Ahadi za Slaa hazitekelezeki! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ahadi za Slaa hazitekelezeki!

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Kalunguine, Oct 20, 2010.

 1. Kalunguine

  Kalunguine JF-Expert Member

  #1
  Oct 20, 2010
  Joined: Jul 27, 2010
  Messages: 2,544
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  AHADI zinazotolewa na baadhi ya wagombea uongozi nchini katika kampeni zinazoendelea za uchaguzi mkuu zikitekelezwa, huenda zikawaweka Watanzania pabaya, imebainika.

  Taarifa ya kitaalamu imebaini, kwamba kuna wagombea urais ambao wamekuwa wakiwaahidi Watanzania kuondoa kodi katika saruji watakapochaguliwa kuingia Ikulu.

  Taarifa ya Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki, iliyotolewa jana na Waziri mwenye dhamana, Dk Diodorus Kamala, ilisema ahadi hiyo inapotosha wananchi na kuwapa matumaini ambayo hayatekelezeki.

  Alisema chini ya kifungu 2(4)(c) cha Itifaki ya Umoja wa Forodha wa Afrika Mashariki, nchi wanachama zilikubaliana kuweka na kutekeleza wigo wa pamoja wa ushuru wa forodha kwa bidhaa zitokazo nje ya Jumuiya.

  Aliongeza kuwa wigo huo ulianza kutekelezwa Januari mosi, 2005 na viwango vilivyokubalika ni asilimia 0 kwa malighafi, pembejeo za kilimo, dawa na mitambo; asilimia 10 kwa bidhaa zilizosindikwa kiasi; na asilimia 25 kwa bidhaa zilizokamilika katika uzalishaji.

  Kamala alisema, bidhaa nyeti ushuru wake ni zaidi ya asilimia 25.

  “Hivyo nchi binafsi mwanachama haina mamlaka ya kurekebisha viwango vya kodi ya forodha … mfumo wa uamuzi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) hauruhusu nchi moja mwanachama, kufuta ushuru wa forodha wa bidhaa ya aina yoyote ile, ikiwamo saruji.”

  Alisema, kuwaahidi wananchi jambo ambalo halijakubaliwa na viongozi wa nchi zingine wanachama ni kuwadanganya. “Kwa kawaida muungana na mkweli, hatoi ahadi ya jambo ambalo uamuzi au utekelezaji wake unategemea ridhaa ya mamlaka nyingine iliyo juu yake.”

  Alihoji: “Je, ombi la kufuta ushuru likikataliwa na nchi zingine wanachama itakuwaje? Je, mhusika atawarudia wapiga kura na kuwaambia kuwa alitoa ahadi hewa au isiyo na mantiki?”

  Alisema, saruji ni miongoni mwa bidhaa zilizowekwa katika kundi la bidhaa nyeti, ambazo wazalishaji wa nchi zinakotoka, hupewa ruzuku ambapo wazalishaji wa EAC hawapewi ruzuku hiyo, lakini wanaweza kuzalisha kwa ufanisi.

  Hatua hiyo alisema kuwa inachangia katika maendeleo ya viwanda, ajira, mapato ya Serikali na kuokoa fedha za kigeni, ambapo pia kuweko kwa ruzuku kwa wazalishaji wa nje huku wa ndani wakikosa, kunaweka mazingira ya ushindani usio sawa katika soko la Jumuiya dhidi ya wazalishaji wa Afrika Mashariki.

  Alisisitiza, kwamba kwa upande wa saruji, kuanzia Januari mosi 2005 ushuru wake ni asilimia 55 na nchi wanachama zilikubaliana ushuru huo ushuke kila mwaka hadi asilimia 35 kuanzia Januari mwaka huu na ubaki katika kiwango hicho.

  Alitaja bidhaa zingine katika kundi hili na kiwango cha ushuru kwenye mabano, kuwa ni sukari (100%), mahindi (50%), ngano (35%), mchele (75%), maziwa (60%), tumbaku (35%), sigara (35%), khanga, kikoi, kitenge (50%), mashuka (50%), magunia ya jute (50%), viberiti na betri za redio (35%).

  “Kwa hiyo kufutwa ushuru si tu kutasababisha viwanda kufa, lakini mapato ya serikali na ajira vitapungua sambamba na uanachama wa Tanzania katika Jumuiya kuwa shakani.

