Ahadi za uchaguzi kuhusiana na Afya zimeanza kutekelezwa??

measkron

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
3,782
2,406
Nakumbuka wakati wa kampeni za uchaguzi Kikwete akiongea na wazee wa Dar es salaam alisema kwa mtandao wa internet anataka Hospitali ya Taifa Muhimbili mgonjwa akiwa anafanyiwa upasuaji dakatari anaweza akawa anaongozwa na daktari super specialist kutoka Calofrnia akisema, kata hapa.... kata pale... hata kushauriana na wataalam wengine wa Afya popote duniani kujadili shida ya mgonjes kwa kutumia internet.. hizo fiber wire za internet zimeishia wapi??? na kwa matatizo ya umeme ahadi hii itatimia??
Pia alisema ameikarabati sana idara ya meno pale muhimbili na mwanae ambaye ni Daktari wa meno pale muhimbili kila mara alikuwa akimlalamikia kuhusu uchakavu wa majengo na huduma duni ikiwa ni ukosefu wa vifaa tiba katika idara hiyo hivyo akatafuta wafadhili na ikakarabatiwa na sasa in the best denntal department nchi nzima.. swali ni je walio madakari wa upasuaji, kina mama na uzazi, watoto, wagonjwa wa akili, mifupa, macho wao sio watoto wa mheshimiwa je wakalalamike kwa nani ili idara zao zikumbukwe kufanyiwa ukarabati na vifaa tiba kununuliwa?
Tumeshuhudia juzi juzi madaktari bingwa wakihamishwa kupitia gazeti kwenda mikoani, je wizara ya Afya imeandaa idara za hawa madaktari bingwa kwenda kuzifanyia kazi kutokana na fani zao? tusishangae wanawapeleka halafu hospitali hazina vifaa mwishowe wanaishia kwenda kufungua viduka vya dawa na kufanya tiba vituo binafsi kwa gharama ambazo watanzania wengi hawatamudu...... Nadhani watanzania wengi wanahitaji basic medical services na sio kuanza kuwaza operation ya kuwa monitored na mtaalam toka California.. wana jf mnasemaje?
 
Back
Top Bottom