Kingcobra
JF-Expert Member
- Jan 28, 2011
- 1,000
- 309
Wakuu,
Kwa muda mrefu sasa, wabunge wengi wanapochangia hoja za mawaziri wanaowasilisha bajeti zao bungeni wamekuwa wakiwalaumu mawaziri kwa kutotekeleza ahadi za serikali kwenye majimbo yao. Wengine hutia uzito wa hoja zao kwa kukumbusha kwamba baadhi ya ahadi alitoa mkuu wa nchi kwa maana ya rais Dr. Jakaya Kikwete na wanawashangaa mawaziri kwa kukaidi kutekeleza ahadi za kiongozi mkuu wa nchi.
Ninachojiuliza ni je, hivi wa kulaumiwa ni nani, ni mawaziri au rais mwenyewe anayeahidi na kusahau palepale yaani baada ya hapo hafuatilii tena utekelezaji wake? Kama wa kumlaumu ni waziri, je, rais kabla ya kuahidi kuwa anawasiliana na mawaziri wake kabla ili ajiridhishe na uwezekano wa kutekelezaji anachokusudia kuahidi? Kama sivyo, kwa nini lawama zielekezwe kwa waziri na siyo rais mwenyewe. Tafadhali wataalam mtujuze hapa.