  “Sina hakika kama misamaha ya kodi inaendana na ahadi dhaifu za elimu na afya bure kwa Watanzania zinazotolewa na wapinzani.

  Huwezi kutoa elimu bure na afya bure na wakati huo huo, usamehe ushuru wa forodha,” alisema Kamala.

  Alisisitiza pia kuwa, hatua ya kupunguza ushuru wa forodha kwenye saruji ilichukuliwa kitambo, lakini kufutwa kukashindikana kutokana na hali halisi iliyobainishwa awali.

  “Mwaka 2005 ushuru ulikuwa asilimia 55 ukapunguzwa hadi asilimia 25 ya sasa … hatua hii ilichukuliwa kutokana na maandalizi ya Kombe la Dunia, Afrika Kusini na Olimpiki, China.

  Alisema, wakati huu ambao ushuru kwa muda umeshushwa hadi asilimia 25 huku ikifikiriwa kama utarejea asilimia 35, tayari wazalishaji saruji wameanza kulalamika kuwa wenzao wa nje hususan Misri, wanapata ruzuku na hivyo kuiuza kwa bei ndogo katika Jumuiya.

  “Kwa maana hiyo kufutwa kabisa kwa ushuru, kutasababisha viwanda kufa na dhana ya kuwapa wananchi saruji ya bei nafuu kufa pia … bei ya bidhaa yoyote duniani, hutegemea upatikanaji wake na mahitaji ya soko.

  “Pindi viwanda vya saruji vya Afrika Mashariki vikifa, wazalishaji kutoka nje ya Jumuiya, watashawishika kupandisha bei, kwa kuwa sasa watakuwa wamejengewa ukiritimba katika soko kwa kukosa mpinzani wa ndani,” alisema Waziri.

  Katika kampeni zake nchini, mgombea urais kwa tiketi ya Chadema, Dk Willibrod Slaa, amekuwa akiwaahidi wananchi kuwa akiingia Ikulu atapunguza bei ya saruji hadi Sh 5,000 kwa mfuko wa kilo 50, ili wananchi wajijengee nyumba bora za kisasa.


  CHANZO: habari leo tarehe 20/10/2010
   
 2. Saharavoice

  Saharavoice JF-Expert Member

  #2
  Oct 20, 2010
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 2,644
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Hivi Serikali nayo imeamua kufanya Kampeni?
  Hivi Watanzania sisi ni majuha kiasi hicho? kwamba hatuwezi kubadili sera zetu za maendeleo kwa kisingizio cha umoja wa forodha wa EAC?
  This is very shame, very shame, very shame.
  Sikutarajia statement ya aina hii kutoka kwa mtu eti Dr. Kamala. kukariri bila kuelimika.
   
 3. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #3
  Oct 20, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Mafisadi wamewashika yoote yanawezekana ni MALENGO, Ila naona ccm imewauma kweli bcs DR kashika pale ambapo wananchi wanapataka, siyo mafisadi. leo nilikuwa nasikiliza Redio Moja hv wanasema serilikali inataka kutazama bei za vifaa vya ujenzi eeti hawajui kama vinapanda watafanya uchunguzi duuuuu!
   
 4. Eliphaz the Temanite

  Eliphaz the Temanite JF-Expert Member

  #4
  Oct 20, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,836
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Limbukeni huyo! Maelezo ya Ki-layman kabisa! Ina maana serikali haiwezi kupunguza ushuru kwa wananchi wake kwa kisingizio cha EAC! What a crap!
   
 5. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #5
  Oct 20, 2010
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,525
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Watu wa jimbo la Kamala wana akili sana. Hawakusita kumpiga chini na sababu mmojawapo ni utupu kama huu.Eti tukipunguza bei ya Cement yaet hadi Kenya ,Uganda et al wakubali. Sijawahi kusikia upupu kama huu. Ndio hilo alilopeleka huko EAC? Kama Waziri ndiye huyu huko EAC basi we are finished.

  Tarehe 1/11/2010 atakuwa parmenent bench na cement itashushwa tuone kama hao wakenya wanauwezo wa kuzuia.
   
