Ahadi za Rais Magufuli kuhusu uchaguzi huru na haki hazitekelezeki, ni ahadi hewa kimazingira

Hivi karibuni Rais JPM alipozungumza na Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao pamoja na mambo mengine alitoa ahadi ya kufanyika uchaguzi huru na haki mwaka huu wa 2020 jambo lililoleta mjadala sana kwenye jamii.

Hii kauli haitekelezeki kwa sasa. Hakuna mazingira ya kufanyika uchaguzi huru na haki.

Kumekuwa na malalamiko ya muda mrefu kwamba muundo wa Tume ya UCHAGUZI SIO HURU, mfumo wetu ambapo mwenyekiti wa Chama Tawala ( CCM ) ambae ni Rais ndio huchagua Mwenyekiti na Mkurugenzi wake, na Maofisa kuwajibika moja kwa Serikalini ndio tatizo la kwanza. Hali hio tu basi inatosha kuufanya uchaguzi usiwe huru na haki. Mwenyekiti na Mkurugenzi wanapokea maagizo moja kwa moja kutoka kwa Mwenyekiti wa CCM. Hakuna HATUA YOYOTE YA KUUNDWA tume huru hadi sasa.

Kumekuwa na malalamiko ya muda mrefu ya kuondolewa wakurugenzi wa Halmashauri na manispaa kuwa wasimamiaji wa chaguzi kwenye ngazi ya Jimbo na wqilaya kutokana na kuwa ni wakereketwa wa chama Tawala. Imefika mahali hadi mahakama ikataka wazuiwe lakini chama TAWALA NA TUME WAMEENDELEA KUWATUMIA KWA MASLAHI YAO. Huu ni ushahidi mwengine kwamba hakuwezekani kukawa na Uchaguzi huru na Haki kwa sasa. Vitimbi vya karibuni vya Wakurugenzi hawa kujificha na kufanya figisu kwa wapinzani ni dhahiri hakuwezekani kufanyika uchaguzi huru na haki.

Serikali ya JPM kulea uhuni wa watendaji waliovuruga chaguzi tena wazi wazi kuanzia zile za marejeo na za serikali za mitaa ni ishara nyengine kwamba hakuna utashi na hakuna uwezekano wa kufanyika uchaguzi huru na haki.

Kwa ufupi wa maneno instrumentally, hakuna mazingira ya kufanyika uchaguzi huru na haki na vile vile kiutashi na kimadaraka kwa utawala uliopo hilo haliwezekani.

Hali hio haiko kwa Bara wala Zanzibar. Wakati Zanzibar kuna Malalamikoi ya uandikishaji tayari na hakuna hatua yoyote iliyo wazi ya kutatua tatizo basi tayari ni ushahidi kwamba hiyo ahadi ya Uchaguzi huru na Haki imeshafeli.

WATANZANIA WANASUBIRI AHADI ZA RAIS MAGUFULI.
Watu wanasubiri viashiria walau, JPM atathubutu kupeleka mswaada wa kuundwa Tume Huru wakati huu?

Je, wadau watashirikishwa muundo wa Tume unaotakiwa na kuridhiwa na wote?

Je, wakurugenzi wa Halmashauri na tarafa wataondolewa kuwa wasimamiaji wa chaguzi.

Muda ndio utaongea lakini ni wazi mazingira ya SASA HAYARUHUSU KUFANYIKA UCHAGUZI HURU NA HAKI.

Kishada.
Mie naungana nawe, ila naulaumu upinzani muda wote toka katiba mpya ilipokwama, katiba hile ilikuwa na mapungufu hasa ya muundo wa serikali kama moja,mbili au tatu, wenye nguvu walitaka mbili, lakini tume huru ilipatikana na walikubaliana, wangeridhia serikali mbili na tume huru hatua ingekuwa imepigwa na ni kubwa, baadae wangeshughulika na muundo,uwenda tume huru ingetoa matokea ya kweli ya kura na aidha bara au visiwani kungekuwa na upinzani nao ungeongoza kudai muundo wa serikali wanaoukusudia, sasa mkaleta utoto wa kususia na mambo ndio yakaishia pale, leo eti inatakiwa tume huru, sijui mswada wa dharura kwa kiongozi ambae anajinadi si kipaumbele chake na hakuhaidi wapiga kura, tujitambue, na ikitokea nafasi kama ile tukumbuke heri kidogo kidogo ndio mwendo.
 
Mkuu wewe unaamini kutakuwa na uchaguzi huru na haki kwa mazingira yaliyopo?
Hakuna kitu kama hicho.

Ninachosema kwa jinsi alivyosema kwa kiasi flani anakiri kuwa hakuna uchaguzi wa Huru na Haki Tanzania ...!!
 
Hakuna kitu kama hicho.

Ninachosema kwa jinsi alivyosema kwa kiasi flani anakiri kuwa hakuna uchaguzi wa Huru na Haki Tanzania ...!!
Pamoja na kukiri lakini ahadi ya kuwepo uchaguzi huru na Haki kwa mazingira ya sasa haiwezekani.
 
Mie naungana nawe, ila naulaumu upinzani muda wote toka katiba mpya ilipokwama, katiba hile ilikuwa na mapungufu hasa ya muundo wa serikali kama moja,mbili au tatu, wenye nguvu walitaka mbili, lakini tume huru ilipatikana na walikubaliana, wangeridhia serikali mbili na tume huru hatua ingekuwa imepigwa na ni kubwa, baadae wangeshughulika na muundo,uwenda tume huru ingetoa matokea ya kweli ya kura na aidha bara au visiwani kungekuwa na upinzani nao ungeongoza kudai muundo wa serikali wanaoukusudia, sasa mkaleta utoto wa kususia na mambo ndio yakaishia pale, leo eti inatakiwa tume huru, sijui mswada wa dharura kwa kiongozi ambae anajinadi si kipaumbele chake na hakuhaidi wapiga kura, tujitambue, na ikitokea nafasi kama ile tukumbuke heri kidogo kidogo ndio mwendo.
Kwa hiyo unakubali kuwa ahadi ya uchaguzi huru na haki ni hewa si ndio?
 
Wananchi wa tanzania wanaishi vifungo vya nje,askar magereza ndio hao chama tawala,😆
 
Back
Top Bottom