu mnalipata wapi na jingine kama aliomba miaka mitano yake na akamaliza miaka mitano yake hajafanya katika yale aliyooahidi kuwa atafanya hakuna kumpa kura awe mbunge tena kwa kipindi kingine tena mnamwambia wazi kabisa hatukutaki na hutufai maana umeshindwa kututengenezea hata mradi mmoja wa kutuongezea kipato kuna vyanzo vya maji hapa kwetu umeshindwa kutupatia hata maji ya kunywa yaani hapa tunahitaji wabunge walio tayari kutufanyia kazi na sio kula kwa migongo yetu wananchi tena
 
Kwa hiyo ninachojifunza hapa ni kuwa wananchi wengi hawajui upande wa pili wa shilingi ambao ndio mbunge wao.kwa hiyo sio busara kwa wabunge kutoa ahadi za uongo kama wafanyavyo sasa,badala yake wawe wakweli kwa wapiga kura wao kwa kuwaambia ukweli.je hii elimu ya kuwaelimisha wananchi juu ya haki zao ni ya nani?

Kuhusu rasilimali ktk majimbo husika au mikoa husika,nilisoma zamani goverment accounting ni kuwa kuna kiwango cha pesa ambacho mkoa au halimashauri inapaswa kuwanacho kwa shughuli zao za maendeleo na hakitakiwi kuzidi hapo (mfono laki tano kwa hiyo makusanyo yanayozidi laki tano yanatakiwa yapelekwe hazina)halafu kama wanataka pesa kwa ajili ya mradi fulani inabidi waombe tena kwenye wizara husika.

Kwa mindo huu ndio maana tumekuwa tukirudi nyuma ktk maendeleo siku hata siku.
kuna miradi mingi ambayo wananchi wanaweza kuifanya ilikujiletea maendeleo yao lakini wanakwamishwa na sheria kandanizi za serikali bila kuwa na manufaa kwa wananchi husika.
 
Katibu tarafa,

ndo maana tunalilia kuwa kama ni masuala ya maendeleo kila mko uwe na fungu au hata kama ni kiwango kiwekwe wazi kijulikane kuwa kila mkoa una fungu la kiasi kadhaa kwa ajili ya maendeleo na sio kusubiri fungu kutoka central government na ambalo linatokana na rasilimali zilizopo kwenye mkoa wenyewe.

Kuhusu wabunge inabidi tufikie sehem ya kusema no kwa mbunge antakayetupa ahadi wakati tunajua hana source yoyote ya kipato na yule anayeshindwa kutimiza kile alichoahidi asichaguliwe tena kuwa mbunge.

Elimu ya uraia ni kazi ya serikali kuwaelimisha wananchi kuhusu haki zao wajibu wao kama raia wa tanzania na nini wategemee kutoka serikalini na serikali inahitajika iwafanyie nini wananchi wake. ni kazi ya serikali kuwaelezea wananchi wake jukumu la raia kwa viongozi na jukumu la kiongozi kwa raia

ila naomba tuu nikuambie kuwa hilo halifanyiki kwa sababu serikali ikifanya hivyo itawaamsha wananchi waliolala wajue haki zao na haki za kiraia na hapo ni kama hii ya sasa ya kuwazomea viongozi maana washajua kuwa watu hawa ni wababaishaji tuu hakuna lolote wanalofanya
 
Serikali ya ccm haiwezi kukubali hilo,ni sawa na kutia mchanga kitumbua chao.ndio maana hata sasa wanapoinadi hiyo bajeti hawasemi itawasaidiaje wananchi zaidi ya kusema tunajenga vyumba vya madarasa.
 
Kuhusu rasilimali ktk majimbo husika au mikoa husika,nilisoma zamani goverment accounting ni kuwa kuna kiwango cha pesa ambacho mkoa au halimashauri inapaswa kuwanacho kwa shughuli zao za maendeleo na hakitakiwi kuzidi hapo (mfono laki tano kwa hiyo makusanyo yanayozidi laki tano yanatakiwa yapelekwe hazina)halafu kama wanataka pesa kwa ajili ya mradi fulani inabidi waombe tena kwenye wizara husika.

Ndio leo nasikia kitu cha namna hii. Nadhani hii ndio inarudisha nyuma maendeleo. Lakini mantiki ya kuweka limit ya pesa ni ipi lakini?
 
Na hapo ndipo penye matatizo,hilo swala sio geni ulizia tu kwa watendaji wa mikoa watakuwambia kwa sasa ni kiasi gani sijui.na kama utakumbuka zamani pia sukari inazalishwa kagera lakini huwezi kununua mpaka ifikishwa dar ndipo hianze kusabazwa na yale maduka ya rtc
 
Back
Top Bottom