 6. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #6
  Oct 20, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Ha ha haa!! Kalunguine unatuletea habari za kwenye magazeti ya udaku? Hayo magazeti wanasoma watoto wa shule na yanawasaidia sana akina maama kufungia maandazi na mihogo. Siyo gazeti la kusoma mtu mwenye akili timamu.
   
 7. Who Cares?

  Who Cares? JF-Expert Member

  #7
  Oct 20, 2010
  Joined: Jul 11, 2008
  Messages: 3,465
  Likes Received: 1,950
  Trophy Points: 280
  YOOTE YANAWEZEKANA...ndio maana hata hiyo EAC wengi wetu huwa hatuikubali..ni upuuzi NA KWA KUANZA KUONYESHA KUWA INAWEZEKANA NI PAMOJA NA KUPUNGUZA MATUMIZI YA SERIKALI KWA KUUA WIZARA YA HUYO KAMALA MAANA NI DEPARTMENT KWENYE WIZARA ALIYOKO MEMBE...PILI NI KUJITOA EAC MAANA NAYO INAONEKANA MZIGO WA MISUMARI MAANA HATUJUI TUNAUZA NINI NA KUINGIZA KWETU NINI...TUNAKAA SADC....

  waambie yote anayoyaahidi rais mtarajiwa dr. slaa yanawezekana na inshaalllaaaaahhh MUNGU ATAKUWA NAYE MAAANA IMEANDIKWA NAYAWEZA YOTE HAYA KWAKE YEYE ANITIAYE NGUVU....na waambie wenzao kuwa "HATA TUJAPOPITA KATI YA BONDE LA UVULI WA MAUTI HATUTOOGOPA MABAYA KWA MAANA BWANA YEYE YUU PAMOJA NASI"....naamini mumetuelewa how determined we are this time....
   
 8. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #8
  Oct 20, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280
  Hata Iweje,kanisa Katoliki Haliwezi Kuniambia Nimchague Slaa!! 2010 Hatugawanyiki!!

  Hata Iweje,Waislamu hata waoe wake 100 kila mmoja wenu, hamtaliyumbisha Kanisa Katoliki. Hatugawanyiki!!
   
 9. L

  Lorah JF-Expert Member

  #9
  Oct 20, 2010
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 1,193
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  halafu anaongelea Viwanda vipi eti jamani, vile ambavyo wameviua vyoteeee..

  Mwenzenu nachoka...
  Bora Silaa ana vision kuliko huyo anaepita kutangaza maendeleo ni shule za kata ambazo hazina walimu

  siku hizi hata mwanakijiji wa ndani kabisa anajua kumpeleka mwanao shule ya KATA ni kumharibia maisha....
   
 10. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #10
  Oct 20, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  unategemea nini serikali imejaa wacheza viduku...maneno ya kipumbavu kabisa serikali kutuambia eti inafanya uchunguzi
   
 11. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #11
  Oct 20, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Ndio maana kapigwa chini jimboni kwake !! Wasomi wa nchi hii wanefunikwa na siasa.
   
 12. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #12
  Oct 20, 2010
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Dk Slaa anasma Tanzania kwanza, wageni baadaye. Tanzania si Afrika Mashariki bali ni sehemu ya Jumuiya hiyo, hatuklazimishwa kujiunga na wala EAC haiwezi kutupangia mustakabali wetu.
   
 13. M

  Mbalinga JF-Expert Member

  #13
  Oct 20, 2010
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 1,382
  Likes Received: 408
  Trophy Points: 180
  Napenda kumwambia Kamala kuwa TANZANIA KWANZA, EAC BAADAYE. Msianze kutuzingua hapa, kama kuna makubaliano ccm imeingia yanayomrudisha nyuma na kumdidimiza Mtanzania yatafutwa. Mikataba yote itafumuliwa ili Mtanzania anufaike. Kipi bora kumfanya Mtanzania ajenge nyumba bora kwa urahisi ama kumuweka kwenye jumuia isiyo na faida kwake ya haraka. 2010 tunasema HATUDANGANYIKI.
   
 14. Power to the People

  Power to the People JF-Expert Member

  #14
  Oct 20, 2010
  Joined: Jul 11, 2007
  Messages: 1,193
  Likes Received: 238
  Trophy Points: 160
  Anayejua bei za cement katika nchi za Afika mashariki atuwekee hapa ili tuone tofauti.
   
 15. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #15
  Oct 20, 2010
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Bei ya Cement ya Kenya ni rahisi kuliko ya hapa Tanzania, hapa Arusha wameshaanza kuifanyia marketing cement ya Kenys. Nilikwena Musoma mwaka jana bei ya Cement ya Kenya iko chini kuliko ya Tanzania. Labda wao Kenya waliomba kibali cha kushusha ushuru wa cement yao EAC.
   
 16. The Invincible

  The Invincible JF-Expert Member

  #16
  Oct 20, 2010
  Joined: May 6, 2006
  Messages: 4,723
  Likes Received: 1,213
  Trophy Points: 280
  Huyu Kamala ni kihiyo tu, na udokta wake wa kinajimu.
   
 17. Kalunguine

  Kalunguine JF-Expert Member

  #17
  Oct 20, 2010
  Joined: Jul 27, 2010
  Messages: 2,544
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  hahahaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!!! Mapadre wamebakaaaaaaaaaaaaa,wakalawitiiiiiiiiiiiiiiiiii,sasa wanaamua kuutaka urais,naapa kwa jina la mungu aliye hai daima,na kwa kuutumia uwingi wetu nchi,hasa ukizingatia wengine tuna wake wawili ,watatu,na wanne,kampenzi zetu ni za kitanda kwa kitanda,kura za waislamu mwaka huu only ni kwa ajili ya maslahi ya dini yetu,na si vinginevyo

  mwaka kesho mwezi huu tunazungumzia habari ya kadhi na oic si habari ya padre kutaka ikulu,akafungue makanisa kule karatu
   
 18. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #18
  Oct 20, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,944
  Likes Received: 2,091
  Trophy Points: 280
  Kwanza inasemekana PhD yake haina viwango. Pili kwa mijitu mizima mivivu ya kufikiri na mijizi lazima ione kuwa haiwezekani. Wanashindwa kuelewa kuwa serikali itakuwa ina - subsidise!
   
 19. L

  Lorah JF-Expert Member

  #19
  Oct 20, 2010
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 1,193
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0

  WALIOISHIWA SERA WANAKUWA KAMA IFUATAVYO  hivi Mwalimu Julius Kambaraghe Nyerere alikuwaga Mwisilamu eheeeeeeee- hivi ni kumbeeeeeeeee....... na Mkapa alikuwa Mwisilamu eheeeeeeee
  Ni kanisa Katoliki ndo lililosema tuwachague eheeeeeeeeee duh

  hivi Kikwete alisomeshwa na wakatoliki eheeeeeeeee, na Makamba eheeeeeeeeee

  hivi wachaga ndo wamenynyua uchumi wa Tanzania eheeeeeeeeee so ni wajanja nchi itakuwa kama ulaya eheeeeeeeeeeeeee

  hivi wakristo wengi ndo wenye uelewa eheeeeeeeee na wamejiandikisha kwa wingiiii eheeeeeeeeee
  hivi Kikwete ni Mweupe mweupe eheeeeeeeeeee bora Lipumba ni mwafirika halisi eheeeeeeeeee
  Hivi Nyerere alikuwa Mrefuuuuuuu eheeeeeeeee kama Lipumba eheeeeeeeeee kikwete mfupi eheeeeeeeeeeeeeee

  Hivi walioongoza miaka yote iliyopita ni wasomi eheeeeeeeeee sasa kuwe na vita vya wasomi na wasiosomaaaaaaaaaaa

  au vita vya walionacho na wasionacho eheeeeeeeeeeeeee
  Matajir wengi wako CCM eheeeeeeeeee kwa Hiyo masikini wengi wako CAF au?????

  hatuhitaji huu ujinga ...............TAFAKARI CHUKUA HATUA
   
 20. m

  manunuzi Member

  #20
  Oct 20, 2010
  Joined: Sep 5, 2008
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Hiyo PHD ya Kamala ni ya bei za Cement au ya kitu gani? Ninavyojua mimi unavyozidi kusoma na kupata PHD unakuwa mjinga wa mambo mengi na mwerevu wa jambo moja tu uliliochukulia PHD,labda mwenzetu anadhihirisha ukweli huo.
   
Loading...